Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,411
Habari za januari rafiki yangu?
Mwezi huu unakwendaje kwa upande wako? Ni mwezi bora au ni mwezi mgumu kama wengi wanavyolia? Kumekuwa na kelele nyingi sana kila ifikapo mwanzo wa mwaka ya kwamba mwezi huu wa kwanza ni mwezi mgumu sana. Na mwezi huu umepewa majina mengi na tofauti, wapo wanaouita mwezi dume, wengine wanasema njaanuari, na maneno mengine kama hayo yanayoashiria kwamba mwezi huu sio sawa na miezi mingine.
Watu wengi wanalia kwamba mwezi huu wa kwanza ni mgumu sana, lakini kama unavyonijua mimi, kama tumekuwa pamoja kwa muda, huwa sipendi majibu rahisi, huwa sikubaliani na kitu kwa sababu kila mtu anakubali, bali napenda kuchimba ndani zaidi na kuupata ukweli wenyewe. Na katika hili la januari kuwa ngumu nimekuwa nalichimba kila mwaka kupata ukweli wenyewe wa mambo. Na leo hii nataka nikufahamishe ya kwamba , mwezi januari sio mwezi mgumu bali wewe mwenyewe ndiyo mgumu.
Kama mpaka sasa umekuwa unaamini mwezi januari ni mgumu, na kama mpaka sasa unatumia sababu ya mwezi huu kuwa mgumu kukuzuia kufanya mambo fulani muhimu kwako, unaweza usikubaliane na mimi. Lakini nakusihi uendelee kusoma na mwishoni utachagua kama kweli mwezi huu ni mgumu au wewe mwenyewe ndio umeamua kuwa mgumu. Mwisho tutashirikishana hatua muhimu za kuchukua ili uondokane na aibu hii ya kutumia mwezi januari kuficha uzembe wako mwenyewe.
PATA KITABU HIKI KITAKUSAIDIA SANA 2016.
Kwa nini mwezi januari unaonekana kuwa ni mwezi mgumu?
Mwezi wa kwanza unaonekana kuwa ni mwezi mgumu kwa sababu mbalimbali ambazo zipo wazi kabisa na kila mmoja wetu anazifahamu. Hapa tutashirikishana kwa ufupi sababu hizo.
1. Matumizi makubwa ya mwisho wa mwaka.
Mwisho wa mwaka huambatana na sikukuu mbalimbali kama krismasi, mwaka mpya na hata sherehe nyingine binafsi. katika kipindi hiki watu huwa na matumizi makubwa sana lakini uzalishaji unakuwa mdogo. Hili linachangia kwa kiasi kikubwa sana mwazo wa mwaka kuonekana ni mgumu kwa sababu hata akiba ambayo mtu alikuwa ameweka anakuwa ametumia kwenye msimu wa sikukuu
SOMA; Msimu wa Sikukuu Umekuacha ‘Mweupe’? Fanya Mambo Haya Matatu Kujikomboa.
2. Mahitaji makubwa ya mwanzo wa mwaka.
Pia mwanzo wa mwaka kuna mahitaji makubwa sana ya fedha na haya yanasababisha mwezi huu kuonekana kuwa mgumu zaidi. Kwa wale wenye familia na watoto ndiyo kabisa mambo yanaonekana kuwa magumu. Kuna ada za kulipia watoto shuleni, kuna kodi za nyuma za kulipa, kwa wale wanaopanga na mengine mengi. Haya ni muhimu na yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha, na hivyo hili kuchangia mwezi kuonekana mgumu zaidi.
3. Mategemeo ya kipato kimoja, ambacho kinawahi mwisho wa mwaka.
Kwa wafanyakazi ambao wanategemea mshahara peke yake kama chanzo kikuu cha kipato, mwezi huu unaonekana mgumu zaidi kwao. Hii ni kwa sababu mwezi disemba mshahara uliwahi kutoka, mapema kabla ya sikukuu ya krismasi, na fedha hizo zikatumia wakati wa sikukuu, hivyo tangu mwaka unaanza hakuna tena kipato kingine ambacho kimeshaingia, hapo mwezi unaonekana kuwa mgumu zaidi.
4. Mabadiliko ya kiuchumi.
Kutokana na mwisho wa mwaka kuwa watu wengi wana sikukuu, uchumi ni kama unabadilika kidogo, fedha nyingi zinakuwa zimepelekwa kwenye maeneo ya burudani na starehe na maeneo mengine yanakuwa hayafanyi vizuri. Hivyo hata baadhi ya wafanyabiashara ambao biashara zao haziendani sana na msimu wa sikukuu, wanajikuta wakishindwa kupata wateja wa biashara zao.
5. Mtazamo wa wengi.
Pia mwezi huu wa kwanza unaonekana kuwa mgumu kwa sababu mtazamo wa wengi umeshakuwa hivyo, kwamba huu ni mwezi mgumu na utaendelea kuwa mgumu. Tutajadili hili zaidi hapo chini.
Kwa nini januari sio ngumu bali wewe ndiyo mgumu?
Pamoja na sababu hizo zinazofanya mwezi januari uonekane ni mgumu, bado mimi nakwambia mwezi januari sio mgumu, bali wewe mwenyewe ndiyo umeamua kuwa mgumu. Na nina sababu za msingi sana z akudhibitisha hilo kwamba wewe umeamua kuwa mgumu, na mwezi huu unakuonesha ugumu huo ulioamua wewe mwenyewe.
Tujibu maswali haya kwa pamoja ili tuone kweli kama mwezi januari diyo mgumu au wewe mwenyewe umeamua kuwa mgumu.
1. Wakati unafanya matumizi makubwa mwisho wa mwaka ulikuwa unafikiri nini?
Jiulize wakati wa mwisho wa mwaka, wakati unafanya matumizi makubwa, na wakati huo ulikuwa hauna uzalishaji mkubwa, ulikuwa unafikiria nini? Ulikuwa unafikiri kwamba kuna muujiza utakaotokea na kufanya mahitaji yako ya januari kuyeyuka? Jipe jibu kwenye hilo.
2. Mahitaji yako ya januari umeyajua lini?
Kwamba januari unatakiwa kuwapeleka watoto shule na kulipia ada, taaifa hizi ulipewa lini? Tarehe moja ya mwezi wa kwanza?
Kwamba unatakiwa kulipa kodi ya nyumba mwezi wa kwanza, taarifa hizi ulipewa lini? Tarehe moja mwezi wa kwanza?
Yote hayo ulikuwa unayajua mapema kabisa kabla hata hujaanza kuwa na matumizi makubwa, lakini wewe uliamua kuwa na matumizi makubwa na kusahau haya ukifikiri labda yatapotea yenyewe, unaona unavyojiletea ugumu wa maisha?
3. Wakati unapokea mshahara wa mwisho wa mwaka mapema, hukujua unaofuata utachelewa?
Kwa kawaida umekuwa unapokea mshahara mwisho wa mwezi, halafu mwezi wa mwisho wa mwaka unapokea mapema zaidi, hapa si iko wazi kabisa ya kwamba mshahara unaofuata utachelewa? Hilo halihitaji uwe mjuzi wa hesabu, ni rahisi sana na iko wazi.
Kwa maswali haya na majibu yoyote ambayo umejipa, iko wazi kwamba mwezi januari sio mwezi mgumu bali wewe mwenyewe umeamua kuwa mgumu, kwa sababu hukujiandaa mapema kwa majukumu yanayokuja mbele yako na pia ulikubali kufanya matumizi makubwa mwisho wa mwaka bila ya kujali kwamba mwanzo wa mwaka mambo yatakuwa magumu.
Lakini mimi hali yangu ni tofauti...
Mimi sijafanya matumizi makubwa kwenye mwisho wa mwaka, tena kipindi hiko bado nilikuwa na hali ngumu. Ni kipati changu ndio kiko chini na hivyo kwa hakika januari ni ngumu kwangu. Huu ndio utetezi ambao najua umekuwa unautengeneza tangu umeanza kusoma makala hii. Na mimi bado nakusisitizia wewe kama rafiki yangu ya kwamba wewe umeamua kuwa mgumu.
Nakubaliana na wewe kwamba hukuwa na matumizi makubwa kwa mwisho wa mwaka na kipato chako ni kidogo ndio maana januari inakuwa ngumu kwako. Lakini bado nakuambia januari siyo ngumu, bali wewe ndio mgumu.
Twende taratibu, kwa kipato chochote ambacho umekuwa unapata kwa mwaka jana, kama ungefuata ule ushauri ambao nilikupa huko nyuma wa kujilipa wewe kwanza kabla hujafanya chochote, na kuchukua sehemu ya kumi ya kipato chako na kuweka mbali, leo hii mambo yangekuwa tofauti. Kama hukusoma ushauri ule usome japa; Unawalipa Watu Wote Kasoro Huyu Mmoja wa Muhimu
Na kama ungeamua kufuata ule ushauri wa JINSI YA KUTAJIRIKA KWA KUANZA NA SHILINGI ELFU MOJA, kwa siku 365 za mwaka 2015, leo hii ungekuwa na zaidi ya tsh laki nne kwenye uwekezaji wako. Usome ushauri huo kwa kubonyeza hayo maandishi, kama bado hujausoma.
Na kama kipati chako ni kidogo kweli yaani kidogo mpaka kinasikitisha, unafikiri ni nani ana jukumu la kukiongeza? Mwajiri wako? Kama jibu lako ni ndio, nakuambia rafiki yangu utaendelea kuwa na januari ngumu sana kwenye maisha yako yote. Kuongeza kipato chako hilo ni jukumu lako, na naweza kukuambia ndio jukumu kubwa unalohitaji kulifanyia kazi 2016.
Hata kama unafanya biashara na biashara yako inakuwa ngumu kipindi cha mwanzo wa mwaka kwa sababu wengi wanakuwa hawanunui, bado ni jukumu lako kujua mzunguko wa biashara yako na kuangalia ni jinsi gani unaweza kujiandaa vyema ili mambo kama haya yasikukute tena.
SOMA; USHAURI; Unawezaje Kuacha Kazi Yenye Maslahi Kidogo Na Kujiajiri?
Yote tuliyojadili hapa yanaanza na nidhamu ya fedha, na wala sio ukubwa wa kipato. Kwa kipato chochote ulichonacho sasa, ukiwa na nidhamu ya fedha utaweza kutoka hapo ulipo na kwenda mbali zaidi. Lakini kama huna nidhamu ya fedha, unakula kama unavyopata, unakopa kila mara, utazidi kujichimbia shimo na kila mwanzo wa mwaka utakuwa unaimba pambio lile lile.
Nakusihi sana rafiki yangu januari hii ya mwaka 2016 iwe ndiyo ya mwisho kwako kuimba wimbo huu wa aibu sana ya kwamba mwezi ni mgumu. Chukua hatamu ya maisha yako sasa, anza kuweka fedha kwa ajili ya mahitaji ya januari ya 2017 kuanzia sasa, na utaona jinsi maisha yako yatabadilika na kuwa bora.
Nakutakia kila la kheri katika kuondokana na hali hii ya kukosa nidhamu ya kifedha. Soma hizo makala zilizoambatanishwa kwenye makala hii na utajifunza mengi zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz