Je, upinzani Tanzania ni kivuli cha CCM?

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
11,136
19,871
je, lengo LA upinzani ni kuboresha au kutoa dira mbadala ya kiutawala?

Kabla ya yote lazima tafsiri au maana ya neno "Upinzani" ifahamike, katika maana ya kawaida upinzani ni hali ya kupingana au kwenda kinyume na utaratibu au hali ya kawaida.
katika nyanja za kisiasa imezoeleka kuona au kusikia mpinzani akipinga jambo lolote kutoka chama tawala au mamlaka iliyo madarakani, je dhana hii ndiyo udhihirisho( oppositional manifestation) wa kuwa mpinzani? ingefaa zaidi kama mpinzani angeziba ombwe la mboreshaji kuliko kusimamia tafsiri ya kizamani isiyoendana na Hali, mda, na mazingira tuliyonayo kwani ingefaa kutumika kupinga ukoloni na sio kupinga dola ya waafrika/watanzania wenyewe.

Ni dhahiri wapinzani katika nchi yetu wamejikita zaidi katika kupambana na matokeo ya maamuzi ya watawala badala ya kutoa dira mbadala ya nini kifanyike kabla ya uamuzi wa serikali kutolewa, kwa hali hii ccm wameweza kuwachezea wapinzani kwa namna watakavyo, hii ni kwa sababu:-

1. mapungufu ya Ccm ndiyo turufu ya upinzani, hii ina maana kwamba pindi ccm wanapopunguza matatizo ya kwa kufukuza baadhi ya wanachama kwa kashifa Fulani, upinzani huwapokea wakidhani wanaongeza nguvu, hili ndio kosa kubwa ambalo upinzani hulifanya, huwezi kuboresha au kufanya matengenezo ya gari kwa spea mbovu, mfano kuwakaribisha watuhumiwa wa madawa ya kulevya na kuanza kuwatetea.

2. Wapinzani hawana mbadala dhidi ya dola, hili huwafanya kila mwaka kuwa na shida kubwa katika chaguzi kuwania dola, hii ni sawa na kumkosoa fundi aliyejenga nyumba ilihali huna tofali za kujenga nyumba mbadala ambayo ingeonekana bora kuliko ya yule fundi, hapa itaonekana kuwa huna uthubutu wowote kwani huna mbadala,
wapinzani kwa kukosa utashi thabiti hujizika kirahisi na kuonekana wakosoaji tu na hivyo kuzoeleka.
Vitendo hivi huufanya upinzani kuwa tegemezi ( dependent) na sio kujitegemea( independent)
3. Wapinzani hawana mbinu sahihi na salama za kutwaa dola,
picha inayoonekana ni wazi kuwa upinzani umediriki kutumia njia zisizo sahihi na haramu kwa kile wanachokiita kutwaa dola, mfano kitendo cha kumruhusu Edward N. lowassa kugombea urais ilihali walimtaja kuwa ni fisadi ni mbinu batili isiyoendana na lengo, msimamo na matakwa ya jamii.

Tuutumie upinzani kwa malengo sahihi na nia njema.
Karibuni tujadili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom