Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Salam, wanabodi,
Kuna habari zimeenea kwenye vyombo vya habari kuhusu siku ya ijumaa ya tarehe 27/05/2016, maalim seif atahitajika kwa ajili ya mahojiano na jeshi la polisi mjini zanzibar. Hii ni kauri ya kamishina wa upelelezi, msangi aliyonukuliwa na vyombo vya habari.
Swali! Maalim seif kuhojiwa na polisi ni dhambi? Na jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kuhoji watu wa aina ipi? Nasema hili kwa sababu baadhi ya wanasiasa wanalalamika kwamba ni kumdhalilisha maalim seif kwa kuhojiwa na polisi, rejea gazeti la mwananchi la leo 25/05/2016.
Naweza kusema jeshi la polisi limetumia hekima sana kwa kumuandaa kwa mahojiano kwa kumpa almost a week, wakiamini ni kiongozi mkubwa katika nchi hii. Vinginevyo uwezo wa kumkamata na kuhoji bila kumpa taarifa wanao, kwa mujibu wa sheria za nchi zilizotungwa na bunge letu,kwani hakuna aliye juu ya sheria.
Ikumbukwe maalim seif aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akizuia raia wa zanzibar kutokulipa kodi. Je? Ninyi mnaosema anadhalilishwa kauli hiyo ilikua sawa? Mbona mlikua kimya? Au mkuki kwa nguruwe?
Naomba wanasiasa tuliache jeshi la polisi lifanye kazi yake. Cha msingi sheria na kanuni zifuatwe, pasiwepo aina yoyote ya uonezi.Ukitokea uonevu wa aina yoyote hapo ndipo wanaharakati na wanasiasa kupaza sauti zao kwa nguvu zote.Kuanza kupaza sauti sasa ni kuingilia kazi za jeshi la polisi.
Naomba wajuzi wa masuala haya tujadili jambo hili kwa wema na si kutanguliza itikadi ya uvyama.
Nawasilisha.