Jeshi la Polisi laua majambazi 3 Masaki Dar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi eneo la masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tatu eneo Masaki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kamishina Sirro amesema kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa wakati wakiwa wanajiandaa kufanya tukio la uhalifu katika moja ya ofisi ya kubadilisha fedha za kigeni iliyopo Masaki.

Amesema kuwa watu hao walikuwa katika gari lenye namba za usajili T 135 AQJ aina ya Rav 4 rangi ya Silver, polisi walilisimamisha gari hilo ndipo majambazi hao wakaanza kurusha risasi na kisha kuzidiwa na kuuawa na polisi waliokuwa katika doria.

Amesema baada ya kuwaua majambazi hao walikwenda kukagua na kukuta bunduki mbili aina ya pisto, Hirizi, Bomu la Kurusha na Mkono pamoja na karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa maneno ya kiaraabu. Sirro amesema ametangaza kiama kwa watu wanaotumia nguvu katika utafutaji fedha kuwa hawana nafasi tena katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa mwandishi, Salma Said aliyetekwa Zanzibar hivi karibuni ni mzima kutokana na kumkuta kuwa hana jeraha lelote katika mwili wake.

Amesema kuwa mwandishi huyo wamechukua malalamiko ambapo wanafanyia upelelezi juu maelezo aliyetoa baada kuonekana katika mazingira hayo.

Aliongeza kuwa baada ya upelelezi watachukua hatua lakini kwa sasa yuko katika matibabu katika Hospitali ya Regency Jiijini la Dar es Salaam.
 
1. RC Makonda andaa milioni tatu hapo za kulipa walioopambana na kuyashinda majambazi matatu.

2. "Amesema kuwa mwandishi huyo wamechukua malalamiko ambapo wanafanyia upelelezi juu maelezo aliyetoa baada kuonekana katika mazingira hayo". Wajuzi wa lugha nisaidieni hapa sijaelewa.

3. "Aidha amesema kuwa mwandishi, Salma Said aliyetekwa Zanzibar hivi karibuni ni mzima kutokana na kumkuta kuwa hana jeraha lelote katika mwili wake."

HAPA NI TAARIFA INATETEMEKA AMA MWANDISHI ANATETEMEKA? TATIZO HASA NI NINI JUU YA HII TAARIFA HADI IWE HIVI?

4. " Aliongeza kuwa baada ya upelelezi watachukua hatua lakini kwa sasa yuko katika matibabu katika Hospitali ya Regency Jiijini la Dar es Salaam".

Number tatu na namba nne. Sikuwahi kufikiria hadi sasa polisi wanaangalia majeraha mwilini kama kiongozi cha kuangalia usalama wa mtu. Na kama ndivyo, anatibiwa nini Regency? Polisi hawana madaktari wa kusaidia kuficha hizi aibu?

Sijui kwa nini ninapata shida sana na hii taarifa mwanzo hadi mwisho wake. Imejaa woga na mitetemeko inayoaashiria kuna mambo hayako sawa.

Tuendelee kusikiliza.
 
Huyo mwandishi alitekwa wakati alikua anakuja dar kwaajili ya matubabu katika hospital ya regency....so its obvious baada ya tukio lazima amalizie dhima yake ya kufika regency
 
Mkuu, Nashangaa hiyo baseless and pointless comment ya Sirro, ati maandishi maneno ya "kiarabu" Yaani hakuona ushahidi mwengine..... (kweli hawa ndo wakulinda nchi na rasilimali zake!!!!)
Dont get it twisted......ametaja vitu walivyokutwa navyo majambazi, kimojawapo ni karatasi yenye maandishi ya kiarabu! Mbona hukushangaa kutajwa hirizi?!
 
Safi sana polis kama kweli hao ni majambaz. Yameonja utamu wa vitu vyenye ncha kali vinavyoruka hewan
 
Dont get it twisted......ametaja vitu walivyokutwa navyo majambazi, kimojawapo ni karatasi yenye maandishi ya kiarabu! Mbona hukushangaa kutajwa hirizi?!
Msimamo yenu unajulikana ( Jungle Warrior ) !! Yaani Jambazi ni mzawaa yeye na maneno ya kiarabu ni wapi na wapi? (1000 questions)... Uhalifu wenye kutumia SILAHA moto, hizo silaha hazina brand names au maandishi ya LUGHA ingine??!!?? au hiyo hirizi ililetwa na kutoka kwa mganga wa Arabuni......
Still pointless and Baseless !! haiingi akili kbs kwa mtu mwenye akili timamu !!!
 
Unakuza issue tu...ni hivi baadhi ya majambazi wanatumia uchawi na mara nyingi huwa wana hirizi na makaratasi ambayo yameandikwa kwa maandishi ambayo wengi wanaona ni ya kiarabu....sasa wewe kama inakuuma kusikia neno 'kiarabu' umia tu.....huwezi kukuta mganga wa kienyeji anaandika yale maandishi mekundu kwa kiingereza au kijapani.
 
Zamiluni! Mbona unapotoka na unapotosha? Afande ametaja bastola, hirizi na karatasi yenye maandishi ya kiarabu. Mbona unakosoa kutajwa karatasi lenye maandishi ya kiarabu tu?
Huyu ni wale wale ukitaja uarabu ni shida!
 
Back
Top Bottom