ng`wana ong`wa kulwa
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 2,420
- 1,755
hawakuongezewa mishaharabinafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini wachangiaji katika jukwaa hili ni wachache? Lakini kwa uchunguzi wangu nimekuja kugundua kuwa watu wenye uwezo wa kuchangia jukwaa hili ni wengi sana.kilicho nishitua zaidi ni id.za watu niliowajua waliokuwa wakitoa michango yao mizuri wameipa kisogo site hii utaona wakichangia kwenye jukwaa la siasa nk.
Kwa mawazo mengine mtu mwingine anaweza kusema ma doctor ni wachache na wataalamu wengine wa afya ni wachache kitu ambacho si kweli maana kuna wengine wana uwezo wa ku google na kutoa mchango wao vizuri sana.
Nilichogundua mimi pamoja na wewe unakaribishwa kutoa maoni yako nini ila nilichoona ni kuwa watu wengi wanapo post shida zao jf doctor wanaondoka,kama mjuavyo kuna mambo mengi kabla hujaanza kumshauri mtu nini cha kufanya, mfano unaweza taka kujua uzito,umri maana dawa nyingi zinatumika kulingana na kilo za mgonjwa,sasa wataalamu wakiuliza unakuta muulizaji hajibu chochote.mbona majukwaa ya mahusiano,siasa wengi wanaopost hutulia kuangalia michango na kujibu maswali huku si zaidi sana maana inahusiana na uhai.
Kutokana na hili wengi wameona ni kupoteza muda unataka kumsaidia mtu asiyekuwepo kukujibu hata maswali ya msingi,kumbuka muda anaokusaidia huenda kuna mgonjwa amemuomba asubiri kidogo huku akikujibu wewe uliyepost.
Kabla sijakukaribisha wewe kwa mchango wako niombe wataalamu turudi tusaidie wadau angalau wale wanaokuwepo kujibu maswali tusikimbie jukwaa hili.
Bado naisoma tena na tena lakini sijapata ujumbe uliodhamiriwa.
Inaweza kuwa vizuri iwapo utai-rephrase hoja uliyodhamiria...
Ninachotaka kujua ni kwa nini wachagiaji ni wachache na wengine waliokuwepo wengine hawachangii tena naona umenielewa.
hawakuongezewa mishahara
Ok sasa nimekuelewa.
Ipo thread moja sticky kwenye hili jukwaa inayozungumzia hilo.
hawakuongezewa mishahara
Mkuu mie naona kikubwa zaidi ni pale watu wanaposhindwa kutoa historia yao hili wapate msaada. Ndio maana mara nyingi ni bora kumshauri mtu aende hospitali baada kumtajia vitu basic kuhusu tatizo lake.
Kingine ni vizuri watu walete feedback baada kupata ushauri hili wengine wajifunze.
Tatizo huwezi kupona siku hiyo hiyo hata ukijieleza ipasavyo kwa Dr wa JF ndio maana watu hukimbilia New Post ambazo hujaa recent topic.
Wengi wa wachangiaji sio lazima wawe MaWitch Doctor au MaDr wa kawaida lakini kutokana na uzoefu wao ndio maana watuelekeza tutmie Maji mengi au miti shamba
Bahati nzuri @ng`wana ong`wa kulwa
,
mara zote upomOn line ndio maana unasema hatujielezi na tunaondoka kabla ya kupata ushauri hiyo ni kweli lakini ukirudi baadaye hata mwaka, mwezi au siku lazima utaukuta huo ushauri maana Siasa au Habari za kimataifa ukiziacha huyakuti yakiwa Live ni sawa kusubiri kitu kilichocha
inategemea na topic, mfano za udaku zinapata michango mingi.na watu kutokuwa serious na majibu yao.mfano kuna topic iliwekwa ya kijana aliingiliwa tigo,alipata comment nyingi.humu wengi hawako serious unless uweke vitu vinavyowafurahisha wao na wajibu majibu ambayo ya upondaji tu
kikubwa ni kama ulivyosema watu wanaanzisha thread kuomba msaada pale anapoulizwa maswali na Dr hajibu anakuwa ameshatelekeza uzi wake,au anarudi baada ya siku kadhaa sasa ni ngumu kumpa msaada mtu usiyeelewa historia ya tatizo lake! Nadhani baadhi ya wataalamu wamekosa mvuto wa kuendelea kuwepo hapa,ila tunaomba warudi Cc: Riwa Mupirocin pia shukrani za pekee kwa Mzizi Mkavu
mimi nipo nawasaidia wengi tu ingawa walio wengi hawarudishi feedback, lakini najipa moyo kwamba mchango wangu unawasaidia. huwa natoa nafasi kama mtu anashida anaweza hata N Pm namsaidia. karibuni sana