JAYRUTTY aonyesha IRIZAR la Simba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,469
Reaction score
14,773
Mkurugenzi wa Kampuni ya JAYRUTTY akiwa amepiga picha na basi litakalotumiwa na kampuni hiyo katika uuzaji wa jezi za Simba pamoja na promosheni mbalimbali zinazohusiana na Klabu ya Simba. Tukio hilo limefanyika nchini China, ambapo maandalizi yote yamekamilika, na basi hilo linatarajiwa kuingia majini kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.


Wakati huo huo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyanzo vyakuaminika, basi la Simba aina ya IRIZAR pia tayari limeshanunuliwa na linatoka nchini Hispania, kama ilivyoahidiwa. Hata hivyo, kutokana na changamoto za njia ya maji kutoka Ulaya, njia ya usafirishaji imebadilishwa. Kutokana na mabadiliko hayo, basi la Simba IRIZAR linatarajiwa kuwasili Dar es Salaam mwezi Februari mwaka huu.

Your browser is not able to display this video.
Zaidi
 
Hiyo picha I wapi?
 
Isije tu ikawa ni muendelezo ule ule wa maigizo kwa mashabiki na wanachama wa hiyo timu! Hata kwenye ule uchaguzi wa kipindi kile, Manzoki alikuja kutoka China!
 
Kilio kipo pale pale, kitachobadilika sasa ni michozi kuililia ndani ya "Irizar ya mchongo" badala ya Yutong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…