Je, Kugawa Pedi Shule ya Viziwi Ndivyo Vipaumbele vya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma?

Infiltrator

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2017
Posts
205
Reaction score
333
Nimestaajabu kuona mtu mwenye hadhi ya ubunge akijihusisha na matukio yanayofaa kufanywa na mjumbe wa nyumba kumi, huku akijinasibu mitandaoni.

Je, hili ni “funika kombe mwanaharamu apite” au ni dharau kwa wananchi? Je, wabunge mnadhani hatujitambui?

Mbali na nafasi yake ya ubunge, huyo mshangazi ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma.

Wanawake wa Dodoma, kama huyu ndiye kiongozi wenu, kuna haja kubwa ya kujitafakari; kwa kifupi, hajitambui kabisa!
Hali kama hii inaleta maswali makubwa kuhusu uwazi na vipaumbele vya ziara za wabunge.

Wananchi wanatarajia uwajibikaji, si matukio yanayoonyesha ukosefu wa utambuzi hadharani.

Neema Majule (Mshangazi), jitafakari sana; matukio yako ya mchongo hayana nafasi katika hadhi ya ubunge.
 
Attachments

  • IMG-20260225-WA0111(2).jpg
    IMG-20260225-WA0111(2).jpg
    91.3 KB · Views: 4
sijaelewa, kwa nini uko against wanawake (watoto) kusaidiwa ''pedi'' ? ...

Sidhani kama umeelewa hoja yangu vizuri. Sipo dhidi ya watoto wa kike kusaidiwa pedi, hilo ni jambo jema na la kibinadamu. Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kupinga msaada kwa wanafunzi wa kike, hasa wenye mahitaji maalum.

Hoja yangu ni kuhusu vipaumbele na hadhi ya nafasi ya ubunge. Mbunge ni mtunga sera, msimamizi wa bajeti na mwakilishi wa wananchi katika masuala makubwa ya maendeleo. Tunatarajia aoneshe mchango wake katika kutatua changamoto za kimfumo, si kujinasibu kwa matukio madogo yanayoweza kufanywa na viongozi wa ngazi za chini au taasisi za kijamii.

Aisha, tatizo zaidi linakuja pale tukio linapogeuzwa ajenda ya kujitafutia sifa kana kwamba huo ndio uzito wa kazi ya ubunge.

Kwa kifupi, sipingi msaada. Nahoji uongozi na mwelekeo wa vipaumbele.
 
Viti maalum wanawake mpaka kupeleka pedi shule ya viziwi🤣 huyo hajui majukumu yake...

Then, aache mara moja kumhusisha Rais wetu kipenzi katika siasa zake za kukurupuka.
 
Sidhani kama umeelewa hoja yangu vizuri. Sipo dhidi ya watoto wa kike kusaidiwa pedi, hilo ni jambo jema na la kibinadamu. Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kupinga msaada kwa wanafunzi wa kike, hasa wenye mahitaji maalum.

Hoja yangu ni kuhusu vipaumbele na hadhi ya nafasi ya ubunge. Mbunge ni mtunga sera, msimamizi wa bajeti na mwakilishi wa wananchi katika masuala makubwa ya maendeleo. Tunatarajia aoneshe mchango wake katika kutatua changamoto za kimfumo, si kujinasibu kwa matukio madogo yanayoweza kufanywa na viongozi wa ngazi za chini au taasisi za kijamii.

Aisha, tatizo zaidi linakuja pale tukio linapogeuzwa ajenda ya kujitafutia sifa kana kwamba huo ndio uzito wa kazi ya ubunge.

Kwa kifupi, sipingi msaada. Nahoji uongozi na mwelekeo wa vipaumbele.
Upo sahihi kabisa
 
sijaelewa, kwa nini uko against wanawake (watoto) kusaidiwa ''pedi'' ? kwa nini ni jambo baya hadi ufure namna hiyo? ...
Hao walevi wa Dar hawaelewi mengi tu ya maana yanayofanyika hapa duniani.

Pengine hana dada hivyo hawezi kuwa na ruhuma kwa jinsia ya kike.
 
Nimestaajabu kuona mtu mwenye hadhi ya ubunge akijihusisha na matukio yanayofaa kufanywa na mjumbe wa nyumba kumi, huku akijinasibu mitandaoni.

Je, hili ni “funika kombe mwanaharamu apite” au ni dharau kwa wananchi? Je, wabunge mnadhani hatujitambui?

Mbali na nafasi yake ya ubunge, huyo mshangazi ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma.

Wanawake wa Dodoma, kama huyu ndiye kiongozi wenu, kuna haja kubwa ya kujitafakari; kwa kifupi, hajitambui kabisa!
Hali kama hii inaleta maswali makubwa kuhusu uwazi na vipaumbele vya ziara za wabunge.

Wananchi wanatarajia uwajibikaji, si matukio yanayoonyesha ukosefu wa utambuzi hadharani.

Neema Majule (Mshangazi), jitafakari sana; matukio yako ya mchongo hayana nafasi katika hadhi ya ubunge.
Charity begins at home.

Hongera sana Mh. Neema Majule.
 
Back
Top Bottom