Je ni nani yuko sahihi?

KEMPANJU BOY

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
508
Reaction score
1,255
Katika Ukristo kuna madhehebu mengi sana, yenye utofauti tofauti katika kile wanachoamini! Misingi ya imani yao inatofautiana.
Lakini tofauti na madhehebu mengine Wenzetu wa RC wanakitu wanaita KANUNI YA IMANI( NASADIKI). Hii kanuni Ukiangalia imejaa yale mambo muhimu ambayo kama kanisa wanaamini na ndiyo imani yao kwa ufupi, na kwao ni kama kiapo ambapo kila wakutanapo(misa/ibada) ni lazima waapishane kwa kila muumini kukili kwamba anamini katika ayo mambo.
Swali! Kwanini sisi madhehebu mengine hatuna kitu kama iki cha kuelezea haswa imani yetu imeegemea nini? Maana tukisema imeegemea kwenye biblia naona tunakuwa tunakosea maana biblia ni kama katiba katika Ukristo!
Ni sawa na kusema Kila chama cha siasa kina imani fulani japo imani iyo lazima iwe haivunji katiba( biblia kwenye Ukristo).
HITIMISHO! Wale wenye kuanisha misingi ya imani yao na sisi tusiokuwa na iyo miongozo ni wapi wako sahihi kiimani? Je labda tuseme siku ya mwisho tukiulizwa tuelezee tulikuwa tunaamini katika nini tutajibu vipi?
N:B kama kuna dhehebu/ Dini yenye kitu kama icho( kanuni ya Imani) tujulishane zaidi.

Sent Using!! Nokia kitochi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…