Janga la Njaa litaendelea kuwepo Kama serikali haitatumia Busara

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Sijafurahia kuona Rais wetu akiendelea kutoa akauli zile zile kuhusiana na Janga la njaa bila kuwapa wananchi msaada au mbadala wowote.

Hivi sasa mvua zimeanza kunyesha katika mikoa mingi hapa Tanzania. Hasa ile mikoa iliyokuwa inanyemelewa na ukame kama vile Tabora, Shinyanga, mwanza, na Kagera. Ila Mvua kunyesha haimaanishi kuwa chakula kipo. Ndyo maana vyakula mpaka sasa vinaendelea kupanda bei.

Nimekuwa nikizunguka maeneo mbalimbali hasa vijijini ambako kumekuwa na ukame. Ingawa mvua zimeanza kunyesha toka mwanzo wa mwezi wa pili mpaka sasa, Wakulima wengi wamegoma au wameshindwa kupanda hasa Mahindi na Maharagwe kwa hofu ya ukame. Wengi nimekutana nao na kuwauliza ni kwanini hawalimi wakati mvua zinanyesha tena nyingi tu? Wengi wamedai kuwa hii hali ya hewa hawaiamini. Inawafanya wawe na hofu ya kukaukiwa mazao yao tena kama wakilima na mvua ikapotea. Wengine wamedai kuwa mbegu walitumia msimu uliopita sasa hawana mbegu au hawana uwezo wa kununua mbegu. Wengine kwa sababu ya njaa walikula mpaka mbegu walizokuwa wametunza.

Serikali haiwezi kila siku kuwa inatoa matamko yasiyo na msaada wowote bila kutazama kwa umakini tatizo halisi. Sio kuwa watu hawafamyi kazi. Kwani zamani walikuwa hawafanyi kazi au serkali ndyo ilikuwa ikiwalisha?

546a47a58f1de43eea4910380ae18de5.jpg

Serkali inabidi itambue kuwa Tanzania ilipatwa na Ukame. Hili sio janga la kulipuuza hata siku moja. Serkali itambue kuwa wakulima sasa wanahofu ya kukaukiwa mazao yao kama wakilima tena. Ni sawa na aliyeumwa na nyoka hata akikanyaga jani huhisi ni nyoka.

Serikali isijifanye kujitoa katika hili janga. Zipo njia mbadala za kutatua hili tatizo.

Kwanza ni kutumia Mamlaka ya hali ya hewa kutabiri na kuwahakikishia wakulima hali halisi ya mvua na hali ya hewa kiujumla. Hii itawasaidia wakulima kuwa na uhakika wa mvua au hapna.

Pili. Serikali iwape ruzuku wakulima hasa za Mbegu bora watakazoweza tumia kulima mazao ya muda mfupi na yenye kuhimili ukame.

Tatu, Serikali pitia wizara ya Kilimo itoe ushauri kwa wakulima wa maeneo mbali mbali nchini kulima mazao yanayoweza endana na hali ya hewa kutokana na eneo husika mkulima anapolima.
 
NImesikiliza Clouds redio leo wakisema Tanzania kuna UKAME lakini hakuna NJAA,nikajiuliza kama vijana wale wanajua nini maana ya UKAME,na kama kukiwa na UKAME zao gani linaota na kupata mazao??

Nikawashangaa vijana hawa wasivyoweza kutumia akili kwamba UKAME unaleta NJAA,bila mvua maana yake hakuna chakula.Kwa kilimo cha bongo ambapo tuantegemea mvua zaidi kuliko njia nyingine kama umwagiliaji wa mazao.
 
Clauds mm nlisha ucha kuckilza wala kuangalia Tv yao. Wanatia kinyaaa
 
Kama Haujawahi kulala bila Kula huwezi ielewa njaa. Wanasema mwafwaaaa. wamewahi kulala huku wakiwa na njaa? waache dhihaka.
 
wfp-world-food-programme-logo-flag-symbol-icon-CY22R0.jpg

Si udhaifu kuheshimu vyombo kama hivi.
Lakini kimsingi vina lemaza..hivyo tukomae hakuna njaa.
1440061797.png

Hapa ni ndani ya jiji la London,
Iwapo njaa itatokea watajistiri.
grain.jpg

Hivi ni vihenge vya kuhifadhia nafaka katika jiji la New York.

Kwa bongo yetu...katika miji mikubwa umeshawahi kuona sehemu inayoeleweka ya kuhifadhi nafaka?
Na kama kuna kihenge je? mmiliki ni nani?
 
Back
Top Bottom