Je kweli nimerogwa? Uko uchawi? Naomba msaada. Dada yenu kutoka ujerumani

henkel

New Member
Oct 17, 2011
4
1
Assallamu Aleikum!

Nimekuwa na bwanangu miaka 13 bila shida na watoto wawili.
Mara si mara, tulihamia mombasa na bwanangu kapata msichana wa kikamba.
Nikapata mimba na huyo msichana kasema nitaona kama utazaa.
Nilizaa mtoto akafariki. Kisha bwana kanifukuza na watoto, na isitoshe nikaambiwa nina maradhi ya moyo, figo mbovu, ini mbovu, sukari na pumu. Hivi napewa madawa mengi sana siptali ujerumani na wala sioni nafuu.
Mimi ni mtu ambaye pia nimeshika dini sana na siamini kuna uchawi, lakini watu wengi wasema kuwa miye nilitupiwa jini na huyo msichana.

Jamani naomba muniambiye kama haya mambo yako kweli na wapi tanzania nitapata mwalimu maarufu mzuri kwa kiislamu ?

Shukran.
 
Pole sana kwa yaliyokupata, usiamini sana mambo ya kishirikina cha msingi muombe Mungu akusaidie kutatua matatizo ako. Cha muhimu jitahidi uwe karbu na viongozi wako wa Dini watakupa ushauri mzuri
 
Mmmh pole sana ila waswahili wana mambo sana inabidi Mahona jaribu kuona viongozi wa ko wa dini na wazazi na watu wazima. Kama ulivyosema ww ni mcha Mungu muombe akuonyeshe njia na tiba ya maradhi yako, hilo ndio muhimu kama maradhi yatakuwa yameletwa na uchawi utakuwa umetibu na ww uko salama
 
Kuwa kweli umerogwa au hujarogwa hilo naweza kusema liko nje ya uwezo
wa wana JF, Kuhusu uchawi ni kweli upo. Unasema wewe unaamini dini, Hakuna
dini ambayo inapinga kuwepo kwa majini au uchawi kati ya dini hizi mbili yaani
uislamu na ukristo labda uwe Mshintu, budha, free.... n.k Ishu ya mwalimu
nzuri ni tata...... Nipm kwa ufafanuzi zaidi!
 
Pole sana Dada; Uchawi kweli upo lakini ukiuweka sana katika akili yako kwamba umerogwa unaathirika kisaikolojia. Jaribu kufanya vipimo vya kimaabara kwanza kabla ya kutafuta mwalimu kama unavyodai;Kama daktari (Doctor of Medicine) atakuambia yeye haoni ugonjwa hapo yawezekana kuwa kuna urogi lakini kama ugonjwa unaonekana na daktari kwa vipimo vya maabara hapo hakuna urogi. Narudia kusema, pole sana.
 
bibie kama kweli ni mcha Mungubasi lazima atakuwa unajua kuwa dini zote zinazungumzia uwepo wa uchawi,kuufuata au kutoufuata ni juu yako
 
Assallamu Aleikum!

Nimekuwa na bwanangu miaka 13 bila shida na watoto wawili.
Mara si mara, tulihamia mombasa na bwanangu kapata msichana wa kikamba.
Nikapata mimba na huyo msichana kasema nitaona kama utazaa.
Nilizaa mtoto akafariki. Kisha bwana kanifukuza na watoto, na isitoshe nikaambiwa nina maradhi ya moyo, figo mbovu, ini mbovu, sukari na pumu. Hivi napewa madawa mengi sana siptali ujerumani na wala sioni nafuu.
Mimi ni mtu ambaye pia nimeshika dini sana na siamini kuna uchawi, lakini watu wengi wasema kuwa miye nilitupiwa jini na huyo msichana.

Jamani naomba muniambiye kama haya mambo yako kweli na wapi tanzania nitapata mwalimu maarufu mzuri kwa kiislamu ?
Shukran.

Kwa kuwa umesema wewe ni mtu wa dini siamini kama huo ni uchawi, kwa sababu tunafahamu moja katika njia za kutoa uchawi ni kutumia maombi ya dini. Kama unafanyiwa maombi na ugonjwa hauondoki maana yake sio uchawi, ila ni magonjwa ya kawaida. kumbuka moja ya sifa ya kiumbe hai ni kuuguwa!!
Lakini kumbuka pia shida uliyonayo ni shida ambayo inawapata watu wengi sana hasa watu wanaoishi nchi zilizoendelea, na hata katika nchi zinazoendelea shida hiyo imeanza kuonekana sana.
Suala la kutishiwa na yule binti na hatimaye kupata magonjwa uliyonayo nadhani it was just coincidence. But inaonesha kwamba ulipata stress kubwa sana ile ya mume wako kukuasi na tena kukufukuza, na pia vitisho ulivyopata kutoka kwa huyo binti. But kisayansi inajulikana kabisa kwamba stress inaweza kusababisha abortion, kuzaa mtoto ambaye atafariki, kisukari na magonjwa mengine.
Na tena inafahamika wazi kuwa mtu akipata kisukari ni rahisi sana kupata complications za magonjwa ya moyo, figo, pumu (cardiac asthma), ini na kadhalika.
Nadhani mtafaruku uliotokea kwenye ndoa yako mpaka sasa bado upo na stress kwa kiwango chaa juu sana (sometimes unconsciously) na kama upo na stress ni vigumu kupata nafuu kwa dawa unazotumia kwa sababu stress inasababisha utoaji wa hormone fulani (catecholamines etc.) kwenye damu ambazo zinazidisha ugonjwa wa sukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine.
ushauri wangu ni kuwa badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao wanaweza wakakupa dawa ambayo inaweza kukudhuru zaidi, haswa kwa sababu una shida za ini na figo naomba jaribu kumuona social counseler au psychologist anaweza akakusaidia to coupe with the situation.
Mwisho jipe moyo wa matumaini, maisha ni safari yenye vituko vingi ambavyo ni vigumu kuvizuia lakini unaweza kuzuia madhara yake. UTAPONA
 
Assallamu Aleikum!

Nimekuwa na bwanangu miaka 13 bila shida na watoto wawili.
Mara si mara, tulihamia mombasa na bwanangu kapata msichana wa kikamba.
Nikapata mimba na huyo msichana kasema nitaona kama utazaa.
Nilizaa mtoto akafariki. Kisha bwana kanifukuza na watoto, na isitoshe nikaambiwa nina maradhi ya moyo, figo mbovu, ini mbovu, sukari na pumu. Hivi napewa madawa mengi sana siptali ujerumani na wala sioni nafuu.
Mimi ni mtu ambaye pia nimeshika dini sana na siamini kuna uchawi, lakini watu wengi wasema kuwa miye nilitupiwa jini na huyo msichana.

Jamani naomba muniambiye kama haya mambo yako kweli na wapi tanzania nitapata mwalimu maarufu mzuri kwa kiislamu ?

Shukran.

Henkel, pole sana kwa matatizo.

Ukweli ni kwamba hakuna dini yeyote inayoweza kuzuia wachawi wasikuloge.

Henkel kila tatizo lina mlango wa kutokea, nitafute nitakuonyesha mlango, na baada ya siku tatu urudi kwenye jukwaa hili utueleze maendeleo yako.
 
Shukran kwa majibu yenu.

Ila wengine wanaruka kuandika kabla kusoma maneno yangu vizuri, ndiyo majibu mengine naona hayaeleweki.

Kwanza sijasema nataka mganga kabisa , nilitaka mwalimu kama vile sheikh wa msikitini aniombeye na kisomo cha Rukiya.
Ndiyo nilikuwa naulizia mwalimu mzuri ambaye atakaye nisomee Rukiya.
Yani kwa wakristo ni priest na kwetu waislamu ni mwalimu ndiye mwenye kusoma.
Tafadhali wale walioruka na maneno ya mganga wasome vizuri kabla kujibu upuzi!!

Maradhai ninayo miaka tatu naelekea mwaka wa nne. Na napata matibabu ya hali ya juu hapa ujerumani.
Stress sina wangelikuwa madaktari washasema kitambo, hakuna stress ikabaki miaka nne.

Shukran
 
Naomba kuongezea kuwa, maradhi yangu mara daktari moja anaona mara daktari wapili hayaoni. Na ujerumani kwasifika kwa matibabu, lakini wamekuwa very confused!!!
Mimi miaka tatu nauguwa wala sijafika kwa mwalimu yeyote anisomee Rukiya. Lakini nilioteshwa kuwa nitasafiri tanzania kwa mwalimu sheikh ambaye atakaye nisomea na nitapata nafuu. Na huyo mwalimu apenda kuvaa kanzu nyekundu. Na ndiyo maana i got curious and asked if there is any famous Mwalimu in Tz ambaye afanya visomo vya Rukiya.
Sitaki mchawi wala mganga nataka Mwalimu Sheikh.

Shukran
 
Nimeongea na rafiki yangu Mkenya hapa kasema ni kweli Wakamba ni kiboko yao. Angalia namna nzuri ya kutatua tatizo.
 
Henkel Pole sana!
Kwa hakika matatizo yameganyika katika mafungu matatu.
1-physical
2-spiritual
3-mental

Kwa kua umehakikisha mwenyewe umepitibiwa bado haujapona.
Kweli usipate tatizo mtaalam utampata...subiri JF members wakushauri ikifikia mwisho wao. Ni PM kwa msaada makin Inshaallah.
Pia Mwalim au shaykh si sababu ya wao kuijua ilm hyo... iwapo ni wajuzi wa ilm hizo watakusaidia!.
Wallahu shafiy!
 
Assallamu Aleikum!

Nimekuwa na bwanangu miaka 13 bila shida na watoto wawili.
Mara si mara, tulihamia mombasa na bwanangu kapata msichana wa kikamba.
Nikapata mimba na huyo msichana kasema nitaona kama utazaa.
Nilizaa mtoto akafariki. Kisha bwana kanifukuza na watoto, na isitoshe nikaambiwa nina maradhi ya moyo, figo mbovu, ini mbovu, sukari na pumu. Hivi napewa madawa mengi sana siptali ujerumani na wala sioni nafuu.
Mimi ni mtu ambaye pia nimeshika dini sana na siamini kuna uchawi, lakini watu wengi wasema kuwa miye nilitupiwa jini na huyo msichana.

Jamani naomba muniambiye kama haya mambo yako kweli na wapi tanzania nitapata mwalimu maarufu mzuri kwa kiislamu ?

Shukran.

Bwana Yesu ni mponya, mwite naye atakuweka huru kwelikweli
 
Back
Top Bottom