Janga la petroli duniani

Janga la petroli duniani

Joined
Jun 18, 2019
Posts
6
Reaction score
3
Wachambuzi wameonya kuwa shambulizi lililofanywa na ndege zisizokuwa na rubani (droni) katika vituo viwili vya mitambo ya kusafisha mafuta, inaelekea kuwa umezidi kuharibu uwezekano wa suluhisho kati ya Tehran na Washington, na huenda ukasukuma bei ya mafuta kufikia dola za Marekani 100 kwa pipa moja la mafuta.

Rais Trump ameonya Jumapili kuwa Marekani iko tayari kujibu mashambulizi yaliyofanywa kwa kutumia droni katika mitambo ya kusafisha mafuta nchini Saudi Arabia, ikisema Washington inajua nani aliyefanya shambulizi hilo.

"Tuko tayari kujibu mashambulizi lakini itategemea na uthibitisho utakaopatikana,lakini pia tunasubiri kupata taarifa kutoka Saudi Arabia juu ya yule aliyehusika na shambulizi hilo na makubaliano gani tutajibu shambulizi hilo”

Iran imekanusha kuhusika na shambulizi hilo la kutumia droni ambalo limeathiri uzalishaji wa mafuta kwa asilimia 5.

Waasi wa kikundi cha Kihouthi nchini Yemen wanaosaidiwa na Tehran wamedai kuhusika na shambulizi hilo, na kusema droni 10 zilitumika kushambulia vituo vya mafuta vya Abqaiq na Khurais, na kusababisha moto mkubwa. Kwa wiki kadhaa Saudi Arabia itakabiliwa na uhapa wa uzalishaji mafuta ghafi na gesi, maafisa wa Saudi wamesema.

Maafisa wa Marekani walitoa picha za satellite na kueleza habari za kijasusi zinazothibitisha kuwa Iran ilihusika na shambulizi hilo. Maafisa wa Marekani wanasema muelekeo na uwezo wa shambulizi hilo unaweka ulakini juu ya Wahouthi kuhusika.

Jenerali Amir Ali Hajizadeh, kamanda wa kikosi cha anga cha majeshi ya mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran, amesema Jumapili vituo au manuari za Marekani ziko kilomita 2000 ambapo makombora ya Iran yanaweza kuvifikia.

Shambulizi hili limekuja wakati Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa anafikiria kuondoa vikwazo juu ya Iran ikiwa ni hatua ya kuwahamasisha viongozi wa Iran kuingia katika mazungumzo kufikia makubaliano yanayotarajiwa kuzuia Iran kurejea upya katika hatua yake ya kuzalisha nyuklia.

Hatua ya Rais Trump kumfukuza kazi mshauri wake wa uslama wa taifa John Bolton – ikiwa inatokana na tafukuri ya rais, kulingana na ripoti za vyombo vya habari – ilileta matumaini kuwa angalau kutakuwa na uwezekano wa kupunguza mvutano uliopo kati ya Washington na Tehran.

Magazeti ya Iran yalifurahia kuondoka kwa Bolton, ambaye wamemtaja kama “moja wa maafisa wenye msimamo dhidi ya Iran” ambaye yuko karibu na Rais wa Marekani.Wachambuzi wanasema kuwa Marekani na Iran wako katika ncha ya mgogoro kamili tangu Rais Trump alipoiwekea vikwazo Tehran mwaka 2018, aliposusia mkataba wa kimataifa uliokusudia kudhibiti harakati za Iran kutengeneza silaha.
 
Umekuwa Aljazeera!
wachambuzi wameonya kuwa shambulizi
lililofanywa na ndege zisizokuwa na rubani
(droni) katika vituo viwili vya mitambo ya
kusafisha mafuta, inaelekea kuwa umezidi
kuharibu uwezekano wa suluhisho kati ya
Tehran na Washington, na huenda
ukasukuma bei ya mafuta kufikia dola za
Marekani 100 kwa pipa moja la mafuta.
Rais Trump ameonya Jumapili kuwa Marekani
iko tayari kujibu mashambulizi yaliyofanywa
kwa kutumia droni katika mitambo ya
kusafisha mafuta nchini Saudi Arabia, ikisema
Washington inajua nani aliyefanya shambulizi
hilo.
"Tuko tayari kujibu mashambulizi lakini
itategemea na uthibitisho utakaopatikana,
lakini pia tunasubiri kupata taarifa kutoka
Saudi Arabia juu ya yule aliyehusika na
shambulizi hilo na makubaliano gani tutajibu
shambulizi hilo”
Iran imekanusha kuhusika na shambulizi hilo
la kutumia droni ambalo limeathiri uzalishaji
wa mafuta kwa asilimia 5.
Waasi wa kikundi cha Kihouthi nchini Yemen
wanaosaidiwa na Tehran wamedai kuhusika na
shambulizi hilo, na kusema droni 10 zilitumika
kushambulia vituo vya mafuta vya Abqaiq na
Khurais, na kusababisha moto mkubwa. Kwa
wiki kadhaa Saudi Arabia itakabiliwa na uhapa
wa uzalishaji mafuta ghafi na gesi, maafisa wa
Saudi wamesema.
Maafisa wa Marekani walitoa picha za satellite
na kueleza habari za kijasusi zinazothibitisha
kuwa Iran ilihusika na shambulizi hilo. Maafisa
wa Marekani wanasema muelekeo na uwezo wa
shambulizi hilo unaweka ulakini juu ya
Wahouthi kuhusika.
Jenerali Amir Ali Hajizadeh, kamanda wa kikosi
cha anga cha majeshi ya mapinduzi ya Jamhuri
ya Kiislam ya Iran, amesema Jumapili vituo au
manuari za Marekani ziko kilomita 2000
ambapo makombora ya Iran yanaweza
kuvifikia.
Shambulizi hili limekuja wakati Rais wa
Marekani Donald Trump alikuwa anafikiria
kuondoa vikwazo juu ya Iran ikiwa ni hatua ya
kuwahamasisha viongozi wa Iran kuingia katika
mazungumzo kufikia makubaliano
yanayotarajiwa kuzuia Iran kurejea upya katika
hatua yake ya kuzalisha nyuklia.
Hatua ya Rais Trump kumfukuza kazi mshauri
wake wa uslama wa taifa John Bolton – ikiwa
inatokana na tafukuri ya rais, kulingana na
ripoti za vyombo vya habari – ilileta matumaini
kuwa angalau kutakuwa na uwezekano wa
kupunguza mvutano uliopo kati ya Washington
na Tehran.
Magazeti ya Iran yalifurahia kuondoka kwa
Bolton, ambaye wamemtaja kama “moja wa
maafisa wenye msimamo dhidi ya Iran”
ambaye yuko karibu na Rais wa Marekani.
Wachambuzi wanasema kuwa Marekani na Iran
wako katika ncha ya mgogoro kamili tangu Rais
Trump alipoiwekea vikwazo Tehran mwaka
2018, aliposusia mkataba wa kimataifa
uliokusudia kudhibiti harakati za Iran
kutengeneza silaha
 
Inatafutwa sababu ya kuharalisha uvamizi dhidi ya Iran.Aliyefanya shambulio ni American wenyewe.CONSPIRACY
 
Back
Top Bottom