Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam lasitisha ulinzi Shirikishi mjini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487

Na Avila Kakingo,
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lasitisha shughuli za ulinzi shirikishi kwa muda usiojulikana katika vituo vya Polisi vya mjini kati kutokana na malalamiko na utendaji kazi ambao hauna tija kwa jamii.

Kauli hiyo imekuja baada ya kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kuona mapungufu mbalimbali ikiwa na matendo yenye harufu ya rushwa, vikundi hivyo kutokufuata sheria na taratibu za ukamataji kwa kutumia nguvu kupita kiasi hata pale isipohitajika pamoja na utendaji mbovu.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Katazo hilo limesababisha kufungiwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwa muda usiojulikana mpaka pale Jeshi la polisi litakapo lidhishwa na kuwapa mafunzo maalumu ya ukamataji wa bodaboda zinazovunja sheria za barabarani.

Pia Kamanda Sirro amesema kuwa limefanikiwa kukamata magari mawili yanayosadikiwa kubeba vitu vilivyoibwa kwenye ofisi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) magari hayo ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CNV na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV na kuwakamata walinzi wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo katika jengo hilo.

"Katika wizi huo vitu vilivyoibwa ni Compyuta mbili, aina ya Dell pamoja na CPU, Monitor zake na Televisheni moja aina ya Sumsung inchi 40" Alisema Sirro.

Katika tukio jingine Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuokoa Tumbaku boksi 71 yenye thamani ya shilingi 150,000,000 mali ya Ahmed Huwel miaka 36 mfanyabiashara na mkazi wa Msasani Regent.
 
Mimi sikubaliani na kusitisha ulinzi shirikishi, bali waboreshe utendaji wao kwa kuwapa mafunzo zaidi na kuwaondoa wale wote wanaoharibu sifa ya jeshi la polisi
 
Hongera Sirro hawa watu walizi kwa rushwa, hata hivyo alitakiwa aelezee ameingiza shillingi nagapi alizokamata bodaboda zenye makosa
 
pole sana kamanda wa ulinzi shirikishi Kigamboni ndugu HAKIM, pamoja na Babu edi.

bila kuwasahau wale wa polisi msimbazi kariakoo
 
Nimefurahishwa na hili agizo. Hawa ulinzi shirikishi wengi ni wachumia tumbo watu wasiokuwa na ajira na shughuli maalum. Wanaonea wananchi na wengi wao kwa mamlaka ya serikali za mtaa wameanzisha vikampuni uchwara vya ulinzi na kukusanya mapato bila risiti za efd. Kwa ufupi ni Impossible people.
 
Back
Top Bottom