Je, baada ya Urusi kumsaidia Trump kuingia White house, Marekani ipo salama kwa kiasi gani?

Lancashire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,057
10,366
Wadau habari za muda huu,
Najaribu kutafakari na hatua ambazo Rais Donald Trump anachukua kwa sasa na matokeo yake kwa wamarekani na ulimwengu kwa ujumla.

Sote tunajuwa kwamba Urusi aliinjinia uchaguzi mzima wa marekani na kuhakikisha Trump anakuwa rais wa taifa hilo.Hii ilikuwa confirmed na FBI na CIA mpaka Rais Obama wakati huo aliamua kuvunja mahusiano ya kibalozi na Urusi kwa kuwafukuza maafisa wa kidiplomasia wa Urusi walioko Washington DC.

Tuna maswali kadhaa ya kujiuliza lengo la Urusi kumsaidia Trump kuingia White house ni lipi? Uhusiano kati ya Urusi na Marekani unafahamika toka kumalizika kwa vita baridi.
Kwa sasa Trump ameanza kazi na anachukua hatua ambazo kwa namna moja au nyingine ni ngeni machoni pa wamarekani na walimwengu wengi kwa ujumla. Je zinaweza kuwa na matokeo gani kwa taifa la marekani na dunia kwa ujumla?
Je wakuu bado tunaamini marekani ni salama?
Hebu tuje na hoja zenye mantiki katika hili suala.
Karibuni sana
 
Si kweli ni unafiki na ujinga wa Obama wa kuleta siasa za akina Yahya Jammeh wa Gambia, .

Kwa kifupi Obama anaweka mazingira magumu ya kazi kwa Trump, ili baadaye aseme kuwa USA hawakumsikiliza alipowaambia Trump hafai.

Ila ni unafiki wa Obama, mama Clinton na Democratic., kutaka kushinda hata kwa nao la mkono ila ikashindikana.

Mfano, wamehesabu kura, bado ni bila bila Trump anaongoza sasa hapo huoni kabisa kuwa ni fitina na hujuma anayofanyiwa na mafia Obama?

Any way huu mchezo wa kiobama ni hatari sana kwa nchi yake; kwa sasa yeye anaweza ona anamkomoa Trump, ila akawa anaweka jipu kwa USA kwa ujumla japo mwisho wa siku watakujakuona wazi kabisa kuwa aliyesababisha hasara ni Obama na Democratic wenzake.
 
Mi nampenda Mke wake na asili yake na msimamo wake wa kutaka kuwa balozi wa USA nchini Czech Republic
 
Hatua mbaya aliochukua Trump juzi juzi ni kusaini kujitoa TPP, TPP ni Mkataba wa Ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi za Pacific, Wacha Russia na China wakenue, mara moja China amekuja na mpango wa Asia- Pacific trade relations Russia yupo mlango wa uani anahema vizuri, hilo ni pigo kubwa sana Marekani katika historia ya biashara
 
Si kweli ni unafiki na ujinga wa Obama wa kuleta siasa za akina Yahya Jammeh wa Gambia, .

Kwa kifupi Obama anaweka mazingira magumu ya kazi kwa Trump, ili baadaye aseme kuwa USA hawakumsikiliza alipowaambia Trump hafai.

Ila ni unafiki wa Obama, mama Clinton na Democratic., kutaka kushinda hata kwa nao la mkono ila ikashindikana.

Mfano, wamehesabu kura, bado ni bila bila Trump anaongoza sasa hapo huoni kabisa kuwa ni fitina na hujuma anayofanyiwa na mafia Obama?

Any way huu mchezo wa kiobama ni hatari sana kwa nchi yake; kwa sasa yeye anaweza ona anamkomoa Trump, ila akawa anaweka jipu kwa USA kwa ujumla japo mwisho wa siku watakujakuona wazi kabisa kuwa aliyesababisha hasara ni Obama na Democratic wenzake.
Mkuu hili suala CIA wamekiri kwa ni kweli hata FBI sasa uwongo hapo uko wapi?
 
Kwa msaada huu wamarekani inabidi wajikaze ktk hili maana mengi yaja ktk msaada huu.
Na hilo ndo la msingi Urusi ana mipango ya kuiteremsha marekani kutoka kuwa superpower. Na dalili tumeshaanza kuziona.hatua anazochukua Trump toka ale kiapo Ijumaa tarehe 20 January 2017.
 
Hatua mbaya aliochukua Trump juzi juzi ni kusaini kujitoa TPP, TPP ni Mkataba wa Ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi za Pacific, Wacha Russia na China wakenue, mara moja China amekuja na mpango wa Asia- Pacific trade relations Russia yupo mlango wa uani anahema vizuri, hilo ni pigo kubwa sana Marekani katika historia ya biashara
Mkuu na huu ni mpango uliosukwa kumuweka Trump ili kuhakikisha marekani anakufa kiuchumi. Lakini naamini kuna Kitu kitafanyika bado kuna muda kidogo.
 
Pale wabongo wanapokutana kijiwe cha kahawa na kujadili mambo yaliyo nje ya uwezo wao wa kufikiria!..
Kosa unalofanya ni kudhani akili/fikra ulizo nazo wewe za kuvukia Barabara ( zebra crossing) kila mmoja yupo kama wewe.
Kama mada imekuzidi unaweza kukaa kimya mkuu
 
CIA na FBI wamethibitisha kwamba Urusi wali hack system ya uchaguzi ya Marekani na kumsaidia Trump.
Acha owongo na ushabiki wa kijingaa...Urusi wali hack email za bi clintoni na system za DNC,wakaonyesha ni jinsi yani DNC walimkandamiza Beni sanders na kumpendelea Clinton...Urusi hawakuweza kugusa mifumo ya kupiga na kuhesabu kura ya Marekani...Kama hujui kitu iliza,sio kuleta ushabiki na upotoshaji.
 
Trump ni pandikizi na wasipokuwa makini wataumia. Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa taifa kama la Marekani.
Hakuna pingamizi lolotee hapo...Russia hawana uwezo wa kupandikiza raisi marekani...Sera za nje za marekani zipo palepale,na kwa taarifa yako matekani inaendeshwa kutikea Pentagon,Hakuna chochote kitachobadilika kwe sera za nje kijeshi,even Putin knows that...Hata sanctions zitabaki palepale...Acheni u ndezi
 
Russia hajahusika kwa chochote juu ya uchaguzi wa US zaidi ya kupick side kama ambayo siku zote dunia inafanya pale panapotokea uchaguzi marekani russia walikuwa upande wa Trump kwa sababu ya misimamo binafsi ya trump si ya chama dhidi ya russia ndio wakaona ni mtu anayefaa lakini hakuna kitu walichofanya juu ya hacking kwenye saver za tume ya uchaguzi wa USA na inajulikana trump ameshinda kwa kura za watu wachache crinton ameshinda kwa kundi la kura za wengi na amemzidi trump zaid ya kura milion 2 na kura za watu wachache zinajulikana idadi na mshindi anatangazwa akipata kura zaid ya 270

Swala la Obama kujitoa kwenye lawama juu ya kushindwa kwa chama chake Dems na juu ya lawama za kambi ya bibi Clinton kwa vyombo vya usalama vya US kama FBI ambavyo Obama ni kiongozi wao kama Rais na ndie vyombo vyote vipo chini yake na ma DG's wake wameteuliwa na Obama sasa inabidi waje na sababu za kusingizia kuwa russia anahusika na kuingilia mifumo ya uchaguzi wa US ambao kwa kura za popular vote bibi Clinton ameshinda na wao walikuwa wanajua uchaguzi huu ni lazima watashinda na walikuwa wamejipanga kuanzia kifedha na kipropaganda na vyombo vyote vya habari vikubwa dunian walkuwa upande wao sasa baada ya kushindwa wamechanganyikiwa na wanataka uchaguzi urudiwe au wanataka ule mzigo wa lawama wawapatie wengine ndo maana wakaja na ushaidi dhaifu sana juu ya Russia kuingilia mifumo yao ya uchaguzi
1 Jina la kikundi kilichokumika kuhack ni APT 28 au Fancy Bear na APT 29 au Cozy Bear note APT inasimama kama Advanced President threats vikundi hvyo viko chini ya serikali ya Russia
2 Pia wnasema GRU na Jeshi la Urusi kitengo cha Cyber army wapo nyuma ya APT 28 au ndo code name yao
3 Pia wanasema FSB kitengo cha ujasusi cha Russia ambao makao makuu yake ni majengo ya iliyokuwa KGB zamani wapo nyuma ya APT 29 au ndo code name yao
4 Pia wanaamini APT 28 walivamia saver za DEM's kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2015 na APT 29 walivamia saver za DEM's kipindi cha kipupwe mwaka 2016
note ; ktk swala la kijasusi au kiupelelezi inatakiwa uje na details kamili si kutaja ma code names na kama kitu umeamua kuweka adharani ni lazima kila mtu ajue sasa code name za nini? kwa nini wasije na Tarehe ,mwezi kamili baada ya kusema majira ??
5 Pia wanaamini APT 28 ndio waliohack emails za Bib clinton na za DEM's na kuwapa Wikileaks wazichapishe kitu ambacho Julian Assange amekikataa
Kitu ambacho kinanichanganya na kunipa wasiwasi mimi juu ya hizi habari na kwa nini zinatangazwa japo ni aibu kwa serikali ya Taifa kwa kuonyesha udhaifu wa upande wa cyber security wamekubali kutangazwa dunia nzima wajue wakat kuna mambo makubwa sana ya hacking yametokea hapa lakini wameficha iweje hii watangaze tena kwa promo kubwa?
 
Back
Top Bottom