January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Tanesco kweli ni tamu. Wanakusanya zaidi ya trillion 2 kwa mwezi sawa na zaidi ya shilingi trillion 24 kwa mwaka. Hii ni karibu sawa na bajeti ya mwaka ya nchi ya Tanzania. Yaani tanesco ndiyo Tanzania. Wanavyoitumia pesa yote hiyo wanajua wenyewe. Hata gawio la serikali hawalipi. Mitambo yao ya kuzalisha umeme wananunuliwa na serikali. Kwa mfano huo mradi wa NHPP ambao gharama yake ni trillion 6 tu serikali ilibidi kukopa nje ili kuugharimia.

Hizo wiki mbili za Makamba zimegeuka kuwa miaka. Na bei ya umeme wanapanga kuipandisha mara dufu, yaani wawe wanakusanya trillion 48 kwa mwaka ndipo waache hiyo katakata ya umeme. Yaani hadi waizidi bajeti ya serikali. Bunge la tanesco ambalo ndiyo hupitisha bajeti ni hiyo bodi yao iliyosheheni wafanyabiashara. Makamba ndiyo mkuu wa nchi hiyo inayoitwa tanesco. Wananchi wake wanampendaaa hadi raha.
 
Hizo wiki mbili bado hazijafika au?
 
Mimi nawalaani wote wanaohusika na kukatika umeme bongo! Hii si bahati mbaya ni makusudi yao kutesa watu , namuomba Mungu awape mwisho mbaya inshaallah!

Mbona enzi za Mwendazake umeme haukuwa ukikatika? Mbona ulaya umeme haukatiki? Shida si miundombinu chakavu shida ni wahusika wa ofisi ya nishati na madili yao ya kuuza Solar na Majenereta!

Haya majitu yenye madaraka bongo yana undugu na shetani yanatutesa sana wakati yanaishi kwa kodi zetu , tuko duniani hatuna raha sababu ya sera zao za kishetani, siku haya majitu yakifa huwa hakuna anaewalilia na always inajulikana yanapokelewa kuzimu na mashetani wenzao na kushangiliwa huko na mazombi, mazimwi, vibwengo, ibilisi na mapepo!!

Roho zao mbaya huwekwa mahali panastahili!

Enyi viongozi bongo kumbukeni duniani tunapita tu, tendeni haki siku zenyewe ni chache tu duniani, yuko wapi Mugabe na miaka yake ya kobe duniani, yuko wapi Patrice Lumumba? Yuko wapi Baba wa taifa? Yupo wapi Mandela? Sote tunaenda tu! Ila kupokelewa ndo hatujui!
 
Shida ni wahusika
 
Aibu iseee hii nchi uwongo tumefanya uwe sehemu ya maisha..
 
Kumbe yamuda mrefu ningeshangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…