Je! Marekani itaishambulia Iran?

Je! Marekani itaishambulia Iran?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,720
Mzozo wa Iran na Marekani ndio habari ya dunia sasa. Katika makala tatu za mda mrefu ambazo niliandika juu ya Korea, Syria na Iran, nilisema kuwa Syria lazima ivamiwe na kuwa uwanja wa vita maana Syria alikuwa mshirika wa Iran mkubwa katika Mashariki ya Kati, na baadae vita hiyo kuhamia Iran, kuna baadhi hawakunielewa na wengine wakanipinga sana.

Sasa tumeona kuwa Syria imedhoofishwa sana kiuchumi, haina uwezo wa kijeshi tena, nchi hiyo imekuwa ni uwanja wa makombora ya Marekani, Urusi na Israeli, na raia wengi wa Syria wameikimbia nchi hiyo.

Trump alivyoingia madarakani, Marekani ikaanza kuishinikiza kijeshi serikali ya Pyoyang ya Korea Kaskazini, pressure ilikuwa ni kubwa sana kiasi wengi wakajua vita itatokea, ila nilisema kwamba hapo hakuna vita bali Iran ndiyo itageuziwa kibao cha ghafla maana ndiyo mlengwa mkubwa.

Watu hawakunielewa wakati huo ila baadhi tu. Ila wote tuliona Marekani inaiwekea Korea vikwazo vikali sana halafu ghafla Marekani iligeuka na kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran, mkataba huo ulikuwa unakibali cha umoja wa mataifa na umoja wa Ulaya kwamba Iran iache kurutubisha madini ya Uraniam[nyuklia] na kuahidiwa kupata misaada na Iran ilitii, na mzozo uliisha na Iran ikaanza kufanya biashara na nchi za Magharibi.

Lakini Trump alipoingia madarakani alidai Iran inakiuka na hawezi kuiamini, hivyo akajitoa katika mkataba huo na kuiwekea Iran vikwazo vya kiuchumi, na akatishia kuiwekea vikwazo nchi zote ambazo zitaiunga Iran mkono kiuchumi. Baadae alifanya hilo jambo lililofanya nchi za Ulaya kujitoa kufanya biashara na iran, na Ujerumani ambayo ilionesha kupinga ilitishiwa kuwekewa vikwazo pia ikatii.

Trump aliongeza vikwazo vikali sana ambavyo sasa vinaifanya Iran nayo ianze kujitutumua kukabiliana na vikwazo vya Marekani, na kuitishia mno Serikali ya Washtong. Iran haukuishia hapo iliteka meli ya Uingereza mshirika wa Marekani pamoja na kusumbua meli za mafuta za washirika wa Marekani, na ikadaiwa imeishambulia meli ya mafuta ya Marekani pamoja na kudungua drone ya upalelezi ya Marekani, kisha kushambulia kituo kikuu cha mafuta huko Saudia Arabia.

Jambo hilo liliipa Marekani sababu ya kuongeza vikosi katika ghuba ya Uajemi ili kulinda maslahi yake na washirika wake. Marekani ilisogeze kwenye ghuba ya Uajemi U.S.S. Abraham Lincoln air craft carrier ambayo ilikuwa katika bahari ya Meditaranian, jumla zikawa aircraft carrier mbili na nyambizi za chini ya maji pamoja na Meli za mashambulizi, aircraft carrier zote zimebaba ndege za kutosha za aina mbalimbali. Marekani ana base 800 za kijeshi duniani, na base ambazo zipo mashariki ya kati zinakadiriwa kuwa na wanajeshi 70,000, na zote zimeizunguka Iran. Hizo basi ni kama ifuatavyo.

1. Afghanistan: Kuna wanajeshi 14,000 jumlisha wanajeshi 8,000 wa NATO.

2. Bahrain: Kuna zaidi ya wanajeshi 7,000 wengi ni wanajeshi wa majini ambao wanalinda usalama katika ghuba ya uajemi huko Bahrain.

3. Iraq: Kuna wanajeshi 5,200 kwajili ya kulinda makampuni ya mafuta ya Marekani pamoja na kupambana na wanamgambo wa Isis.

4. Jordan: Kuna vikosi 2795

5. Kuwait: Kuna vikosi 13,000

6. Oman: Kuna wanajeshi kama 100, hii base imekuwepo toka 1980.

7. Qatar: Kuna vikosi 13,000, na sasa base hii ipo katika mchakato wa kupanuliwana kuongeza wanajeshi Zaidi.

8. Saudia Arabia: Kuna vikosi lakini idadi yao haitajwi, lakini November 19 Trump alitangaza kuongeza wanajeshi 3000 kwajili ya kupambana na uchokozi wa Iran huko Saudia.

9. Syria: Kuna vikosi 2000, lakini Trump alitangaza kuvitoa na kubakiaza wanajeshi 800 kwajili ya kulinda maslahi ya mafuta huko.

10. Uturuki: Base hii ina siri kubwa sana, mara nyingi hawataji idadi ya wanajeshi kwasababu eneo hilo ni strategic location, ila hapo kuna base kubwa sana ya anga.

11. United Arab Emirates: Kuna vikosi 5000 hapo.

Pia eneo hilo kuna base kadha wa kadha ambazo ni za siri, hazisemwi kwajili ya usalama wa kijeshi. Na sasa Marekani imepeleka vikosi 3000 Iraq kwajili ya kuongeza nguvu dhidi ya ushawishi wa Iran baada ya kufanya shambulizi dhidi ya Suleimani; na Trump amesema yupo tayari kupeleka wanajeshi 120,000 katika ghuba ya uajemi kama Iran itazidi kuleta vitendo vya uchokozi.

Msuguano wa Marekani na Iran ni mkubwa sana huko mashariki ya kati, kama tunakumbuka mwaka 2017 Trump alifanya ziara kubwa sana huko Saudia na huko alikutana na nchi karibu zote zenye itikadi ya Kisuni pamoja na mashekhe wa kisuni kupanga mkakati mmoja dhidi ya Iran-mshia na washirika wake.

Wote walikubaliana katika azimio la kuwa pamoja na Marekani kupambana na Iran, na serikali ya Trump ikapitisha budget kubwa ya silaha za kivita kwa mataifa hayo. Tokea hapo tunaona mashambulizi yanaongezeka juu ya Iran na Iran pia inajibu mashambulizi kwa mashiriki wa Marekani. Saudia nayo imeingia vitani huko Yemeni na huko wamekutana na Iran katika uwanja wa vita, kwa kweli Saudia imevuruga nchi hiyo lakini nayo imepata hasara kubwa ya kupoteza wanajeshi wengi na kituo chake cha mafuta kushambuliwa.

Marekani ndiyo anafaidika katika vita hivi, na anatumia mgogoro wa shia vs suni kujijenga kijeshi na kiuchumi katika kanda hiyo.

Mashambulizi ya Marekani.

Marekani imemuua Al-baghdadi kiongozi wa isis msuni, tendo hilo limeivua Marekani lawama kuwa inaunga mkono vikundi vya kigaidi. Na gafla lawama zimeigeukia Iran na wana mgambo wa Hezbollah wa Lebanon kuwa ndio magaidi, Hezbollah ni kikosi cha kishia huko Lebanon kinachoungwa mkono na Iran, ni kikosi hasimu kwa Israeli na Marekani pamoja na wasuni.

Hezbollah na Iran wapo Syria wakiumuunga mkono Assad, lakini lengo lao kuu ni kujipatia base za kijeshi kwajili ya kuishambulia Israeli; Wayahudi kwa kutambua hilo, hawalali, daima urusha ndege zao kushambulia vikosi vya Iran na Hezbollah. Iran imejitanua huko Syria na sasa imejiingiza Iraq ambako kuna Washia wengi na wasuni wachache, washia wanaunga mkono Iran na wasuni wanapingana na Iran.

Wanamgambo wa Hezbollah wamejingiza Iraq kwa mgongo wa Iran kwajili ya kuliunga jeshi la Iraq dhidi ya Isisi lakini ajenda ni kwenda kinyume na Marekani huko Iraq, ndipo Serikali ya Washington DC ikahamua kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya wanajeshi wa Hezbolah na Iran katika kambi yao huko Kataib Iraq, waliuawa wanajeshi 25 katika shambulio hilo la Dec 30.

Iran kuona hivyo ikajipanga kuleta machafuko huko Iraq kwa kupitia wananchi wanaoiunga Iran mkono walivamia ubalozi wa Marekani na kuanza kutupa mabaruti ya moto. Jambo hilo liliikasirisha Marekani, kibaya zaidi Marekani ikagundua mpango wa Iran wa kuleta machafuko zaidi Iraq ili Wamarekani washambuliwe na wananchi wa Iraq, na aliyekuwa nyuma ya machafuko hayo ni Qassim Suleyman jenarali mkuu wa jeshi la Quds force la Iran ambaye ni jenerali mkubwa sana huko Iran na alikuwa ni mtaalamu wa mashambulizi dhidi ya Marekani na Israeli na Saudia.

Huyu ndiye alikuwa mwanaharakati mkubwa wa kupambana na Marekani na washirika wake kwa mda mrefu sana, inasemekana ndiye alikuwa ni mkuu wa Hezbollah wa siri. Alitafutwa sana kuuliwa na alikoswa koswa kuuliwa mara nyingi tu hasa huko Syria, katika mashambulizi yaliyomlenga ilionekana amekufa lakini baadae aliibuka mzima, jambo hilo lilifanya aogopwe zaidi kama mtu wa ajabu.

Alikuja Iraq akitokea Syria kuendesha harakati za kupambana na jeshi la Marekani na ushawishi wake; Marekani kupitia makachero wake na rada zake waliona nyendo zote za Suleyman, walimuua kwa shambulizi la ndege hata kabla hajaanza harakati zake, walimuua pamoja na watu wake wa karibu. Baada ya hapo Marekani imetuma makomandoo 700 huko Iraq kulinda maslahi ya Marekani pamoja na ubalozi wake.

Nchi za kisuni kama Saudia pamoja na wasuni walioko Iraq hata huko Ulaya walifurahia sana kifo cha Suleyman.

Mpaka hapa tunaona dhahiri kuwa vita vinapiganwa baina ya Marekani na Iran, na Jeografia ya vita hivi ni Iraq, na vitakuja kuingizwa mpaka ndani ya Iran. Na wakati huo huo Iran inapigana na Israeli huko Syria, Israeli mara kwa mara wanashambulia kwa ndege vikosi vya Iran huko Syria.

Jiulize tu swali hili inakuaje Marekani ina muua ofisa wa nchi iliyo halali duniani kisheria na kimamlaka [sovereighty country]? Kwa upande wangu ni kwamba kitendo cha Marekani kutangaza kwamba jeshi la kimapinduzi la Iran ni kama kikundi cha Kigaidi ni kwamba kwa mujibu wa sheria za ugaidi, gaidi anapaswa kukamatwa ama kuuawa kabisa.

Hii ni moja ya sababubu kuwa vita ipo, pili Marekani imeamuru raia wake watoke mashariki ya kati hasa Iraq, mwenye akili lazima ajiulize kuwa amri kama hizi zilishatolea Iraq, Libya, Syria, baada ya hapo nchi hizo zikavamiwa. Ingawa Trump katangaza shambulio juu ya Suleyman ni kukomesha vita iliyotaka kuletwa na Suleyman lakini si kuanzisha vita nyingine, lakini kasema kama Iran itajibu mashambulizi hata nyamaza naye atashambulia kwa kishindo zaidi ikiwemo kumuua hata Ayatollah Ali Khamenei.

Hivyo Marekani ipo vitani na Iran, na tutegemee vita vikubwa sana zaidi ya vile vita vya Iraq hata kama havitapiganwa sasa, kuna uwezekano Urusi na Uchina kuingia vitani kwa kutoa msaada wa kijeshi ama moja kwa moja, vita hii itakosa mshindi, lakini imeonesha wazi kuwa Uchina na Urusi wapo tayari kuingia katika vita hivi, na tumeona mazoezi yao ya pamoja hapo juzi.

Kwa mujibu wa wachambuzi mbalimbali wanasema kuwa vita hivyo vitauporomosha uchumi wa dunia, maana nchi za ghuba ya uajemi ambazo ndizo wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani zitaingizwa katika vita na kuleta anguko la uchumi wa dunia.

Hili anguko la uchumi wa dunia litakuwa nusra kwa utawala wa kidini duniani, askofu wa Roma chini ya harakati zake za KIUKUMENE (EUCUMENISM) atapata fursa ya kuileta dunia katika wito wa Amani, na atapokelewa kama mjumbe wa Amani katika mataifa yaliyo dhoofishwa kivita na kiuchumi, na wakazi wa dunia wataimba wimbo huo wa Amani.

Hivyo maandamano ya Amani yatalindima dunia nzima, ambayo yatawanyang’anya wana siasa sauti na kuwapa maskofu na mashekhe pamoja na viongozi wa dini mbalimbali sauti ambao watakomesha vita kwa muda, litakuwa ni shirikisho kubwa la dini na serikali duniani, hivyo secularism itawekwa chini ya religionism.

Kwahiyo dini itachukua mkondo tena wa kuendesha siasa za dunia kama zamani katika zama za giza [dark ages]. Na unabii wa kuinuka kwa mpinga kristo na utawala wake wa zamani utatimia dhahiri. Utawala huo utaipeleka dunia katika hatima ya mwisho.

Maandiko yanasema kwamba juu ya utawala huo,

“Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako. [Ufunuo 18:8].”

Mungu akijalia kesho nitaleta historia ya Iran.

FB_IMG_1578246392119.jpeg
FB_IMG_1578246171173.jpeg
 
#BREAKING
IRGC commander Hajizadeh: All US military bases across the Middle East are within reach of #Iran... their forces in the region are like pieces of meat under the IRGC's teeth Iran on Twitter

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari ya zaaaaaaamaaaaaani yani zamaniiiii washasemaga hivyo.
Military base za U.S middle east ziko kwa target yao.
.
Wanasahau Israel yupo pale na ni pasua kichwa kuliko hata U.S mwenyewe, wanasahau military base za S.Korea na Japan wanasahau za Pakistan na India 😝😝😝 ni kiama
 
Iran hana ubavu wa kuthubutu kuchokoza mziki wa America.. Marekani ameshasema aguse maslahi yake au base yake yoyote aitakayo alafu wao watajibu kwa haraka na kwa nguvu ambayo haijawahi kuonekana popote pale duniani kwahiyo Iran iache singeli inatakiwa ijibu kama mwanamme kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom