Jee ni vyema sasa ikatungwa sheria ya siasa za kiustaarabu?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
5,072
4,508
1. Demokrasia siyo uanaharakati
2. Demokrasia siyo kufanya fujo bungeni na kurushiana makonde au matusi.
3. Demokrasia siyo kufanya fujo mitaani na kupinga serikali iliyo madarakani wakati wote.
4. Demokrasia si kushinikiza mawazo ya minority yatekelezwe, hata kama ni mazuri.
5. Demokrasia dhana yake ni wengi wape na wale wachache wasikike.
5. Demokrasia ni kutekeleza maamuzi ya wale walio wengi hata kama yahako sahihi ili mradi hayakiuki katiba iliyokubaliwa na wananchi walio wengi.
6. Kipindi cha kuipima na kuishitaki kwa wananchi serikali iliyo madarakani kidemokrasia ni wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu inapokaribia kumaliza kipindi chake ili wanamchi waichukulie hatua sitahiki kupitia sanduku la kura.
7. Demokrasia siyo kuishitaki serikali kwa wananchi wakati wo wote minority wanapoona inafaa.
8. Kujenga chama cha upinzani cha kidemokrasia ni kujenga hoja bungeni zenye nguvu na ushawishi kwa njia ya kiustaarabu na siyo za kiubabe.
9. Kujenga chama cha kisiasa kidemokrasia si kwa njia ya maandamano mitaani ambayo lazima yatasababisha virugu. Vyama vinajengwa kwenye ngazi ya shina na si vinginevyo. Vikao vya ngazi za juu mbali mbali vya kimkakati na shirikishi ni mhimu lakini si mikutano ya hadhara ya kuponda kinachofanywa na serikali iliyo madarakani kihalari. Mikutano hii inaruhusiwa tu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Kile kinachoendelea sasa ni kizungumkuti. Kuna haja ya kutunga sheria na kanuni zake za namna ya uendeshaji wa siasa zetu kiustarabu ili kuondokana na kizungumkuti hiki ambacho kinaweza kutupeleka pabaya tukawa kama Syria na kadhalika.

Ninatoa hoja.
 
Mwenye mbio husifiwa na hutuzwa ila akimbiaye mpaka akapitiza kwao huchekwa na kuzomewa.....
 
Mwenye mbio husifiwa na hutuzwa ila akimbiaye mpaka akapitiza kwao huchekwa na kuzomewa.....
Sijakuelewa vizuri mkuu. Ni nani huyo kapitiliza kwao kuhusiana na mada hii ya siasa za kistaarabu?
 
Back
Top Bottom