LAITI JESHI LA MISRI LINGEKUA LINAENDESHWA KWA MISINGI YA
KIITIKADI NA KISHABIKI ZAIDI KAMA BAADHI YA
VYOMBO VYETU VYA ULINZI HAPA NCHINI LEO
HII MISRI LINGEKUA MGENI WA NANI??
Nadhani kuna upekee kule Misri kwa njia nyingi mno kuweza kujifunza mtu. Mojawapo ni ukweli kwamba Mubarak alipinduliwa na wananchi bila hata ya kuwepo mtu au kikundi chochote cha kuwaongoza isipokua tu azma yao ya kuwa watu huru na kulinusuru taifa lao na ufisadi.
Ukweli huu ulidhihirika pale muda wajadiliano na serikali ilipofika na kukosekana kikundi chochote rasmi cha kujadiliana nalo. El Baradei japo kasaidia sana kuweka mambo sawa kwa upande wa waandamanaji, ukweli wa mambo ni kwamba alifanya kudandishwa tu treni iliokua kwenye mwendo tayari huku wengine wakiwa ndio wanapata kumuona kwa mara ya kwanza akitokea ughaibuni hivi karibuni tu. Kwa mantiki hiyo asingeipewa nchi wakati hata kona zake bado kuzifahamu.
Omar suleiman (Othman wa Misri) licha ya kukubalika sana na mataifa ya Magharibi, naye ilishindikana kumuachia madaraka maaana kwa madai ya vilevile kero za kushabikia serikali ya Mubarak hata kwenye madhambi dhidi ya wananchi naye hadi leo hii nguvu ya umma haitaki kumuona jicho moja akiwaongozi - Misri ni zaidi ya darasa kwa idara zetu mbalimbali katika mataifa ya ulimwengu wa tatu. Lakini hapa kwetu; aaahh wapi, ajaifunze nani wakati sisi kila siku sisi ni mafundi karibia wa kila kitu na kutegemea tu uzoefu wa miaka ya 47 katika karne ya 21.
Kama kweli tunalo taifa linalojifunza - kama si uchokozi wa makusudi kwa raia kwa KANUNI YA BUNGE ILIVYOPINDISHWA, MWENENDO WA KIMIZENGWE KANA KWAMBA TUNAENDESHA BUNGE KATI YA WATANZANIA DHIDI YA WAMALAWI VILE, CHAMA TAWALA KUJICHAGULIA VIBARAKA KAMA MIMOSA CHEYO KULISIMAMIA KWA NIABA YETU NA KUZUIYA CHADEMA HALALI YAKE NA KUBWA ZAIDI KITENDO CHA KUMWEKA MTUHUMIWA WETU NAMBA MBILI LOWASSA KWENYE KITI HICHO NI KANA KWAMBA CCM TAYARI INAJIANDAA NA VITA DHIDI YA RAIA WAKE KWA KUTETEA UFALME WA KIFISADI - LAKINI MUDA UKIFIKA WALA HAKUNA CHA LOWASSA WALA MJOMBA WAKE - KAZI KUTUTIA TU UMASIKINI HAPA KILA SIKU!!!!!!!!!!!
Laiti ningalikua Mwamnyange, Mwema, au Othman; kitendo cha kusikia tu kijana wangu anatamba kwamba yeye ni KADA (Adengenya) wa chama hiki au kile, ni wa dhehebu hili au lile, ukanda huu au ule, au tu hata bila kusema ila udadisi wa mtendo yake yanaashiria hayo hapo juu basi moja kwa moja nitachukua hatua ya kumpa muda zaidi kuendeleza hicho anachokipenda zaidi akiwa nje ya jeshi langu.
Matumizi mabaya yavyombo vya usalama, na hata kufikia mahala hata baadhi ya vyombo hivyo kuwa chini ya MILIKI NA AMRI BINAFSI lakini kuendelea kugharamiwa na wote ni jambo moja linalouma saaana, hutowesha haki upesi, kujenga chuki na watu kugeuka mbogo juu ya hilo.
Kwa kweli laiti nalo jeshi la Misri lingegeuka kuwa mashabiki wa NDP na Mubarak jinsi ambavyo BAADHI ya vijana wake Othman na Mwema walivyohiari kuwa WATENDAJI WKUU katika mambo kibao yenye maslahi kwa kijikundi tu ndani ya CCM dhidi ya vyama vya upinzani, ambao licha tu ya itikadi zao tofauti, amba ni Wazalendo kweli kweli lakini unachagua tu kumnyima huduma na au kumkandamiza kwa kuwa KAMPINGA SHUJAA WAKO, nadhani nchi ya Misri ingeenda moja kwa moja mikononi mwao kikundi hatari cha Islamic Brotherhood na kulibandua hapo ingalikua mbinde tena!!
Hakika hili ni dosari kwa baadhi ya watu ndani ya vyombo vyetu ambalo sisi kama raia walipa kodi tunayaona n a yanaweza kuyumbisha imani zetu kwenu kama si kuwanyima kabisa ushirikiano dakika mnapolihitaji zaidi kama hivi sasa vyombo vya dola vinavyowahitaji raia hivi sasa nchini Misri kuliko hata raia wanavyovihitaji vyombo vyenyewe.
Kusema kwamba Mhe Kikwete sikubaliani na kwa kuwa kaingia madarakani bila ridhaa yetu hilo si sababu tosha kulifanya chombo changu cha ulinzi na usalama kisiendelee kunilinda usalama wangu na mali za kama ambavyo mkataba kati yangu na wewe kikatiba kukutunza kwa kodi yangu inavyoelekeza.
Mwisho, mafunzo ya vyombo vyetu vyote ni sharti vibuni mitaala ya kuelewa mambo mengi sana yanayoendana na wakati ili kuto huduma bora zaidi, haki zaidi (ikibidi hata kuwakosoa na kuwakatalia wakubwa juu ya baadhi ya mambo yasiotuleta pamoja kama nchi yasitendeke), na kutambua ukweli kwamba Tanzania ni kubwa zaidi kulikohataa rais wa nchi. Leo hii Mubarak hayupo Misri lakini taifa lipo, Mwalimu Nyerere katangulia mbele ya haki lakini Tanzania bado linaendelea licha ya mapenzi makubwa tuliokua nayo kwake.
lKwa kuhitimisha tu, napenda nirudie kwamba ushiriki wa kishabiki wa baadhi ya vyombo vyetu vya ulini na usalama kwenye mambo ya siasa nchini tangu Pemba, Unguja, Chaguzi zetu mbalimbali, mauaji ya Arusha na Mbarali, yote kwa pamoja ni miongoni mwa mambo ambayo yatachukua kipindi kirefu sana kurekebishwa, kuondoka vichwani mwetu na pia kurejesha imani na heshima kama zamani.
Chukueni hatua za haraka, za wazi kutufanya tuamini kwamba mnaweza kuwa zaidi ya jeshi la Misri kwa hapa kwetu.