Je, tutafika?

Je, tutafika?

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,339
Reaction score
1,493
Habari Tanzania !

Naomba kuuliza je tutafika?

Tukitaka tufanikiwe, tuamue kwenda kwa pamoja yaani kuwekwe viwango sawa, sera sawa, ufahamu sawa na nia sawa tusiingize siasa au dini kabisa katika maendeleo yetu kitaifa. Kila raia ajue wajibu wake na lengo la taifa letu.

1. Tuna vyuo vikuu vingi, vyuo vya kati vingi na vyuo vya ufundi vingi, kwanini hatuna maendeleo ya maana?

2. VETA, NIT, DIT, MUST, ATC, tuna mavyuo mazuri, majina mazuri mbona hatuna hata mashine za kulima, kupanda na kuvuna mpunga, hatuna kompyuta wala simu za Tanzania, hatuna majembe ya mikono, hatuna magari tuliobuni na kuunganisha wenyewe, hatuna pikipiki zetu, hatuna vifaa vya umeme vyetu, hatuna umeme wetu kwanini?

3. SIDO upo wapi na nani anaweza jivunia ?

4. TIB, NEEC & TIC ?

Nyongeza

Eti hata bulbs tunaagiza ng'ambo kweli?

a) Pesa yetu ya kigeni inapotea kwa kununua teknolojia za nje na wakati mwingine hazina manufaa kwetu kwa wakati uliopo na ujao. Inauma kuwa bendera kwenye ulimwengu wa teknoloji.

b) Tunatengeneza ajira ng'ambo na kudumaza ajira nchini.

Tukiamua tunaweza.
 
Siyo tu bulb tunaagiza mkuu, hadi tooth stick tunaagiza china na Thailand.Hadi Toilet paper ya kujitawazia tunatuma hapo Kenya, Just Imagine.

Alafu kuna watu mchna wamekuja na uzi wa kushadadia kujengwa kwa viwanja vya mpira na wanashangilia kbsa km ndo uchumi wa kati tunaoutaka watz au walionao.

Tukumbuke kunawa mikono wanazengo.
 
Juhudi zetu kubwa ni kuua upinzani na yeyote anaekosoa wenye mamlaka. Hayo mambo ya viwanda sio kipaumbele chetu.
 
Back
Top Bottom