Je utajisikiaje kama ukigundua mke wako amejenga nyumba bila kukushirikisha na ameufilisi mradi?

Malifa

Member
Mar 7, 2017
43
45
Naomba mawazo yenu,kwa niaba ya rafki yangu, alikopa mkopo benki ili mke awe na mradi,anakatwa mshahara , wanapoishi bado wanajenga ,pesa inayotumika ni ya mwanaume,mke wake amejenga nyumba kwa siri yenye thamani kubwa kuliko mradi, pasipo kumjulisha mme, mradi pia ameufilisi,, wanawatoto watatu nani wanandoa,upande wa mwanamke wanashangilia na kutetea tukio hilo.Je huyu afanye nini ili moyo wake uwe na amani na famila idumu?
 
hizi ndoa za kisasa hizi ni shidaaaa...

mi machoka hapo upande wa mwanamke wanashangilia
 
Kama anatabia ya kuchepuka basi mke kajiwahi, ila pia mke huyo ni mpumbavu sana kufilisi mradi na inaelekea hampendi mumewe kabisaaaa.

Yaani yupo yupo tu kusukuma maisha, ushauri atafute meanamke mwingine wakumpa furaha huku akiendelea kuishi na mkewe. Ameshamjua na ajue jinsi ya kuishi nae afanye yake kwa usiri pia. Ndio dawaaaaaa atamuheshimu akijua anayake pia, inaweza kuwa labda ni wale wanaume ambao hawafishi kitu wake zao.
 
Huyo mwanamke ni kabila gani? Ushauri amruhusu mwanamke akaishi kwenye nyumba aliyojenga na watoto wote na mume abaki pale pa awali. Kama anakuficha jambo kubwa kiasi hicho inawezekana hata hao watoto si wake
 
kwa mimi sina mchezo na pesa kama anataka ndoa hati ya hiyo nyumba iwekwe majina ya watoto na kama hataki aende huko huko
 
Naomba mawazo yenu,kwa niaba ya rafki yangu, alikopa mkopo benki ili mke awe na mradi,anakatwa mshahara , wanapoishi bado wanajenga ,pesa inayotumika ni ya mwanaume,mke wake amejenga nyumba kwa siri yenye thamani kubwa kuliko mradi, pasipo kumjulisha mme, mradi pia ameufilisi,, wanawatoto watatu nani wanandoa,upande wa mwanamke wanashangilia na kutetea tukio hilo.Je huyu afanye nini ili moyo wake uwe na amani na famila idumu?

Nyumba iuzwe na fedha zifufue Biashara na zingine zimalizie hiyo nyumba wanayoishi ambayo unasema bado wanaijenga
 
Suluhisho mume apotezee alipe deni na maisha yaendelee. Isipokua kuanzia hapo miradi na mipango yote atekeleze mwenyewe kwa siri, na kama mke sio mwajiriwa wa sehemu yeyote asikanyege kwenye biashara, wala mradi wowote.
Abaki kuwa mama wa nyumbani. Umpangie kilakitu hata za marakwamara (mkate wa mwezi) aombe. Vinginevyo utaruditena kuomba ushauri ukiwa umechelewa.

Na watoto kawapime vinasaba mkuu.
 
Alichofanya mke sivyo kabisa ila kuna umuhimu wa kusikiliza pande zote mbili. Huyo rafiki yako ukute ana madudu hajakwambia. Mwanamke kuinuka tu na kuanza kujenga nyumba kisirisiri na kufilisi mradi itakua uwenda wa zimu, kuna kitu kilicho pelekea achukue hatua hiyo.
 
Mwanaume apeleke shauri mahakamani aombe kisheria ili mahakama itambue kwamba hiyo nyumba ni yake maana kisheria aliyetoa pesa ya ujenzi ndiye mwenye nyumba. Mahakama ikishaamua hivyo aandikishe majina ya watoto kama ndio warithi wake. Atafute wasimamizi wa mirathi tofauti na mkewe. Mambo hayo yakishakamilika ahamie kwenye nyumba yake na hata kama mke atataka kumfuata atafute 'kifaa' kingine aachane kabisa na huyo aliyemfanyia unyama.
 
Back
Top Bottom