S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Tafakuri.
Nini maana ya Demokrasia katika ndani ya vyama vya siasa?
Je, kuwafukuza baadhi ya wanachama ndani ya chama ni kukosa au ndo kuwa na Demokrasia?. Au inategemea na walivyofukuzwa?.
Baada ya Chama Kikongwe Afrika cha CCM kutangaza kuwa baadhi ya wanachama wake kuwafutia uanachama kwa kile kinachodaiwa kuwa ni WASALITI mjadala umepamba moto. Wapo wanaounga mkono na pia wapo wanaoupinga uamuzi huo.
Ukifuatilia kwa kina kama ilivyo nyuma ambapo baadhi ya vyama vya siasa vilishafanya maamuzi kama hayo, wengi ya wafuasi nadhani kwa kukosa vyanzo sahihi au kwa sababu ya mapenzi hawajui na hawana sababu za kutosha wanazopinga ama kwa kafukuzwa au kutofukuzwa kwa wanachama hao. Na huko nyuma kulitokea kwa baadhi ya vyama mjadala ukawa kama huu. Kwa hiyo, kwa wafuatiliaji wazuri wa siasa za Tanzania. Mjadala huu si mgeni kabisa.
Je, tunajipa muda kuangalia kwa nini wale wamefukuzwa?. Na kwa nini chama kimeamua kufanya hivyo kama kilivyofanya. Je, baadhi ya wanachama wakishafukuzwa tunajipa muda kutafakari kuwa walisitahili kufukuzwa kulingana na Katiba na taratibu za chama husika?.
Martin Luther Jr King, aliwahi kunena kuwa; mara nyingi yeye hupenda kuwahukumu watu kulingana na kanuni na taratibu walizojiwekea wao. Kwa mfano, kama chama lazima kiwe na katiba ambayo wanachama wake wanatakiwa wakifuate. Mtu akihukumiwa kinyume na katiba ya chama chake, na kweli ikaonekana wazi kuwa amehukumiwa kinyume na katiba, hapo unaweza kusema kweli huyu mtu hakutendewa haki.
Naona sisi tuna siasa za kwamba jambo lilelile likifanyika katika mlengo unaoutaka unaona ni Demokrasia na jambo lilelile likifanyika upande ambao wewe hauko huko unaona si Demokrasia hata kidogo. Mara nyingi huwa hatujipi muda wa kufuatilia kwa nini wale wamefanya hivyo, na utaratibu wao uko kama walivyofanya? Yaani katiba na taratibu zao zinaweza zikawa sawa kulingana na wao walivyoamua?. Maana usihukumu watu au kundi la watu bila kuangalia utaratibu wao ulivyo.
Japo kuna mambo ambayo yako katika haki za msingi za binadamu na vyama vyote huzingatia kama kuheshimu haki ya kuishi kwa mwenzako bila kujali amevunja taratibu za chama au la.
Vichekesho kwa vyama vyote nchini kuhusu Demokrasia.
Kitu cha kuchekesha kwenye siasa ya ndani ya vyama vyetu ni kwamba: maamuzi yaleyale ambayo yalifanywa na chama chenu na mkayashangilia lakini wenzenu wakiyafanya mnaona si sahihi lakini kwenu ni Demokrasia. Pia, nao wakisahau kuwa nao waliwapinga wenzao na kuwatetea kwa nguvu kabisa wale ambao wamewajibishwa na chama tofauti na wao. Je, nini maana ya Demokrasia
Nitawapa mifano michache ili kupata mwanga kwa jambo hili ninalolijadili. Chadema iliwatimua madiwani watano (5) wa Arusha kwa mpigo upande wa CCM ukapiga kelele na kusema si demokrasia.
Pia, Chadema iliwatimua viongozi waandamizi wakina Zitto, Mwigamba na Prof. Kitila Mkumbo na wengine wengi wakina Mchange, Juliana Shoza upande wa pili ukapiga kelele kuwa oooooh chama hiki hakina Demokraisa kabisa.
CUF nao walishawahi kutimua viongozi waandamizi kwa mfano, Mapalala aliyekuwa Mkiti na juzi wamemtimua Mkiti mwingine Prof. Lipumba. Wengi walipinga na kusema chama hiki hakina Demokrasia kabisa na kujaribu hata kuwakingia kifua waliofukuzwa na vyama husika.
Hali kadhalika NCCR ilishawahi kumtimua Mkiti wake Mrema na viongozi waandamizi. Wengi hasa upande ambao si wa huko waliona chama hiki hakina Demokrasia kabisa. Je, demokrasia ni nini hasa ndani ya vyama vyetu?.
Juzi, CCM walifanya hivyo na wengi hasa walioko nje ya CCM wamepiga kelele kuwa oooooh wameonewa hao watu. Je, demokrasia ni nini ndani ya vyama vyetu.
13/03/2027.