Je, hizi zinaweza kuwa ni sababu za ongezeko la UTI?

Rose Bud

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
252
256
Kwa miaka ya hivi karibuni watu wanaokuwa diagnosed na UTI imeongezeka maradufu. Katika kutafuta sababu nimekuja na sababu tatu ambazo zinazoweza kuchangia.

Wakuu, je wewe unadhani ipi ni sababu kubwa kwa ongeze la ugonjwa huu kati ya hizi

A: Ongezeko la mwanawake wa sikuhizi kushindwa kujisafisha au maji si masafi.
B: Ongezeko la madaktari ku diagnose magongwa ya sehemu za siri kuwa ni UTI hatakama si UTI.
C: Ongezeko la ngono kinyume na maumbile.
 
Hayo mengine nakuachia wewe..

Turudi kwenye uzi, unaposema haswa madaktari kudiagonise magonjwa ya sehemu za siri kuwa ni UTI hata kama si UTI. Kwa lugha nyepesi, unasema Madaktari wanakosea.

Kabla ya yote, anayechunguza Uwepo wa UTI si Daktari, bali mtaalam wa Maabara. Yeye atakuandikia kipimo, utaambiwa kalete mkojo kisha atachunguza na kutuma ripoti ya alichokiona. Daktari ataitafakari na kutoa hitimisho.

Kwanza, unapaswa kuelewa kuwa Daktari anakutibu kulingana na maelezo na dalili zako. Usipokuwa muwazi na pengine huduma ya Maabara hakuna, unaweza kuwa na ugonjwa fulani daktari akakutundika dawa za UTI kwa sababu hujataka kufunguka.

Pili, ni kweli UTI na magonjwa mengine ya zinaa huwa na dalili zinazoshabihiana. Mfano, UTI na kaswende zinaleta maumivu wakati wa kukojoa. Lakini ukiwa muwazi kwa mtaalam wako wa afya, basi atakutibu vema..

Tatu, wagonjwa mmekuwa wajuaji sana. Kila ukienda hospital unamuambia daktari nina UTI na ukiambiwa upime unalia sina hela. Daktari akishakusikiliza na anakuandikia matibabu. Dawa mmekuwa watumiaji holela.

Nne, wapo wenye UTI na STDs kwa pamoja.

Nahitimisha kwa kusema, uchunguzi wa Madaktari huelemea sana maelezo ya mgonjwa. Daktari hawezi kusema una UTI wakati dalili na majibu ya uchunguzi wako zinaonyesha uwepo wa bakteria wa Neisseria wanaosababisha Gono.
 
Miaka ya 1980 UTI ilikuwa wapi?
Miaka ya 80 uti ilikuwa inaitwa mkojo mchafu. Sasa ilipofika miaka ya 2000, madaktari wakaona neno mkojo mchafu lina sound kijima kijima bora wauite mkojo mchafu uti ili kuupandisha hadhi.
Kweli bwana sasa ukienda hospitali ukimwambia daktari hujielewi elewi unapimwa mkojo fasta hata kama unaharisha. Na majibu yakirudi (ndani ya dakika 10) jibu ni moja tu ni una uti kali. Daktari anakuandikia cipro na panadol lundo ukaugue pole.


Kwa hiyo:
1. Siyo wote wanoambiwa wana UTI wanayo UTI
2. Kipimo sahihi cha UTI kinachukua zaidi ya siku mbili
3. Matumizi holela ya antibiotics yana uhusiano na kuongezeka kwa UTI

Kwa maana nyingine
Point A, B na C za mleta mada zote zinachangia kupata UTI
 

Wagonjwa wanaojisemea wana UTI naona wanafikiri dawa za UTI (antibiotics) zitatibu gonjwa lolote walilokuwa nao
 
Wewe ni Dr wa afya au Phd??
 
Mapenzi kinyume cha maumbile ndio kisababishi kikuu cha maradhi yote ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Sehemu ya haja kubwa inamlundikano wa virusi wengi zaidi kuliko mbele, hivyo nyuma kuna hatari kubwa Sana, ndio maana kuna ongezeko la uti, gono, kaswende na HIV
 
Demu ana makucha kama ya Kunguru unategemea atajisafisha vipi huko ikulu?? Ukiona demu ana hayo makucha hiyo ni kiashiria namba moja cha UTI sugu
 
Namba C
 
Sababu;
1. Matumizi yaliyo Kithiri ya Karatasi za chooni (toilet papers) . KWA UVIVU WA KUTUMIA MAJI KUNAWA.

2. Kukosha maumbile kwa mikono michafu kabla ya kukosha mikono halafu ukimaliza ndo unakosha mikono kwa sabuni.

3.Kutokunywa maji ya kutosha kwa kuogopa/ UVIVU wa kwenda maliwatoni mara kwa mara.

4..kuto kwenda haja ndogo kwa wakati na badala yake kuibana kwa muda mrefu.

5.UCHAFU SEHEMU HIZOOO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…