Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Nilifanya mazungumzo na kada na kiongozi fulani (jina kapuni) wa CCM kuhusiana na mwenendo wa siasa nchini, aliniambia jambo moja tu kwamba; wanachama wa CCM wamechoshwa na namna chama chao kinavyodumazwa na mtu mmoja anayedhani chama ni Mali yake na kusahau kwamba chama ni cha watu, na kinatakiwa kiongozwe na watu.
Kada huyo mkongwe amesema hata Mwl. Nyerere hakuwahi kukifanya chama hiki kama Mali yake, amedai miaka hii watanzania wana ulimbukeni na u...levi wa madaraka. Aliongeza kwa kusema kuwa miaka yote ya CCM, sasa hivi chama kimepata kiongozi mzigo, asiyejua hata kesho ya chama chake, anayedhani yeye ni wa maana sana kuliko chama, akamalizia kwa kusema kwamba, muda utasema na siku sio nyingi watu watajipiga vifua kwa hasira na kutoa ya moyoni.