Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,108
- 34,933
Wapendwa Wakuu
Muundo wa uongozi Tanzania unaelekea kuibua maswali mengi. Pamoja na kuwa tumo ndani ya Muungano bado Watanzania Bara hawana nafasi ya Uongozi huko Zanzibar.
Juzi tumeshuhudia Zanzibar imepata Rais na Makamu wawili wa Rais wote wazanzibar. Je kwanini Wa-bara hakuna hata mmoja huko Zanzibar?
Lakini: Wazinzabar wanatawala Bara, na kuwatungia sheria Wa bara. Tunaona makamo wa Rais Mzanzibar, wabunge wengi tu Wazanzibar; na Mawaziri kadha kutoka Zanzibar watatangazwa hivi karibuni KUJA KUWAONGOZA WA-BARA. ILIHALI HAKUNA HATA WAZIRI MMOJA WA HUKO ZANZIBAR AMBAYE ANATOKA BARA.
Je, kama Tanzania ni moja ni lini Wa-Bara watatawala Zanzibar kama wa Zanzibar wanavyotawala Bara?
Mimi Binafsi napata maswali mengi; ninapoona hakuna hata MBUNGE mmoja Msukuma huko Zanzibar
Tutarajie nini kwa mfumo huu?
Nakaribisha maoni Yenu Asanteni.
Mathematically
Muungano =Zanzibar+Bara
but
Bara>>>>Zanzibar
therefore
Bara{zanzibar} and not Zanzibar{Bara}
For that reason Bara{zanzibar} will exist and Zanzibar{Bara} will not exist"impossible set" or true "Null set"
However Bara kuiongoza zanzibar is logicless, kwa sababu sehemu ndogo ndio huhitajika kuiongoza sehemu iliyo kubwa and not vise versa. (i.e kikundi kidogo cha watu kitaongoza kundi kubwa na sio kundi kubwa liongoze mtu moja au kikundi kidogo cha watu)
So,
Bara will need Zanzibar na Zanzibar will not need Bara. Hence proved
Japo ni kinyume cha katiba buti kwa maslai fluani fulani ya kichama na kitaifa itaaminika iwe hivyo. But in reality Katika lazima iheshimiwe.
Karata zilizochezwa wakati wa kuunda "Tanzania" zilizaa utata ufuatao: Zanzibar ni nchi ndani ya muungano - Tanzania bara si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyo Zanzibar . Kwa "equation" hii ni wazi wazanzibari wanaweza kuongoza bara kwani ni raia wa 'Zanzibar" na pia ni raia wa "Tanzania". Si rahisi kwa mtanzania kutoka bara kuongoza Zanzibar kwani yeye ni raia wa Tanzania lakini si raia wa Zanzibar!
Kwa majibu yako ni kuwa sisi Wabara hatuwezi kuwaongoza Wazanzibar?
Karata zilizochezwa wakati wa kuunda "Tanzania" zilizaa utata ufuatao: Zanzibar ni nchi ndani ya muungano - Tanzania bara si nchi bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyo Zanzibar . Kwa "equation" hii ni wazi wazanzibari wanaweza kuongoza bara kwani ni raia wa 'Zanzibar" na pia ni raia wa "Tanzania". Si rahisi kwa mtanzania kutoka bara kuongoza Zanzibar kwani yeye ni raia wa Tanzania lakini si raia wa Zanzibar!
Hivi kweli eeh!, unajua linawezekana hili ni taifa la viongozi. Inawezekana wenzetu wamebarikiwa kutawala, kati ya viongozi wakuu 5 wa nchi yetu 3 wanatoka Z'bar na 2 ndio bara. Z'bar inawatu wasiozidi 1mil na bara si chini 40mil du!, halafu majaji wakuu wote Z'bar. Hawa jamaa wana kipaji cha uongozi.Kama ni hivyo kwa nini kila leo Wazanzibari hawaachi kulalamika kuwa wanatawaliwa na Watanganyika ? Hivi sasa wana Raisi wao, Makamu Raisi wawili wao na huku Tanganyika wanaye Makamu wa Raisi. Kwa mahesabu rahisi ni kuwa kati ya viongozi wakuu (maraisi) wanne ndani ya Jamhuri ya Tanzania, watatu wanatoka Zanzibar ! Hii ina maana kwamba kila wakaazi 250,000 huko Zanzibar wanamtoa Raisi wakati huku Tanganyika ni Raisi moja kwa wakazi 40,000,000 ! Talk of the absurdity of it all !!
Sasa mnasema mnaibeba Znz, na ni mzigo, kwanini hamuitui?
Ukweli ni kwanza hata waznz pia hawawataki, sasa cha kujiuliza ni nani ana-provide 'gundi' ya huu Muungano? CCM na now CUF..sasa hao ndio wakuulizwa.