Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
Umemaliza kaziNyalandu alikimbia ukatili wa Meko, sasa meko is no more ni haki yake kurudi.
Ni nyumbu tu atakayebaki chademaJE, HOJA ZA MHE NYALANDU ZIMEJIBIWA?
Na Elius Ndabila
0768239284
Leo Mhe Nyalandu aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amerudi CCM katika Mkutano mkuu maalum uliofanyika hapa Jakaya Kikwete Convention. Mhe Nyalandu anarudi CCM baada ya kujivua uwanachama wa CCM tarehe 30/10/2017.
Kama ilivyo kwa watu wengine wanapohama Chama kimoja kwenda kingine huwa wanakuwa na sababu lukuki zinazowafanya kuhama vyama vyao. Ndugai naye akiwa anaondoka na kujivua ukada wa CCM alielekeza shutuma kuwa Katiba ya nchi si rafiki. Alisema kuwa mihimili haijitegemei.
Maswali ya kujiuliza ni kuwa Mhe Nyalandu hoja zake alizokuwa akizisimamia zimefanyiwa kazi? Je, Nyalandu aliukimbia utawala wa hayati Magufuli au aliikimbia Katiba? Kama ni Katiba mbona bado ni ile ile aliyoikimbia? Je, Mhe Nyalandu anaamini katika utawala au katika Katiba?
Mhe Nyalandu, aliyewahi kuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano wakati anatimukia CHADEMA alisema kupitia taarifa yake kwamba amejuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama cha mapinduzi CCM ikiwemo ubunge wake.
Nyalandu alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola - Serikali, Bunge na Mahakama. Hizi zilikuwa ni tuhuma kubwa kutokea kutoka kwa mtu aliyekuwa ndani ya serikali ukimuondoa mzee Mrema.
Katika taarifa yake ya kujiuzulu aliyoiweka katika ukurasa wake wa Facebook ambayo hadi muda huu ninaandika hakuifuta, Nyalandu alisisitiza umuhimu wa nchi kupata katiba mpya.
Mhe Nyalandu alisema "Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali,"
Kwa hoja hizi za kuondoka kwa Mhe Nyalandu na kurudi tena leo CCM ingali bado hoja yake ya Katiba mpya haipo, Basi inaonyesha namna Wanasiasa wengi tulivyo na ndimi mbili. Inaonyesha namna Wanasiasa tunavyotumia fursa za Siasa vibaya. Nyalandu sasa anaowajibu wa kuwaeleza Watanzania kuwa sababu iliyomkimbiza CCM haikuwa Katibu mpya kwa mwamvuri wa Mhimili kuto kuwa independent bali alikuwa na sababu nyingine.
Ni vema kama Taifa tukajenga siasa za ushindani bila uzushi na kutengenezeana ajali.
CHADEMA kama chama hakipaswi kukataa wanachama kutoka vyama vingine lakini hakipaswi kuwaamini na kuwapa uongozi mpaka kwenye nafasi nyeti za kitaifa.CHADEMA wajifunze kupapatikia makapi ya CCM, la sivyo kitakuwa kinapiga hatua kumi na kurudi hatua 15 halafu wanajipongeza....
CHADEMA inawanachama waaminifu wengi Sana wenye uwezo wa kujitolea kwa jasho na damu..lakini ajabu wanawaacha na kubabaika na watu waliozoea kula kuku kwa mrija toka CCM.
JE, HOJA ZA MHE NYALANDU ZIMEJIBIWA?
Na Elius Ndabila
0768239284
Leo Mhe Nyalandu aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amerudi CCM katika Mkutano mkuu maalum uliofanyika hapa Jakaya Kikwete Convention. Mhe Nyalandu anarudi CCM baada ya kujivua uwanachama wa CCM tarehe 30/10/2017.
Kama ilivyo kwa watu wengine wanapohama Chama kimoja kwenda kingine huwa wanakuwa na sababu lukuki zinazowafanya kuhama vyama vyao. Ndugai naye akiwa anaondoka na kujivua ukada wa CCM alielekeza shutuma kuwa Katiba ya nchi si rafiki. Alisema kuwa mihimili haijitegemei.
Maswali ya kujiuliza ni kuwa Mhe Nyalandu hoja zake alizokuwa akizisimamia zimefanyiwa kazi? Je, Nyalandu aliukimbia utawala wa hayati Magufuli au aliikimbia Katiba? Kama ni Katiba mbona bado ni ile ile aliyoikimbia? Je, Mhe Nyalandu anaamini katika utawala au katika Katiba?
Mhe Nyalandu, aliyewahi kuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano wakati anatimukia CHADEMA alisema kupitia taarifa yake kwamba amejuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama cha mapinduzi CCM ikiwemo ubunge wake.
Nyalandu alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola - Serikali, Bunge na Mahakama. Hizi zilikuwa ni tuhuma kubwa kutokea kutoka kwa mtu aliyekuwa ndani ya serikali ukimuondoa mzee Mrema.
Katika taarifa yake ya kujiuzulu aliyoiweka katika ukurasa wake wa Facebook ambayo hadi muda huu ninaandika hakuifuta, Nyalandu alisisitiza umuhimu wa nchi kupata katiba mpya.
Mhe Nyalandu alisema "Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali,"
Kwa hoja hizi za kuondoka kwa Mhe Nyalandu na kurudi tena leo CCM ingali bado hoja yake ya Katiba mpya haipo, Basi inaonyesha namna Wanasiasa wengi tulivyo na ndimi mbili. Inaonyesha namna Wanasiasa tunavyotumia fursa za Siasa vibaya. Nyalandu sasa anaowajibu wa kuwaeleza Watanzania kuwa sababu iliyomkimbiza CCM haikuwa Katibu mpya kwa mwamvuri wa Mhimili kuto kuwa independent bali alikuwa na sababu nyingine.
Ni vema kama Taifa tukajenga siasa za ushindani bila uzushi na kutengenezeana ajali.
Nyalandu kama Mt zero walidhani wakienda Chadema watapata nafasi ya kugombania urais. Ni tabu sana kuona watu kama hawa wanaendeshwa na fursa
Anyways tusimlaumu sana, hawa ni wana siasa na kusema kweli nje ya ccm kwa sasa Tanzania hakuna mtu mwingine anafanya siasa. Wamepigwa pini maisha hayaendi, acha waende huko labda watapata nafasi ya kufanya siasa. Vyama vya upinzani kwa sasa ni kama vimekufa tu. Inatakiwa moyo wa kipekee kukomaa navyo. Ikiwa dhamira ni masalhi na ujiko huwezi dumu kwenye vyama vya upinzani sasa hivi.
Eeee, Ndugai kahamia wapi, na lini?Ndugai naye akiwa anaondoka na kujivua ukada wa CCM alielekeza shutuma kuwa Katiba ya nchi si rafiki. Alisema kuwa mihimili haijitegemei.
Nyalandu aishukuru CoronaHayupo hayupo tena na hatarudi , Sasa Nyalandu hana wa kumuogopa amerudi tena, baada ya kuona muasisi wa siasa chafu kaenda zake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kahamia Chachandu.Eeee, Ndugai kahamia wapi, na lini?