Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 10,460
- 12,196
CCM kama taasisi kwa sasa inaonesha kila dalili za kusambaratika.
Kansa vya makundi ya urais iliyoasisiwa na Jakaya Kikwete sasa imemaliza kula ngozi imehamia kwenye minofu, mifupa na damu.
Kama vyama vingine vyote vikongwe vilivyofanikiwa kufa; CCM nayo kwa sasa inafuata mkondo ule ule.
Hakuna chama kilichokuwa na nguvu hapa Afrika Mashariki kama TANU. Jiulize kwa sasa kipo wapi.
Walau akina Uhuru Kenyatta walikuwa na Exit Strategy; sisi huku watu wanataka kufa ndani ya meli mbovu wakidhani itawafikisha mwisho wa safari yao.
Kilichopo Tanzania kwa sasa ni kuwa wananchi wamechoka na wapo tayari kwa lolote litakalobadilisha mfumo wa maisha yao.
Chini ya CCM nchi imepwaya na kukosa dira/muelekeo. Chini ya CCM viongozi imeonekana wanazidiwa busara na wananchi walio wengi!
Chini ya CCM wanasiasa teule wa CCM wanajiandalia maisha bora huku wakiwatelekeza watanzania walio wengi!
Chini ya CCM rasilimali za taifa zinakwapuliwa na wajanja wachache huku wakilindwa na mfumo mbovu wa kubebana bebana na kulipana fadhila!
J.K Nyerere aliwahi kutabiri kuwa kuna kipindi kinakuja CCM itayumba na mustakabali wa nchi nao utayumba vile vile (Bila CCM imara nchi itayumba). Aliongea vile kumaanisha kuwa chama tawala kinaposhindwa kujitambua basi nchi lazima iyumbe hadi ipoteze dira na muelekeo. CCM wana haya maneno kwenye majengo yao lakini wamepigwa upofu.
Laana imewafumba macho.
Wao wanajua tatizo la watanzania ni nani awe raisi wa nchi.... BAAASI! Kwa sasa tayari wameshaanza vita vyao vya makundi ya urais. Lingine wanalojua ni kuwa matatizo ya watanzania yatamalizwa kwa burudani ya muziki!
Hakika CCM wamepigwa upofu! Wao kila siku wanafikiri kuwa adui yao mkuu ni wapinzani wenye nguvu (wakiongozwa na CHADEMA). Wanazunguka huku na kule kuwarubuni watanzania wenye shida. Wanafanya siasa za upinzani ilhali wao ndiyo wenye serikali yenye uwezo wa kubadilisha muelekeo wa nchi kwa sasa.
Wanasahau kuwa yote wanayofanya wanawafanyia wananchi wa Tanzania.
Nathubutu kusema kuwa haya ni maadhimisho ya miaka 37 Mbeya ni ya mwisho kwa CCM. Yakitokea maadhimisho mengine yatakuwa ni mwakani na CCM haitokuwepo tena miongoni mwa vyama hai.
Yeyote anayebisha aueleze umma wa Tanzania na dunia nzima yale mazuri yaliyofanywa na CCM tangu iasisiwe miaka 37 iliyopita.
Je CCM imeifanya nchi ipige hatua kimaendeleo (kiuchumi, kijamii, n.k) na kujiweka kwenye ushindani na nchi nyingine duniani? Je, CCM imetumia vipi rasilimali za taifa kwa ajili ya maendeleo ya watanzania?
Wenye busara wanajua kuwa CCM imewekeza nguvu kubwa kuhakikisha upinzani unadumaa kwa gharama zozote zile huku ikiuza nchi kwa wakoloni mamboleo!
Mengine yote porojo!