MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Tarehe 25 August 1919 ilikuwa ni siku ambayo Jeshi letu la Polisi lilianzishwa rasmi kupitia Serikali ya Kiingereza ambayo ilitangaza katika Gazeti la Serikali kuwa Jeshi la Polisi Tanganyika limeanzishwa rasmi.
Makao Makuu ya Jeshi hilo yalikuwa Wilayani Lushoto chini ya uongozi wa uongozi wa Major S.T DAVIS mpaka mwaka 1930 yalipohamishwa kuja Dar es Salaam.
Baada ya uhuru, Jeshi letu la Polisi lilianza kubadili mwelekeo toka katika kutumikia Wakoloni na kuamua kuwatumikia Wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi.
Katika kuwatumikia wananchi, Tunu/Vithaminiwa (Core Values) vya Jeshi la Polisi vikawa ni Ujasiri (Courage), Uadilifu (integrity), Utiifu (Loyalty) na Haki (impartiality).
Kwa muktadha huu, ninaomba nijikite kwenye uadilifu na haki kama tunu za Jeshi letu la Polisi kwa sababu ni hatari sana kwa jamii iwapo Jeshi la Polisi litafanya kazi nje ya haki na uadilifu.
Kilichonifanya kuandika mada hii ni pale nilipoona jeshi letu la polisi linafanya kazi ya kuendeleza (promote) biashara ya Lugumi Enterprises kupitia crime scene tape.
Inafahamika Jeshi letu la Polisi halikuundwa katika msingi wa kufanya biashara au kuendeleza(promote) biashara au mfanyabiashara. Jeshi letu limeundwa ili kutenda haki katika misingi ya uadilifu, ujasili na utiifu.
Kwa kutumia fikra finyu, Maamuzi haya ya Polisi yanaweza kuonekana hayana madhara lakini ukitumia fikra pana, maamuzi haya yanaliweka jeshi letu la polisi katika mazingira ya ukosefu wa uadilifu na haki.
Jeshi lolote hapa duniani ambalo lina uadilifu na linatenda haki, haliwezi kuruhusu taasisi yake kuwa promoter wa biashara ambazo kesho linaweza kuwa sehemu ya kuzifanyia uchunguzi au kuzipeleka mahakamani.
Uwepo wa Polisi unahitaji imani kubwa kutoka kwa wananchi. Katika taasisi yoyote ambayo uwepo wake unahitaji kuaminiwa sana na jamii, ni hatari sana kwa taasisi hiyo kuanza kujihusisha (promote) kwa karibu na taasisi nyingine ambayo utendaji wake uko nje ya kazi zake au uwezo wake.
Kwa mfano, Kama mmiliki wa Lugumi enterprises, mfanyakazi au kampuni itafanya makosa, let's say, kuua, kusababisha ajali ya kifo au utapeli. Hivi polisi watazitumia crime scene tape ambazo zinapromote Lugumi enterprises kwenye crime scene?
Kama huko mbele ya safari Lugumi enterprises itathibitika ina kashfa au kufirisika, hizo stock za crime scene tape wataendelea kuzitumia? Nani atabeba gharama zake kwa sababu hazitakuwa na maana tena katika kutangaza biashara ya Lugumi enterprises kwenye crime scene.
Polisi haioni inajiingiza kwenye matatizo ya kukosa imani kwa wananchi kwa kuendeleza (promote) Lugumi enterprises halafu kesho ikagunduliwa ni matapeli.
Polisi haioni kuwa haiwatendei haki wafanyabiashara wengine ambao ni competitors wa Lugumi enterprises wakati kodi za makampuni yao zinatumika katika kuliendesha Polisi ili litende kazi katika msingi wa Haki na Kuaminiwa.
Ni nani aliyeridhia hili wazo la kuendeleza (promote) biashara ya Lugumi enterprises kwa kutumia polisi kupitia crime scene tape?
Ni nani anayetaka kubinafsisha Jeshi la Polisi ili liwatumikia wafanyabiashara badala ya kutoa haki?
Wabunge wetu, ninaomba mniulizie hili suala kwa serikali kwa faida ya taifa.