maganjwa
JF-Expert Member
- Sep 11, 2012
- 2,789
- 2,327
Nina pata shida sana kichwani kiongozi mkubwa wa taifa anapowaambia wana wa nchi kwamba tulinde amani yetu na kusema amani ni tunu ya taifa je ni kwa makusudi au hajui kwamba amani kweli si tunu ya taifa ila ni matokeo ya tunu ya taifa.
Kwa sababu nimetafakari sana bila haki hakuna amani je hawajui hilo kweli? bila maadili na miiko hakuwezi kuwa na utulivu wa kisiasa katika nchi. je hawajui hilo? wanaiba mali ya wananchi huku wakisema tulinde amani yetu hii mana yake nini? Angalia richmond, meremeta, kiwira, EPA, na sasa escrow huku wanasisitiza tulinde amani yetu jamani huku wahujumu wanapeta amani itike wapi kama sio kutia hasira
jamani tusaidiane mimi amani ni matokeo ya kufuata tunu ya taifa inayozaa haki na haki ikitamalaki amani ndio hushamiri na watu kuwa imani na serikali yao huku wakiwa na uhakika mambo yanakwenda vizuri.
Karibuni kwa mjadala