Je, viongozi wa CCM wanajali zaidi maslahi ya chama chao kuliko maslahi ya Taifa?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,843
31,049
Tunashuhudia huko Zanzibar kukitokea mkwamo mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kutokea nchini mwetu tokea mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi urejeshwe nchini mwaka 1995.

Chimbuko kuu la mkwamo huo mkubwa ambao umesababisha sintofahamu kubwa visiwani humo na hata hali ya maisha ya wakazi wa visiwa hivyo kuwa mbaya, ni kutokana na tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha tarehe 28/10/2015 kuufuta uchaguzi huo kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo tamko hilo liliwashangaza watu wengi kwa kuwa licha ya kuwa waangalizi wote wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi kuusifu uchaguzi huo uliendeshwa kwa uhuru na haki, lakini pia hadi anaufuta uchaguzi huo, Mwenyekiti huyo alikuwa tayari alikuwa ameshatangaza matokeo kwenye majimbo 31, ambayo ni zaidi ya nusu ya majimbo yote ya uchaguzi ya Zanzibar.

Jambo lingine lililoshangaza Umma wa watanzania na Jumuiya ya kimataifa ni kuwa wakati anatangaza matokeo hayo kulikuwa hakujatolewa malalamiko yoyote na chama chochote cha siasa visiwani humo kulalamikia matokeo hayo.

Kuonyesha kuwa tamko hilo la Jecha lilikuwa lake la binafsi na halikutokana na malalamiko ya vyama, mawakala wote wa vyama vya siasa vikiwemo vyama vikuu visiwani humo vya CCM na CUF walisaini fomu za matokeo hayo na wasimamizi wa uchaguzi huo waliwapa vyeti vya ushindi wajumbe wote wa baraza la wawakilishi.walioshinda uchaguzi huo.

Kwa mazingira hayo inaonyesha wazi kuwa tamko la Jecha la kufuta uchaguzi huo lilitokana na shinikizo la viongozi wahafidhina wa CCM wa kuamini kuwa wao ndiyo wenye hati miliki ya kuvitawala visiwa hivyo hadi mwisho wa dunia.

Jinamizi hilo hivi sasa limehamia huku Bara ambako uchaguzi wa Mameya kwenye yale maeneo ya Halmashauri za majiji ambako hesabu za madiwani wa CCM kwenye maeneo hayo 'zinawagomea' kupata Mameya.

Tumeshudia mwisho wa wiki iliyopita huko jijini Tanga ambako kumetokea vurugu kubwa sana hadi madiwani kutwangana ngumi baada ya msimamizi wa uchaguzi huo Daudi Mayeje kumtangaza mgombea wa CCM Selebosi Mohamed kuwa mshindi wa Umeya kwa kupata kura 19 dhidi ya 18 za mgombea wa CUF Rashid Jumbe.

Hata hivyo kutokana na hesabu za madiwani wa CUF ambao ni 20 na CCM kuwa na madiwani 17 na kutokana na fomu ya matokeo ambayo alisaini wakala wa CUF Khalid Mohamed, ilionyesha kuwa mshindi wa Umeya kwenye Jiji hilo alikuwa Rasid Jumbe wa CUF aliyepata kura 20 dhidi ya kura 18 za mgombea wa CCM Selebosi Mohamed.

Ukizingatia kuwa hata uchaguzi wa Umeya wa Kinondoni na Ilala jijini Dar nao umeahirishwa kutokana na figisufigisu hizo za kutaka kulazimisha ushindi baada ya hesabu kuwakataa, ndipo wakalazimika kuwa-import madiwani 'mamluki' toka Zanzibar.

Kwa kuzingatia hali hiyo na ukitilia maanani kuwa mkwamo huo wa kisiasa umeshaanza kuathiri Taifa letu baada ya nchi ya Marekani kuzuia msaada wao wa shilingi zaidi ya trilioni moja kutoka mfuko wa MCC.

Kwa hiyo ipo haja kwa Rais Magufuli ambaye watanzania wengi wamejawa na imani na uongozi wake kwa namna anavyowatumikia watanzania, kuingilia kati hila hizi za wanaccm wenziwe wahafidhina ambao wanaamini kuwa wao pekee ndiyo wenye haki ya kutawala kila eneo la nchi hii hata yale maeneo ambayo hesabu zinawakatalia waziwazi, ili kuwaeleza viongozi wenzake wa CCM waweke mbele maslahi ya Taifa letu zaidi ya maslahi ya chama chao.
 
Tuweke Maslahi ya Taifa Mbele; Maalim Seif Apewe Urais wake, Kinondoni, Ilala Na Tanga Almashauri Zikabidhiwe Kwa Hama

CUF or CDM Bila Figisufigisu.
 
Wako Tayari 9 Wafe ili Mmoja Aishi...Chama Cha Majuha
It is absolutely true.
Hao maccm wako tayari wananchi wateseke, ili mradi tu wao waendelee kutawala, hata yale maeneo ambayo wanajua dhahiri wamekataliwa na wananchi.
Mfano halisi ni uchaguzi wa Zanzibar na uchaguzi wa Umeya Kinondoni, Ilala na jijini Tanga.
 
Tuweke Maslahi ya Taifa Mbele; Maalim Seif Apewe Urais wake, Kinondoni, Ilala Na Tanga Almashauri Zikabidhiwe Kwa Hama

CUF or CDM Bila Figisufigisu.
Hao maccm ni watu wanaoshangaza sana kwa kuwa maeneo ambayo Ukawa wamezidiwa idadi ya madiwani huwa hawatii neno, wanawaachia CCM wachukue maeneo hayo bila rabsha yoyote.
Lakini yale maeneo ambayo wao CCM wanajua dhahiri wamezidiwa idadi ya madiwani na Ukawa wanafanya figisu figisu hadi kusababisha uvunjifu wa amani kama ilivyotokea hapo jijini Tanga.
 
Tuweke Maslahi ya Taifa Mbele; Maalim Seif Apewe Urais wake, Kinondoni, Ilala Na Tanga Almashauri Zikabidhiwe Kwa Hama

CUF or CDM Bila Figisufigisu.
Kwa mfano kwenye uchaguzi wa Umeya kule Tanga yule msimamizi wa uchaguzi ndiyo alionyesha Ukada wake wa waziwazi.
Wakati wakala wa CUF akirudi ukumbini baada ya kuhesabu kura akiwa na matokeo kuwa mgombea wa CUF ameshinda kwa kura 20 dhidi ya kura 17 za mgombea wa CCM, akashikkwa na butwaa baada ya jusikia msimamizi wa uchaguzi akitangaza 'mazingaomvwe' yake kuwa mgombea wa CCM ndiye aliyeshinda kwa kura 19 dhidi ya kura 18 za mgombea wa CUF!
 
Tuweke Maslahi ya Taifa Mbele; Maalim Seif Apewe Urais wake, Kinondoni, Ilala Na Tanga Almashauri Zikabidhiwe Kwa Hama

CUF or CDM Bila Figisufigisu.
Hakuna jinsi inabidi hao ZEC wamtangaze tu Maalim Seif kuwa mshindi wa kiti cha Urais huko Zenj.
Kwa huo ubabe wanaoundeleza CCM ndiyo unaendelea kutusababishia nchi wafadhili wanaendelea kukata misaada yao kwa nchi yetu.
Mfano halisi ni nchi ya wamarekani walivyokata msaada wao wa MCC wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 480
 
Halafu cha kushangaza zaidi kila mara wanaotiwa nguvuni ni viongozi wa upinzani. kule Tanga Polisi wala hawakusita kuwakamata Mbunge (CUF), aliyekuwa mshindi halali wa umeya, na wengine, wote kutoka CUF. Jamani! hii ndiyo spirit ya HAPA KAZI TU? ndio maana watu wanajiuliza iko wapi falsafa? Maana ukiwa na falsafa unaweza kutafsiri kwa vitendo katika maeneo mbalimbali, kisiasa, kijamii, kiuchumi, nk.
 
Back
Top Bottom