sonaderm
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 618
- 1,816
Kwa kautafiti kangu kadogo, maisha ya mtaani yaliyopo si yale tuliyoyazoea..Hali imebadilika na watu wakiishi maisha ya nidhamu tofauti na mwaka au miaka miwili iliyopita...Baadhi ya mambo ambayo nimejionea mwenyewe kuwa tofauti sana kwa zama hizi ni:
Umbea wa mitandaoni umepungua kwa asilimia kubwa, ma socialite maarufu kama vile wema na wabongo movie hawasikiki tena kwenye kashfa zisizo na kichwa wala miguu..Waandika magazeti hasa ya udaku wamekosa habari kabisa
Ulaji wa bata wa hovyo umepungua, nidhamu kidogo bar ipo, mambo ya kutandaza mabia mezani hayapo siku hizi na mtu anakuja anagonga bia zake tatu kistaarabu na kurudi nyumbani na hakuna fujo za kijinga sehemu za starehe..Ustaarabu ni wa kiwango cha ulaya sehemu za starehe
Barabarani tunaendesha kistaarabu, mambo ya daladala kuchomekea yamepungua sana..EFD zimetunyoosha, kwa sasa kila mtu anakaa kwenye foleni bila shuruti na njia za mwendo kasi zinaheshimika..Kifupi kama ulaya
Nyumba za ibada zinajaa waumini, kila mmoja kwa nafasi yake ametambua kupambana na shida za dunia bila mungu ni kazi bure, kipindi cha nyuma wazee zaidi walionekana nyumba za ibada..
Kwa sasa tunavumiliana hasa unapodaiwa..suala la hela kuwa ngumu limeanza kueleweka kwa wote, mdaiwa na mdai..Tumeanza kusikilizana na kuvumuliana japo wengine bado hawaelewi..Tumeanza kupendana na kuishi bila matabaka maana hata waliokuwa navyo nao wanaonekana kuishi maisha ya chini au ya kawaida..
Bajeti za harusi zimeanza kuwa za kinidhamu, sherehe za vipaimara au birthday zimekuwa za kifamilia zaidi..Mbwembwe za kwenye maukumbi makubwa na lundo la waalikwa limepungua, upendo umeongezeka zaidi ndani ya familia na watu wa karibu na familia tu
Itaendelea.................