Mtoa mada sijajua ni amani ipi umelenga ila nisemee amanj kwa upande wa maisha ya ki ujumla haswa maswala ya kiutawala. Kuhusu suala la amani hapa nchini kwetu linategemeana na mtu mmoja mmoja au jamii, mfano mkulima aliyeko kijijini , amabaye maisha yake ni ya kawaida, hawazi siasa na kama anaziwaza ni za kawaida tu, hawazi kumiliki mali nyingi, yeye maisha yake ni kufanya shughuli zake za kujiingizia kipato cha wastani, kula na kunywa, watoto kwenda shule, kubadilishana mawazo na wenzeke kujumuika na familia baada ya kazi kula na kulala alafu kesho akawahi kwenye majukumu yake huyu ana kila sababu ya kusema kuna amani , na watanzania wengi wako kwenye kundi hili. Kwa upande wa pili kuna wale marahibu wa siasa, kutaka mali, vyeo, wizi, dhuluma, ukosoaji wa serikali, kutetea maslahi ya jumla au binafsi, ushindani nk na wengi wao wako mijini, hawa hakika hawawezi kusema kuna amani bali hawana amani japo ni wachache kwa ujumla. Lakini kwa Tanzania ukikosa amani mara nyingi ni hali inapotokea pale unapoitafuta mwenyewe ni mara chache mtu kukosa amani bila kutafuta ukosefu wa amani, mnf huko Congo, Syria, Burundi, Sudan, Ethiopia,Sudani K, RCA, nk hakuna cha nani wala nani, ukosefu wa amani ni mkubwa, haijalishi unahusika kwenye siasa, kukosoa serikali, mkulima, mwanafunzi, mtoto nk wote mara nyingi wanajikuta katika hali ya kukosa amani. Ukitaka kuishi kwa amani hapa kwetu basi jiunge kwenye kundi la kwanza.