Je, ni kweli ukichelewa kuhamia kwenye nyumba misukule huishi humo na huwa haitaki kutolewa?

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,663
13,488
Nimeshangazwa na hili, jamaa yangu alijenga nyumba na kuishia kupiga paa. Baada ya hapo ameishi kama miaka nane bila kuifanyia finishing. Last year aliifanyia finishing na kuhamia. Toka amehamia anasema kwenye nyumba kuna mashetani, usiku kuna kelele dalini na wakipika chakula usiku wakiamka kiasi kingine kimeliwa, mfano wakiandaa maandazi 10 kwa ajili ya chai asubuhi, wakiamka wanakuta yako 7 na anasema hakuna panya kwake.

Binafsi siamini ila yeye anaamini hivyo. Je ni kweli ukichelewa kuhamia kwenye nyumba misukule inakuwa inaishi humo na huwa haitaki kutolewa?!

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
 
Shetani anasoma maandiko! Ukijenga nyumba ukaiacha bila kuhamia basi ni halali yake shetani na majeshi yake (mapepo na majini) na makuhani wake (wachawi) kuhamia hapo na kufanya makazi au ofisi. Hii ni kwa mujibu wa maandiko mengi tu kwenye Biblia mimi nakupa moja

Yeremia 9:11
"Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote."

Mbweha inamaanisha shetani.

Ndo maana ukitaka kuhamia nyumba mpya lazima ufanye ibada na kuiweka wakfu vinginevyo utaishi sio tu wewe peke yako bali na mashetani na wanakuwa na uhalali 💯
 
Back
Top Bottom