Je, sababu ni tendo la ndoa?

mwalidebe

JF-Expert Member
Mar 27, 2016
404
250
Kwanini vita kwanini talaka kwanini mauaji kwanini kutengana kwanini mafarakano na migogoro isiyo kwisha?

Tumesababisha watoto kuwa yatima, watoto kuwa na mzazi mmoja wengine kuamua kutokuoa tena au kutoolewa tena kwa sababu ya usaliti wa mapenzi.
Kitu gani husababisha hasira pale tu mtu anapogundua kuwa amesalitiwa au mwenzi wake anatoka kimapenzi na mtu mwingine?

Baadhi ya sababu;
(1) Mtu hujihisi kuwa amevuliwa nguo mbele ya jamii
Mfano mtu huwaza; Huyu mke wangu ametoka kimapenzi na fulani du sura yangu nitaiweka wapi? Jamaa hujihisi kudharauliwa

(2) Magonjwa
Hii huweza kuwa sababu ya kukasirika pale mtu anaposalitiwa. Muhusika hufikiri huyu tayari ameniletea magonjwa au anaweza niletea magonjwa.

(3) Wivu
Inawezeka mtu akajihisi kuwa mwenzake ametoka nje amekutuna na mjuzi wa mambo kuliko yeye.

(4) Kuweza kulea watoto wa mwingine
Nikweli tuliumbwa tukae na mmoja tu mpaka kifo? Yupo ambaye toka amezaliwa mpaka ndoa hajawai kutoka nje kimapenzi?

Embu share nami kwanini hasira chuki pale unapogundua mwenzi wako anatoka kimapenzi na mtu mwingine?
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
yani hisia ni kama mboni ya jicho, hazihitaji kuguswa na kitu kingine chochote zaidi ya ngozi ya jicho!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom