Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,119
- 1,570
Eze 8:6 SUV
[6] Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, hata niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine.
Swali hili linafaa kwetu sote, kama ambavyo alimwonyesha Ezekieli maono ya yale machukizo waliyokuwa wameyafanya Israeli ndani ya hekalu la BWANA.
Moja ya mambo mabaya waliyoyafanya ilikuwa ibada za sanamu, na desturi za kipagani, hizi zilimkasirisha Mungu na kusababisha uwepo wake uondoke, na hukumu ya Mungu kuwa juu yao.
Leo sio hekalu la Yerusalemu mambo ya mabaya yanafanyika humo, miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, je yale tunayoyafanya yanampendeza Mungu? Maana miili yetu inaweza ikawa sehemu ya kufanya mambo maovu yaliyo machukizo mbele za Mungu.
1 Kor 6:19 SUV
[19] Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Machukizo tuliyoona hapa yalitokana na kuabudu sanamu, sasa leo siyo tu sanamu za mawe, zile dhambi zilizo ndani ya mioyo yetu, yaani tamaa mbaya, chuki mbaya, na unafiki, ni mambo yaliyo machukizo mbele za Mungu.
Mk 7:21-22 SUV
[21] Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, [22] wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Usije ukajisifia na kusema mimi siabudu sanamu za kuchongwa, lakini ndani ya moyo wako ukawa umejaa mambo mabaya kama tulivyoona kwenye andiko hili la Marko.
Tunapaswa kujichunguza kila mara mienendo yetu, tusipokuwa na tabia ya kujihoji juu ya mwenendo wetu, tunaweza tukawa tunajiona salama, ila ndani yetu tumefarakana na Mungu wetu.
Ukiwa umefika mahali huoni mabaya unayoyafanya, na hata ukiambiwa na wengine hutaki kubadilika, ujue upo katika eneo baya la kuhitaji kumrudia Mungu haraka sana.
Tunapoona mahusiano yetu na Mungu yameharibika, tuutumie vizuri mlango wa toba, ili tuweze kurejesha uhusiano wetu na Mungu.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana