Mume wangu ni material full. Lol
du! Kweli zege halilali, tayari washakupa habari? Huyu dogo bado sijamchagulia jina rasmi, nasubiri maumivu yapungue network irudi ndo nimtaftie jina.hata wewe ni material full kwake, Umemzalia dume unafikili mchezo. Mungu akubariki wewe na mwanao. tatizo mnawaitaga majina magumu watoto wenu. anaitwa nani vile!?...mia
Ngoja nichangie japo hayanihusu. Kuna dada alimpeleka best friend wake kwa kaka yake ili amuunganishie ili kaka amuoe huyo best friend na kumpiga chini mchumba aliyenaye kisa hawaivi. Wamefika kwa brother, yule binti ambaye ametoka familia bora saaana kaanza nyodo,
Binti: Mbona nyumba yako ina joto sana,
Kaka: Umeme umekatika
Binti: Huna Generator?
Kaka: Nimeipeleka kufanyiwa service
Rafiki mtu kakazana kumkonyeza aache maswali yatamkosesha mchumba yeye anajifanya aoni, anaendelea
Binti: Unajua nimetoka kwenye gari, gari yangu ina AC kali sana...Baba amenambia nikimaliza undergraduate atanipeleka UK nikafanye masters.... Makochi yako mbona ya kizamani...
Kwani kijana alikubali kumuacha mchumba wake, thubutu.
Ni movie lakini ya kinaigeria inaitwa " Jealous Lovers"
haa haaa
unasemaje kuhusu PAT ?
nafikiri ni better kuliko hata Nonso...
kimada material unaweza kum upgrade akawa wife material
its all about upgrade...
Mimi nimekuwa bendera sasa hivi. Kwa kweli Pat ni bomba kuliko hata John nini Nonso. Nimeshaangalia movie zake karibu zote in a month. Ana vutia aswaaa.
Ukimu upgrade kimada material utamweza wewe??? Tayari yuko juu ka dege la Obama wewe unataka uendelee kumpaisha. Kimada material unatakiwa umshushe; ili awe wife material siyo ku up grade. Akikwambia ooh mi nataka lunch Serena unampeleka pale nyuma ya Posta hataki achape lapa.