Hatari za kutumia dawa vibaya
Hii ni orodha ya makosa ya kawaida tunayofanya tunapotumia madawa ya kisasa. Matumizi mabaya ya madawa yafuatayo yanaleta vifo kila mwaka, kuwa mwangalifu Chloramphenical (chloromycetin) -Kwa bahati mbaya, dawa hii hupendelewa sana kutumiwa kwa magonjwa madogo madogo kama vile kuharisha. Hii, ni hatari sana.
- Dawa hii inatumika kutibu magonjwa kama vile homa ya matumbo. Isitolewe kwa watoto wachanga.
- Oxtocin(pitocin) pituitrin na Ergonovine (Ergotrate) - kwa bahati mbaya wakunga hutumia dawa hizo
kuharakisha kuzaliwa kwa mtoto au kumpa nguvu mzazi wakati akiwa na uchungu wa kujifungua.
Matumizi ya namna hii yana hatari sana. Unaweza kumwua mama au mtoto. Zitumie tu, kwa kuzuia kutoka damu baada ya mtoto kuzaliwa.
- Sindano za dawa: Imani kuwa sindano ni bora kuliko vidonge si ya kweli. Mara nyingi dawa za kunywa zinafanya kazi vizuri zaidi kupita sindano. Pia, dawa nyingi zitolewazo kwa sindano huhatarisha maisha kuliko za kunywa. Matumizi ya sindano lazima yapunguzwe.
- Penisilini: Penisilini hufanya kazi kwa magonjwa fulani ya kuambukiza. Ni makosa kutumia dawa hii kwa shida za kustuka misuli, kujiponda, aina yoyote ya maumivu au homa.
Kwa kawaida, majeraha yoyote ambayo hayakuchubua ngozi, ijapokuwa kuna uvimbe mkubwa ni vigumu vijidudu kuingia kwa hivyo hakuna haja ya kutumia penisilini au dawa nyingine yoyote ya kuua wadudu.
Penisilini ina hatari kwa watu wengine. Kabla ya kuitumia lazima ufahamu hatari zake na namna ya kuzizuia.
- Sindano za Penisilini na Streptomisini (zina majina mengine mengi)- Dawa hizi hutumika sana na mara
nyingi kwa magonjwa yasiyohusika. Dawa hizi zisitumiwe kwa mtu aliye na mafua kwa sababu haziponyeshi ugonjwa wa mafua au fluu, zinaweza kusababisha matiti makubwa wakati mwingine, kuzimia au kifo, zikizidi
kutumiwa ovyo ovyo, zitafanya magonjwa kama kifua kikuu na magonjwa mengine ya hatari yasiyoweza kuponyeka.
Vitamini B12; Dawa hii haisaidii kutibu ukosefu wa damu au udhaifu isipokuwa kwa wagonjwa wachache tu. Inaweza kutumika tu, kama mganga ndiye karuhusu baada ya vipimo vya damu. Karibu magonjwa mengi ya damu yanatibiwa kwa kutumia vidonge vya madini ya chuma (Ferrous Sulphate).
Vitamini Nyinginezo: Kwa kawaida, usidunge sindano za vitamini. Sindano hizo zina hatari, ni ghali na hazifanyi kazi yake vizuri kama vidonge.
Bahati mbaya, watu wengi hupoteza fedha zao kwa kununua dawa za maji ambazo zinasemekana zina vitamini. Ukweli ni kwamba nyingi kati ya dawa hizo hazina vitamini. Hata kama zingekuwa navyo ni afadhali kununua chakula kingi na kilicho bora.
Kujenga na kuhifadhi mwili kunahitaji vyakula kama mayai, nyama, matunda, mboga za majani na nafaka; ambavyo vyote vina vitamini na nguvu za kukuza mwili. Mtu mwembamba na aliyedhoofika akipewa chakula
bora mara kwa mara, kitamsaidia sana kuliko kumpa vitamini na chumvi chumvi.
Mtu anayekula vizuri hahitaji nyongeza ya vitamini.
Njia bora ya kupata vitamini.