Je una tabia gani mtandaoni?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,031
Reaction score
168,655
Kijana mmoja alikwenda kufanya usaili kwenye taasisi fulani. Alijibu maswali vizuri kabisa. Pia wakaanza kuzungumzia faida na changamoto za mabadiliko ya kiteknolojia. Kijana akafurahi kwa kuwa kila kitu kilienda vyema na kuahidiwa kupigiwa simu ndani ya siku mbili. Baada ya kijana kuondoka, huyo mwajiri mtarajiwa akafungua computer yake na kuangalia MAISHA huyo kijana MTANDAONI. ALICHOKIONA kikamfanya mwajiri mtarajiwa afungue email hapohapo na kuandika "tunasikitika hatutaweza kukupatia ajira uliyoomba".
Biblia inasema nzi aliyekufa anaweza kuharibu harufu nzuri ya marashi (perfume) hata kama ni ya gharama kubwa kiasi gani. Kumbuka kila tunapotembea tunasomwa. Maana sisi ni barua inayosomwa na watu wote duniani, sisi ni nuru na chumvi ya ulimwengu. Kuna baraka zingine unaweza kuzikosa kwa sababu ya mwendendo na wala sio shetani. Nakuombea Mungu azidi kukufanya NURU inayoangaza kila uendapo katika Jina la Yesu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…