Je, Tundu Lissu aweza kuwa Mwanasheria bora wa Afrika?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,745
239,396
Ni wazi sasa kwamba kwenye eneo hili la maziwa makuu huyu ndiye Mwanasheria bora kabisa kuwahi kuwepo tangu kuumbwa kwa mbingu na ardhi .

Kwa namna anavyopangua kesi za kizushi zilizoambatana na hukumu za kupangwa , sijaona mfano wake , ni mtu anayejiamini na asiyebabaishwa na vitisho , alisema atakuwa Rais wa TLS na amekuwa .

Wakati alipokamatwa kwa tuhuma za " dikteta uchwara " lilikuwa vuguvugu la uchaguzi wa Marekani , sasa tulipoangalia katika Google huyu jamaa alikuwa nafasi ya pili kwa watu wanaotafutwa ili wafahamike , namba 1 ilishikwa na Donald Trump .

dunia nzima ilitaka kujua huyu mtu huyu , nguli wa sheria Tanzania ni nani na yukoje ?

Ili kuweka kumbukumbu vizuri , ieleweke kwamba google search si sawa na Mambo yenu ya instagram.

Kwa kumbukumbu zenu mnadhani kuna Mwanasheria katika bara hili wa kufikia kiwango cha Tundu Lissu ?
 
Tundu Lissu ana uwezo kiasi chake lakini hajafikia hadhi hiyo bado.

Kwanza anaongelea maneno hypothetical.

Mwanasheria wa sifa ulizotaja anajua mambo kiasi cha kutoongelea habari zilizo za hypothetical na speculations.

NB: Sina uhusiano na chama chochote cha siasa Tanzania. Nataka uhusiano mzuri na ukweli tu.
 
Naheshimu mchango wako .
 
Ni mwanasheria mzuri sana, anayezijua sheria vizuri sana tatizo nashindwa kuamini kama anaweza kuwa bora kuliko wanasheria wote africa kutokana na wanaomfungulia mashtaka, tatizo kesi zake anashindana na wenye akili za kibashite bashite, huwezi kumshida mbio mlemavu wa miguu afu ukajisifu unajua kukimbia, mshinde usain Bolt/ Harmorapa hapo tutajua kweli wewe unajua kukimbia.
 
Ni wazi sasa kwamba kwenye eneo hili la maziwa makuu huyu ndiye Mwanasheria bora kabisa kuwahi kuwepo tangu kuumbwa kwa mbingu na ardhi .

Kwa namna anavyopangua kesi za kizushi zilizoambatana na hukumu za kupangwa , sijaona mfano wake , ni mtu anayejiamini na asiyebabaishwa na vitisho , alisema atakuwa Rais wa TLS na amekuwa .

Wakati alipokamatwa kwa tuhuma za " dikteta uchwara " lilikuwa vuguvugu la uchaguzi wa Marekani , sasa tulipoangalia katika Google huyu jamaa alikuwa nafasi ya pili kwa watu wanaotafutwa ili wafahamike , namba 1 ilishikwa na Donald Trump .

dunia nzima ilitaka kujua huyu mtu huyu , nguli wa sheria Tanzania ni nani na yukoje ?

Ili kuweka kumbukumbu vizuri , ieleweke kwamba google search si sawa na Mambo yenu ya instagram.

Kwa kumbukumbu zenu mnadhani kuna Mwanasheria katika bara hili wa kufikia kiwango cha Tundu Lissu ?
:D:D:D:D:D:D:D mkuu mchana umekula kweli au....maana naona hauko serious kabisa
 
Back
Top Bottom