Je, ulishawahi kudhulumiwa au kutapeliwa? Tushikishane mbinu za Matapeli na namna ya kuziepuka

Mimi jana tu. Nimefika bar moja ina watu kibao mida ya saa mbili usiku. Nikuagiza dada mhudumu aniletee Balimi bariiiid. Kaniambia nimpe hela kwanza. Basi nikampa elfu kumi. Nilisubiri beer nusu saa nikaenda kuuliza mbona siletewi beer yangu. Baada ya kum describe bidada na bar maid wote kufolenishwa bidada hakuwepo. Kumbe yule alikua si mfanyakazi wa pale ila alivalia kama wafanyakazi kuwaibia waheshimiwa wateja. Nilikua sina hela nyingine mfukoni hata ya daladala...
Hii michezo ilikuaga sana corner bar Sinza miaka ya 2008 :D:D
Wadada wanakuja wamevaa sare za blauzi white na black skirts au suruali kama wahudumu.
wanakaa nje na bia moja ya kuzugia mkija kikundi bila shaka mtaagiza round na mtatoa kama sio 10k basi 20k bidada anatokomea zake.
 
Nilinunua laptop mpya kabisa 1.2ml kwa ajili ya kumtumia dogo UDOM atumie kwenye masomo yake na alikuwa anahitaji haswa nikampatia rafiki yangu anaefanya kazi Shinyanga ampitishie pale Dodoma,jamaa akasepa nayo mazima mpaka leo na mawasiliano kakata. Simuemdei Polisi wala wapi nimeapa tutamaliza nae Uswahili na ndugu zake nishawapa taarifa,sitasamehe kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Aiseeeehh hatari sana
 
Mimi mpaka sasa uchungu mkali maumivu yamenishika.

Over 40million...nlijinyima nikajidhulumu mambo mengi, naishi maisha ya ovyo sasa kwa ajili hiyo.
Achana na vipesa mbuzi laki sijui million moja mbili, hiyo pesa inaniuma sana na inanipa presha mpaka leo.
Mshanajr Naomba unipe kombora niokoteshe mtu makopo.
 
Mimi mpaka sasa uchungu mkali maumivu yamenishika.

Over 40million...nlijinyima nikajidhulumu mambo mengi, naishi maisha ya ovyo sasa kwa ajili hiyo.
Achana na vipesa mbuzi laki sijui million moja mbili, hiyo pesa inaniuma sana na inanipa presha mpaka leo.
Mshanajr Naomba unipe kombora niokoteshe mtu makopo.
Haha usifike huko mpwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna na jamaa ssaivi anatangaza anauza vifurushi mwitu vya halotel tigo ttcl vya miezi sita unapata GB 48 sms unlimited na midakika ya kucheba kwa 12000 na 13000 anatangaza whatsapp, NI TAPELI MUEPUKENI UKISHAMTUMIA ANAKUBLOCK.

Ujumbe wake huwa hivi

kifurush kinadumu kwa muda wa miezi 6. Kila mwezi kinajirudia upya. inakusaidia kupunguza gharama za vifurush vya mitandao. Kwa gharama nafuu kabisa.
Unatuma namba unayotaka kuungwa kisha unafanya malipo
katika namba *0742* *410* *794* MPESA *MASHAUR* *MPANGE* Na baada ya dakika 5 unakua umeunganishwa
kwenye huduma ya kifurushi cha miezi sita. Ahsante

KUWENI MAKINI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rebeca 83,

Hao jamaa ni washenzi sana, niliwahi kuwakomalia mpaka tukafikishana tra, nilinunua laptop ya 1.5M kutoka ng’ambo naenda kuchukua eti wanataka ushuru wa laki 7.5 tukafikishana polisi hadi tra na nikatoa laki 1.7 kama ushuru hadi leo mzigo wangu huwa haupitii kwao tena


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mother Confessor,
Kwa sheria za ardhi zilivyo mtu mwenye hati feki hawezi kumzidi mwenye hati halisi, pia kisheria hawawezi kwenda kubadili hati wizarani maana itatakiwa kuoana na hati halisi maana hati uliyonayo kopi yake ipo wizara ya ardhi sasa kama unao ubavu waweza fatilia na ukapata kiwanja chako vizuri kama kuna ujenzi ulifanyika waweza vunja nyumba lakini uwe tayari kurogwa
 
Hao jamaa ni washenzi sana, niliwahi kuwakomalia mpaka tukafikishana tra, nilinunua laptop ya 1.5M kutoka ng’ambo naenda kuchukua eti wanataka ushuru wa laki 7.5 tukafikishana polisi hadi tra na nikatoa laki 1.7 kama ushuru hadi leo mzigo wangu huwa haupitii kwao tena


Sent from my iPhone using JamiiForums
Wenzio ndio tunaona urahisi wa kuingiza mzigo kupitia DHL sababu wanakufanyia clearance wao wenyewe.

Hapa wanaibaje? Ushuru unadaiwa na TRA bila shaka. Wao wanakurahisishia kulipa tu. Infact documents zote za customs utapewa na zitareflect values tajwa.

Laptop yako haikuja na invoice kwenye AWB?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao jamaa ni washenzi sana, niliwahi kuwakomalia mpaka tukafikishana tra, nilinunua laptop ya 1.5M kutoka ng’ambo naenda kuchukua eti wanataka ushuru wa laki 7.5 tukafikishana polisi hadi tra na nikatoa laki 1.7 kama ushuru hadi leo mzigo wangu huwa haupitii kwao tena


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu mwa laptop ya 1.5m kodi yake ni around 270,000 pia inaonekana watanzania wengi hamko well informed pale DHL mizigo inayozidi $20 inakua chini ya TRA Customs na inatakiwa kulipiwa ushuru...
 
Kwa sheria za ardhi zilivyo mtu mwenye hati feki hawezi kumzidi mwenye hati halisi, pia kisheria hawawezi kwenda kubadili hati wizarani maana itatakiwa kuoana na hati halisi maana hati uliyonayo kopi yake ipo wizara ya ardhi sasa kama unao ubavu waweza fatilia na ukapata kiwanja chako vizuri kama kuna ujenzi ulifanyika waweza vunja nyumba lakini uwe tayari kurogwa
Yote uliyoeleza mkuu ni sahihi, isipokuwa hili la sijui kurogwa, umepotosha kwa sababu hawezi kurogwa mtu aliyedhulumiwa, bali anayerogwa ni dhulumati kama imani hiyo ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2011 Mimi na broo sote tulikuwa mwanza vyuoni yeye bugaboo Mimi kwa baba askofu. Mimi sina boom yeye analo kwa hiyo ikawa tunatumia sote. Hali ya home financially ilikuwa tight sana tena sana, boom la broo lilikuwa kila kitu usiskie.

Kuna boya mmoja ni fundi seremala na tapeli mkubwa akapata tenda ya kutengeneza madirisha kwenye shule moja ya kata huko Tanga ila hakuwa na mtaji. Akamfuata dingi wafanye partnership yaani dingi atoe 500k halafu mchezo ukiisha wakilipwa basi oya oya. Dingi hana kitu lakini idea ikawa imekaa njema, akampigia simu broo boom lilipoingia pesa ikatumwa jamaa akaifanyia kazi. Alipolipwa akamzika dingi yaani kama akatuzika as a family. Jamaa tuna udugu nao kiasi anaitwa Bakar Jembe kwa watu wa Tanga wanaweza kumjua. Dingi alihangaika nae kiasi mpaka polisi chumbageni ila kufika kule polisi akaambiwa huyu mshenzi ana kesi kibao hapa katapeli. Dingi akaamua kwamba hakuna hakimu wa mahakimu isipokuwa Mungu. Watu tukafunga na kufanya visomo vya kutosha.

Mwaka 2014 jamaa kauvaa mkenge, kapigwa miaka 20 jela alikuwa maweni pale na sasa naskia kahamishiwa gereza la Morogoro. Last time mzee alienda kumuangalia gerezani alimlilia mzee kama mtoto.

Mwaka Jana nlienda cape town nkakutana na mtoto wake kwenye restaurant moja hivi ile Mimi na wife tunaongea kiswahili kumbe na yeye mbongo akatuskia akaja. Katika kuulizana tumetokea wapi ndio tukagundua kumbe sisi ni ndugu na baba yake alitutapeli as a family. Aisee yule dogo aliskitika sana kuhusu baba yake lakini I told my wife "fu.ck them" I don't have any sympathy kwa kweli.

Mwisho wa utapeli si mzuri maana mungu anaona na analipa hapa hapa duniani
 
Kwa asili Mimi ni mpole na sio mtu wa visasi ila hata sijui mabaya huwa yanawakutaje wanaonitapeli.

Mwaka 2009 kipindi nimamaliza form 4 kuna mshkaji alikua form 3 Tena jirani enzi hizo besti sana aliniazima Samsung ya kuslide, kesho kaja home analeta kiswahili kwamba simu wamemwibia, Daaah niliumia sana na wala sikufanya kitu zaidi ya kuona hana thamani ya kuwa rafiki, mwaka ni 2010 jamaa alipiga division 0 , akarudia form 3 akaacha shule kwasababu wanachapa sana, baada ya miaka mitatu nikamkuta na simu ileile, nikaiacha akae nayo mana ilikuwa sio dili tena.......don't scam me fool

Mwaka 2013 nakumbuka nipo chuoni kuna jamaa alikwapua smartphone yangu hostel, kuna mshkaji wangu akanijuza huyo jamaa alikuwa anaulizia wapi atapata kava za simu kama aliyoniibia, aisee nikampandia jamaa fasta sana hewani kwamba simu yangu airudishe na kweli aliirudisha na sikumfanya kitu, huwezi aminj ila akaiiba Mara ya pili tena....nlikuwa najua ni yeye kabisa na wala sikumfata...nakumbuka tupo bonanza la chuoni mida ya usiku kulikua na disco ukumbi wa chuo, ile nipo namcheki rich mavoko nakuta kuna mtoto mbele yangu kajileta ana ham ya kubambiwa, kumcheki freah nikagundua ni dem wa huyo mwizi wangu, nkikumbuka machungu ya smartphone yangu nilimkamatia mtoto mpaka navyotaka kurudi geto kaning'ang'ania tulale pamoja ila namshukuru mungu shetani sikumruhusu anifanye nilipe kisasi kwa njia ya kumd***a dem wa mwizi wangu mana ni dhambi, nachokumbuka tu jamaa alifeli chuoni na kufukuzwa baada ya kupata sup za kutosha na carry mbili....don't scam me.

Mara ya tatu, kuna mfanyakazi wa inn ya Mjomba wangu alikuwa anaipenda sana simu yangu na kunibembeleza sana nimuuzie simu, kuna kipindi mambo yalikuwa yamebana nikamfata hotelini tufanye biashara, sasa sijui hata ilikuwaje....simu nilihakikisha IMO kwenye mfuko kabla sijafika hotelini ila nlipotaka niitoe ili mteja aione nikajisachi kila mfuko haipo....basi nilidhani labda imeteleza au imeanguka hotelini...baada ya wiki moja nikaenda kuzunguka zunguka kwenye hio inn ya uncle nikakuta ofisi ya huyo jamaa nilietaka kumuuzia simu ipo wazi hajaifunga, basi nikaingia nicheki kama yupo nimsalimie,,, nafungua mlango nikaiona simu inayofanana na ile iliyopotea mazingira tatanishi ipo mezani kaiacha...kujiridhisha ni yangu nikatoa Betri na nikaziandika namba zake za imei kwenye kijikaratasi na nikawahi fasts geto kucheki kama hizo imei zinafanana na kwenye risiti nliyonunulia simu, nikajiridhisha ile simu ni yangu baada ya imei nlizonakili na za kwenye risiti kufanana, nikarudi inn nikamkuta huyo kiumbe mwenyewe simu yangu kwenye ofisi aliyosahau kufunga mlango, nikaanza kumchezea kisaikolojia...nilimwambia twende ofisini kwake ila tunavyofika mlangoni Huyu kiimbe alikimbia fasta sana akisingizia kuna simu anataka apige(namcheka kisirisiri), ile naingia nakuta simu kaificha ndo ikabidi nimwambie ukweli kwamba nimeikuta simu kwake na kuongeza chumvi kwamba kesi nimefungua kwa polisi, nlichimba biti sawa na msamaha kwamba alipe laki 2 ama namwambia uncle tabia yake, huwezi amini msela ndani ya masaa machache alileta hio pesa...nikamwachia simu hio ili kumtesa kisaikolojia, tangu siku hio akiniona anajificha, nikimuomba pesa ni lazima anipe na ananiogopa sana....ilibidi ahame pale....don't scam me.
 
Mimi nakumbuka mwaka 2015 nilipokua naishi maeneo ya Mbagala nilikua nauza CPU yang ambayo nlikua naitumia kwa matumiz yangu ya nyumban
Kutokana na ubize Wang wa masomo nilishindwa kutafuta mteja mimi mwemyewe so kuna jamaa mmoja wa pale mtaani nlipokua naishi nikamuomba anisaidie kutafuta mteja, jamaa alikua na ofisi yake akjihusisha na kukodisha CD na kuingiza nyimbo katk simu pale mtaani. Baada ya kuongea nae akanambia nimuachie ile CPU yang pale ofisini kwake kwani kuna watu wengi huwa wanafika pale na kuulizia CPU

Nikaona haina shida kumuachia tena nilimuamuni kama kaka yetu wa mtaani.

Baada ya wiki kama mbili hivi nikapata mteja mimi mwenyewe ikabidi niende nae kwa ofisi ya yule jamaa ili akaione CPU ili tufanye biashara. Mara CPU ikawa inagoma kuwaka some time inawaka inajizima kiufupi ilikua imeharibika
Wakat nliipeleka pale ikiwa nzima
Baada ya kuichunguza kwa makini nikagundua ilifunguliwa na baadhi ya vitu ndani vilibadilishwa lakn nikinuuliza jamaa anasema ajui chchote na anakua mkali, yaani asee tulipandishiana mpaka bimkunwa Wang akaja kuamua hiyo kesi, kwa busara za bimkubwa ikabidi nikubaki ujinga nikabeba mashine yang nakuludi nayo geto nikamshukur mungu.
Asukwambie mtu ubaya huwa unalipwa hapahapa duniani... Yani baada ya kama mwezi hivi jamaa akafunga ofisi baada ya biashara kua mbaya na kushindwa kulipa kodi aliyokua akidaiwa. Ikabidi akimbilie southafrika kwa njia za panya kwenda kutafuta unafuu wa maisha.
Wakati anasafiri huko njiani akipata ajali akaumia sehemu za mikononi na kuchubuka sehemu za usoni, lakin akakomaa mpaka akafika sauz nahuko nasikia kuna siku alikoswakoswa na risasi na kuamua kuludi bongo. Mpaka sahv yupo tu kitaani hana mbele wala nyuma. Jamani nawasihi msije mkataperi watu au kudhurumu haki ya mtu.
 
Wenzio ndio tunaona urahisi wa kuingiza mzigo kupitia DHL sababu wanakufanyia clearance wao wenyewe.

Hapa wanaibaje? Ushuru unadaiwa na TRA bila shaka. Wao wanakurahisishia kulipa tu. Infact documents zote za customs utapewa na zitareflect values tajwa.

Laptop yako haikuja na invoice kwenye AWB?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sio mara yangu ya kwanza kwa hao jamaa kuchukua mzigo kupitia kwao ni hiyo siku moja ndo walizingua na nahisi kulikuwa na misunderstands kati yao na tra, thus why hata tra walikuja nipunguzia kodi baada ya kuzungushana sana
 
Mkuu mwa laptop ya 1.5m kodi yake ni around 270,000 pia inaonekana watanzania wengi hamko well informed pale DHL mizigo inayozidi $20 inakua chini ya TRA Customs na inatakiwa kulipiwa ushuru...
Mkuu nilizungushwa sana kuhusu huu mzigo na mwisho wa siku tra na dhl hawakuwa na masiliano vizuri kwenye mzigo wangu ndo tra wakanifanyia discount ya kodi
 
Back
Top Bottom