Je, uwaziri wa Nape shakani?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Baada ya kumsikiliza Mh Rais jana kwenye sherehe ya kumuapisha mkuu mpya wa Majeshi nchi, kufuatia kauli ya juzi ya waziri Nape kuhusu Madawa ya kulevya inaonekana kabisa kua Rais hajapendezwa na kauli ya waziri huyo na kwa hisia zangu ni kama anaona kua waharibifu wanatetewa.

Kwa jinsi tumjuavyo mkuu, kama waziri huyu hatapokea onyo kali basi nafasi yake iko hati hati.Kwa tulivyomwelewa mh Rais jana ni kwamba yeye aanamini kabisa ukimkamata mtumiaji atakwambia kua madawa anatoa kwa nani,baada ya hapo huyo muuzaji ndio atafutwe akamatwe.

Wema Sepetu nyumbani kwake umekutwa msokoto wa bangi, je,bangi sio Madawa ya kulevya?Ni kweli Wema alikamatwa kwa bahati mbaya?

Huenda waziri Nape alikua na nia njema kabisa kutaka taratibu za ukamataji zifuatwe,Lakini atambue kua huo utaratibu huo kwa sasa haupo na asiwe kama haijui serikali yake.Atulie tu asijekutumbuliwa.
 
Tatizo bado hajatambua kwamba sasa hivi hayupo kwenye propaganda na uenezi, yeye ni waziri ambao nafikiri hawezi kumudu hiyo nafasi.
 
Kwel mkuu ila kumbuka nape ndo mfungaji wa goli la mkono kwenye uchaguz mkuu 2015.kuna watu kama January makamba na Hussein mwinyi wale ni ngumu kutumbuliwa
 
Napenda kuwaambia kwamba CCM wanajua kile wanachokifanya kwa wakati huu mtakuja kuelewa baadae sana
 
Baada ya kumsikiliza Mh Rais jana kwenye sherehe ya kumuapisha mkuu mpya wa Majeshi nchi, kufuatia kauli ya juzi ya waziri Nape kuhusu Madawa ya kulevya inaonekana kabisa kua Rais hajapendezwa na kauli ya waziri huyo na kwa hisia zangu ni kama anaona kua waharibifu wanatetewa.

Kwa jinsi tumjuavyo mkuu, kama waziri huyu hatapokea onyo kali basi nafasi yake iko hati hati.Kwa tulivyomwelewa mh Rais jana ni kwamba yeye aanamini kabisa ukimkamata mtumiaji atakwambia kua madawa anatoa kwa nani,baada ya hapo huyo muuzaji ndio atafutwe akamatwe.

Wema Sepetu nyumbani kwake umekutwa msokoto wa bangi, je,bangi sio Madawa ya kulevya?Ni kweli Wema alikamatwa kwa bahati mbaya?

Huenda waziri Nape alikua na nia njema kabisa kutaka taratibu za ukamataji zifuatwe,Lakini atambue kua huo utaratibu huo kwa sasa haupo na asiwe kama haijui serikali yake.Atulie tu asijekutumbuliwa.
Mkuu

Usiombe nyumbani kwako wakaingia jeshi la polisi, nahakika lazima na wewe utashikwa na msokoto wa bangi.

Hebu kaa kimya, hii nchi imefungamana mihimili yote ikiwemo ya siasa kiasi ambacho kila sehemu kuna mafunza. Tunahitaji mabadiliko ili kusafisha hii mihimili na mafunza
 
Sizonje sio mtu wa kuamini katika "kutuhumiwa"anaamini mtu akishakamatwa ni mhalifu tu..Bwana mdogo mtetezi hakulitambua hili..au labda alimpuuza!
 
Watu wapo serious kufanya kazi wengine wapo serius kutafuta cheap popularity kwa timu za akina dada makonda na president kazeni uzi kelele zimeanza wauza madawa wateketee
 
Back
Top Bottom