Je, CCM imejiandaa kushindwa mwaka 2015???

Je, CCM imejiandaa kushindwa mwaka 2015???

talentbrain

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,187
Reaction score
760
Habari za mapumziko marefu ya sikukuu za Muungano na Maulid ya kuzaliwa Mtume Mohammad (S.A.W). Tumerudi tena katika harakati zetu za maisha ya kila siku kama ilivyoada. Sitapenda kuwachosha ngoja niende kwenye hoja moja kwa moja.

Mwaka 2015 kutakuwa na uchaguzi mkuu kwa Tanzania yetu na kama tunavyofahamu kuwa chama chochote kinaweza shinda. Kushindwa kwa upinzani huwa hakuna matatizo makubwa zaidi ya kupinga na maandamano madogomadogo. Ila ninapojaribu kupiga picha jinsi CCM itavyochukulia kushindwa kwake napata wasiwasi.

CCM imeshawekeza sana katika utawala huu kiasi kwamba wanadhani wanahati milki ya kuitawala Tanzania milele. Siwaoni wakijiandaa kuweka misingi ya yeyote anayeshinda kukabidhiwa madaraka bila tatizo. Sasa nikipiga picha naona vurugu zinazoweza kupelekea machafuko kama watanzania wataamua kuwapatia madaraka upinzani.

Najaribu kukumbuka vurugu kadhaa huko Mwanza na Arusha pale ilipobainika wazi kuwa wamepokonywa ubunge tu. Walijaribu kuweka kila hila na hatimaye vurugu zikatokea. Je, urais??? Je, wamejiandaa kuwa chama cha upinzani???Kila nikitafakari na kuona jinsi wanavyofanya maovu kwa nchi hii wakitegemea kulindwa na serikali yao, ndipo naamini hawa jamaa hawataachia madaraka bila fujo.

Hivi wanaoliibia taifa mabilioni ya fedha, wanaomaliza Tembo na Faru wetu?? Je, wanaofaidika na biashara za madawa ya kulevya kwakuwa wanalindwa na utawala huu!!! Nikitazama jinsi watu wanavyotumia CCM katika kuishi isivyo halali nabaki kuamini kwamba watu hao hawatakaa waache madaraka kirahisi tu.

Je, tunasababu ya kuwaacha CCM watawale daima ili kuepusha vurugu za kuachia madaraka???

Hapana na haiwezekani kuogopa kuwaondoa wahalifu kwakuwa tu tunataka amani ya woga. Tusipowaondoa sasa watajaondolewa baadae tena wakiwa wamewekeza zaidi katika nguvu za kuleta vurugu. Wamelitendea mabaya mengi taifa na hawavumiliki tena.

Hii ni picha kubwa nimeyopiga!!!!
 
habari za mapumziko marefu ya sikukuu za muungano na maulid ya kuzaliwa mtume mohammad (s.a.w). Tumerudi tena katika harakati zetu za maisha ya kila siku kama ilivyoada. Sitapenda kuwachosha ngoja niende kwenye hoja moja kwa moja. Mwaka 2015 kutakuwa na uchaguzi mkuu kwa tanzania yetu na kama tunavyofahamu kuwa chama chochote kinaweza shinda. Kushindwa kwa upinzani huwa hakuna matatizo makubwa zaidi ya kupinga na maandamano madogomadogo. Ila ninapojaribu kupiga picha jinsi ccm itavyochukulia kushindwa kwake napata wasiwasi. Ccm imeshawekeza sana katika utawala huu kiasi kwamba wanadhani wanahati milki ya kuitawala tanzania milele. Siwaoni wakijiandaa kuweka misingi ya yeyote anayeshinda kukabidhiwa madaraka bila tatizo. Sasa nikipiga picha naona vurugu zinazoweza kupelekea machafuko kama watanzania wataamua kuwapatia madaraka upinzani. Najaribu kukumbuka vurugu kadhaa huko mwanza na arusha pale ilipobainika wazi kuwa wamepokonywa ubunge tu. Walijaribu kuweka kila hila na hatimaye vurugu zikatokea. Je, urais??? Je, wamejiandaa kuwa chama cha upinzani???kila nikitafakari na kuona jinsi wanavyofanya maovu kwa nchi hii wakitegemea kulindwa na serikali yao, ndipo naamini hawa jamaa hawataachia madaraka bila fujo. Hivi wanaoliibia taifa mabilioni ya fedha, wanaomaliza tembo na faru wetu?? Je, wanaofaidika na biashara za madawa ya kulevya kwakuwa wanalindwa na utawala huu!!! Nikitazama jinsi watu wanavyotumia ccm katika kuishi isivyo halali nabaki kuamini kwamba watu hao hawatakaa waache madaraka kirahisi tu. je, tunasababu ya kuwaacha ccm watawale daima ili kuepusha vurugu za kuachia madaraka??? hapana na haiwezekani kuogopa kuwaondoa wahalifu kwakuwa tu tunataka amani ya woga. Tusipowaondoa sasa watajaondolewa baadae tena wakiwa wamewekeza zaidi katika nguvu za kuleta vurugu. Wamelitendea mabaya mengi taifa na hawavumiliki tena. Hii ni picha kubwa nimeyopiga!!!!
una mtazama kama wangu, lakini mapinduzi si lele mama, hakuna mtu aliyekuwa madarakani tena kifidasadi atakuwa tayari kuachia madaraka kwa wapinzani. Maana kuna kuwa na uwezekano mkubwa wa kuozea jela
 
Una matatizo ya kupumzika kwenu ambako hakuna mawasiliano!
Hebu cheki na makao makuu ya chama chako juu ya mfupa uliowakwama shingoni, achilia mbali kushiriki uchaguzi wa 2015!!
 
Una matatizo ya kupumzika kwenu ambako hakuna mawasiliano!
Hebu cheki na makao makuu ya chama chako juu ya mfupa uliowakwama shingoni, achilia mbali kushiriki uchaguzi wa 2015!!

Hivi umeielewa mada?? Au unajibu tu?? Jipe muda na uisome mada na kuielewa.
 
Una matatizo ya kupumzika kwenu ambako hakuna mawasiliano!
Hebu cheki na makao makuu ya chama chako juu ya mfupa uliowakwama shingoni, achilia mbali kushiriki uchaguzi wa 2015!!
mfupa upi? au unamaanisha wale mamluki tuliowatimua? wale walishasahaulika ktk ulimwengu wa siasa!
andikisheni daftari la wapiga kura muone moto wa cdm! na pro ccm wote mngeaibika sana ktk huu uchaguzi mdogo kama daftari lingeboreshwa!
 
Tangu enzi ya Nccr yenye nguvu ulishawhi kuwasikia viongozi wake wakisema wakichukua nchi kutatokea vita au vurugu!?,

Enzi za Cuf yenye nguvu ulisikia wapi wakisema ikitokea wameshka nchi hii bsi vurugu n vit vitatokea!?

Leo Cdm yenye nguvu nani unamsikia anasema labda ikiingia madarakani wataanzisha vita na vurugu!?

Lakini nyakati zote Ccm wamekuwa wakihubiri kwamba wapinzani wakichuku nchi vita n vurugu kubwa itatokea'

Kauli hii ni sawa na kusema tukishindwa hatutakubali kuachia nchi n vurugu kubwa itatokea, jamaa hawapo tayari kabisaaaaaaaaaa ila lazima tulazimishe utayari wao.

unapohitji kubadilika yapo mambo mawili
1. mabadiliko chanya
2. mabadiliko hasi
huu upande wa 2 ukiuogopa tu kwa swala kama hili basi utakuwa mtumwa daima' kam tuna mipango n tumedhamiriia tuangalie yetu na yao kwa tahadhari
 
Hivi umeielewa mada?? Au unajibu tu?? Jipe muda na uisome mada na kuielewa.
Mkuu abstract yako ni wishful thinking, na kama nilivosema awali, wakati wewe una concentrate na na kuzi blow up tiny negatives ambazo si general, unaacha kufikiri namna ya kuendeleza utawala bora wa ile alternative unayoifikiria, iliyojaa wazinzi, wezi na walevi wa madaraka hata kabla hawajaonja utamu wa dola!

It is radher naive on your part kufikiri CCM itaondolewa madarakani by an unknown outfit ambao wana run chama kama saccos binafsi, you are underrating Tanzanians!
 
Mwenyekiti wa CCM kitaifa, alishaanza kuwagusia CCM kuwa waanze kujianda kisaikolojia kukubali kushindwa 2015. Ushauri wangu kwa upinzani na wao waanze kujianda kisaikolojia ya kuwa 2014 na 2015 serikali za mitaa na serikali kuu zote zitakuwa mikononi mwao na waache kuwaza kama bado ni wapinzani katika kupanga mipango yao kuanzia sasa. Mipango ya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014: Viongozi wa upinzani lengo ni 70%(+) upinzani na 30%(-)CCM. Na lengo hili liwe kwa uchaguzi wa wabunge na madiwani 2015. Uchaguzi wa Rais usitutishe sana maana serikali kwa maana halisi huongozwa na bunge.
 
Safari hii mshindi ndio atakaye tangazwa kuwa mshindi. Hila zote zitashughulikiwa maana hakuna dhambi kubwa na mbaya kama uoga. Sasa kama Mbwai na iwe mbwai.
 
Mwenyekiti wa CCM kitaifa, alishaanza kuwagusia CCM kuwa waanze kujianda kisaikolojia kukubali kushindwa 2015. Ushauri wangu kwa upinzani na wao waanze kujianda kisaikolojia ya kuwa 2014 na 2015 serikali za mitaa na serikali kuu zote zitakuwa mikononi mwao na waache kuwaza kama bado ni wapinzani katika kupanga mipango yao kuanzia sasa. Mipango ya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014: Viongozi wa upinzani lengo ni 70%(+) upinzani na 30%(-)CCM. Na lengo hili liwe kwa uchaguzi wa wabunge na madiwani 2015. Uchaguzi wa Rais usitutishe sana maana serikali kwa maana halisi huongozwa na bunge.

Haya ndio maneno yaliyo jaa busara ya hali ya juu. Viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wanapaswa kuyazingatia. Hizi propaganda kuwa kuna mpasuko baada ya kufukuza mapandikizi ya watawala zisiwatoe watu kwenye track kuelekea ushindi.
Cc Tumaini Makene
 
Last edited by a moderator:
Watashindaje 2015 wakati hata Mgombea Urais anayekubalika bado kizungu-mkuti.
 
Back
Top Bottom