Je, umemgonga mtu na ukagundua 100% haujaonekana utafanyaje?

hannibali

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
468
427
Habarini za muda huu wanaaJamiiForums natumai wazima na mnaendelea kupigana na changamoto za life.

Aya kijana wenu tena hapa tuzungumze na jamii kwa pamoja:

Leo tujadili suala moja ambalo ni common sana katika jamii. Najua wengi wanaendesha magari, pikipiki na vifaa vingine vya moto washawahi kukutana na changamoto hii na wanauzoefu nayo na hata wengine ambao haijawahi kuwakuta watatamani wasikie machache kutoka kwa wengine.

Je, ikitokea katika kuendesha endesha kwako kwa bahati mbaya ikatokea umemgonga mtu either umemuua au umemjeruhi vibaya sana na ukagundua kwa asilimia karibia 100% hakuna aliyekuona utafanyaje( hapa assumption iwe ni usiku ambapo kuna asilimia kubwa ya kutoonekana).

Na kwa wale wanazengo ambao washakutana na hali kama hii tungepata kujua wao walifanyaje?

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom