Namna Google inavyofanya kazi ni kuwa ukiwa Pakistan unatakiwa uone ramani ya Kashmir inayotambuliwa na Pakistan, ukiwa India unatakiwa uone ramani hiyohiyo inavyotambuliwa na India na hivo zitaonekana tofauti. Ndo maana mwaka jana mwishoni Russia waliitaka Apple ramani zao zioneshe Crimea ni sehemu yake, wakabadilisha lakini ukienda Ukraine utaona Crimea hiyohiyo inaonekana ni sehemu ya Ukraine. Hivo basi Tanzania tulitakiwa kuijulisha Google ifanye marekebisho. Hata hivo jina la Nyasa tunalijua sisi pekee maana hata kwenye mikataba halikuitwa hivo. Assume ziwa Tanganyika Wakongo waliite kilugha chao unadhani kuna jumuiya ya kimataifa italitambua jina hilo.