Je tuna vyama vingi kwasababu ya wazungu au Watanzania?

Je tuna vyama vingi kwasababu ya wazungu au Watanzania?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,268
Reaction score
13,895
Je tuna vyama vingi kwasababu ya wazungu au Watanzania??

Mfano wa Chadema
1. Mwenyekiti kafunguliwa kesi ambayo haina ushahidi mpaka leo ya uhaini. Yupo Jela
2. Tume imeizuia bila kufuata sheria zozote kushiriki uchaguzi
3. Msajili wa vyama amezuia kulipwa ruzuku
4. Msajili kaengua viongozi bila sababu ya msingi
5. Mahakama yasimamisha shughuli za siasa za Chadema

Sasa ni nchi yenye serikali inayotaka demokrasia au ni serikali inadanganya kuna demokrasiasa kwasababu ya misaada ya wazungu. Je huu mfumo tumeweka kwasababu tuna imani nao au kufurahisha wazungu.

Watanzania wengi wanapenda na kutaka demokrasia lakini kwenye serikali ni kama unafiki wa hali ya juu. Kuliko kuumiza watu, kuuwa , kuteka kufunga ni bora wawe wazi kusudi ni nini ili tusiendelee kuwachanganya watanzania.

Kwa upande mmoja tunasema ni nchi ya haki na demokrasia wakati huohuo vitendo ni tofauti. Sasa kama serikali haiamini mfumo na sheria za nchi ipo hapo kwa matumbo yao au kwa jamii yao?
 
Kwa kweli inafikirisha na kusikitisha sana,lkn hata demokrat kule USA uenda ilipitia magumu kama haya 🤭😄😄😂😂
 
AAfrika hatukua tayari kua kwenye mfumo wa vyma vingi
 
Back
Top Bottom