Naomba mchango wenu wana JF kwa hili la mtu kuanza kuhubiri neno la Mungu katika daladala. Kuna jamaa mmoja aliyekuwa mevaa suti aliingia kwenye daladala na kuanza kuhubiri neno la Mungu kwa sauti kubwa huku kashika biblia yake mkononi. Hakujali watu wanamsikiliza au hawamsikilizi. Tena ilikuwa asubuhi na mapema nadhani kwa wakazi wa hapa Dar mnaelewa hali ya daladala ikoje nyakati za asubuhi. Bwana huyo aliendelea kuhubiri kwa sauti ya juu. Wasafiri walikasirika mwisho wakamzoe. Yote tisa, kumi ni pale alipofika mwisho wa kituo na kuamua kushuka bila kulipa nauli, alipoulizwa na konda alidai hana nauli. Je huu ni uungwana? au ndi utapeli wa kisasa wa kujifanya mhubiri wa neno la Mungu ili usilipe nauli?