Andrew Mushi
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 630
- 696
Ninaanza kuingia hofu, ya uchapaji kazi wa viongozi wetu hususan viongozi wa kuteuliwa ktk ngazi ya mikoa na wilaya.
Nimegundua kitu kimoja, wengi wenye kutetea uchapaji kazi wa hawa viongozi wetu, ukiwauliza vielelezo vya msingi juu ya uchapaji wa kazi zao, hawakurudii na takwimu au vielelezo vya msingi vya maendeleo ktk sehemu zao za utawala. Kitu ambacho wote tunaweza kukiona.
Bali watakurudia na maneno yao waliyotamka, hususan maneno ya kibabe, ujeuri, vitisho, audio za majigambo, na wengine wameshaanza kuthubutu hata kuwapiga watu vibao, vitisho vya jela n.k
Sasa tukijichunguza, swala la msingi je hayo ndio maendeleo au huo tunaouita uchapaji kazi unatuhudhirishia vitu viwili kushindwa KIUWELEDI wa hao watendaji wa mikoa na wilaya au ama UBUNIFU wa jinsi gani ya kuratibu njia mbadala za uendeshaji wa halmashauri zetu kwa kutumia nyenjo na wataalam tuliokua nao ktk sehemu zao walizopangiwa, au yote mawili kwa pamoja.
Siasa za waliokua madarakani kutumia ubabe ktk majukumu yao, ndio imekua kama sehemu kubwa ya maongezi mitaani, na ni daraja ya kukutoa kisiasa.
Lakini tukija kwa mwananchi, changamoto na huduma za jamii ambazo ndio makusudi maalum ya utendaji wao kikazi, yako vile vile na yamezidi kuwa magumu, au kuna unafuu wowote huko mikoani, na hapa ndipo bado ninatafuta ushahidi.
Je tunahitajia ubabe wa kisiasa kuwa kiongozi safi hususan wilayani au mikoani au ubabe wa kisiasa?
Na je mikoani tunahitajia watendaji wake wawe ni wanasiasa au wawe technocrat zaidi, yaani wenye ufundi zaidi, kujua jinsi gani ya utendaji wao kazi, na siasa tuwaachie wabunge.
Kwa pointi ya mwisho hapo, Muheshimiwa Rais anapoteua Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi au Jaji hategemei akafanye siasa Bali ufanisi na utendaji wake, ndio aweze kuutumia zaidi, yaani technocrat na sio siasa zaidi, kwa majaji wetu naliona hilo kwa asilimia kubwa, kwa wakuu wa mikoa, naona siasa zaidi ya utendaji.
I sincerely hope I will be proven wrong sooner rather than later!