Jana ya Tabora somo zuri sahihi kwa watawala wa leo

certified mdokozi

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
1,403
814
Zama uja na kupotea miji hufa na historia Yake ubaki kitu cha kuhadithiwa vizazi na vizazi kumbukumbu uleta simanzi nyingi sana......1581km kutoka MTWARA, 658km kutoka ARUSHA, 421km kutoka KIGOMA , 1027km kutoka DAR ...649km kutoka BUKOBA ...ilikuwa ikifika Tabora unahisi utofauti na hakika ungejiua umefika mji wa wanyamwezi mji wa WANARELI hasaaa ....

Hivi karibuni nilikuwa nyumbani Tabora kusalimia ndugu ...hali niliyoikuta inasikitisha sana Dunia ya leo ambapo bodaboda ni moja ya ajira kubwa kwa vijana kwa Tabora hali si hivyo utawaona vijana wengi bado na baiskeli zao wenyewe tukiziiita DALADALA na hii ndo ajira na vijana wachache sana ndo wamejiajiri kama bodaboda

Rais wetu ameingia madarakani kwa kutu ahidi Tanzania Ya viwanda ...kwa Tabora ukizungumza kiwanda una maana ni miundombinu Yake simaanishi kwamba hakuna uwezekano wa kuwa na viwanda ila kwa wakoloni pamoja na waasisi wa Taifa hili wakati wanaleta Muiano sawa wa uchumi katika kila pembe Ya nchi hii Tabora waliifanya kuwa ndo kiini cha usafirishaji kwa kanda zote (kanda Ya ziwa na kanda Ya magharibi ) wapo wanaodiriki kusema Tabora ndo katikati Ya Tanzania siwashangai sana mji ambao uchumi wake uliendeshwa kwa milio Ya honi ...

Ilikuwa ukisikia mlio wa honi asubuhi basi ujue Treni kutoka DAR imeingia Bidhaa mbali mbali zingeingia vijana wa muda huu walikuwa wamechangamka hasa msururu wa Taxi nje Ya stesheni vijana waliobeba biashara mbalimbali .....wageni wangepata chai uji na MAKOPA yetu (Mihogo Ya kuloweka ) basi ilikuwa burudaani hali ingekuwa hivi hivi kwa treni kutoka mpanda mwanza na kigoma ...

Hali hii ilipelekea mkoa wetu kuwa wa uchumi mkubwa sana pesa ilibadirisha mikono na mikono ...kilimo hatukuwa nyuma watu walipiga kazi na ulikuwa na uhakika mazoa Yako kufika sokoni Dar au Mwanza ...ni kwa muktadha kama huu hata Taasisi zingine ziliimalika kuanzia shirika la posta mabank kutaja kwa uchache wake ...

Jioni wazee wangekaa kwenye vilinge vya kahawa wakipeana habari juu ya samaki zilizoingia kutoka kigoma au mchele uliongia kutoka mpanda wanacho ongea leo sitaka hata kukuhadithia wazee wa kuruka debe huu ndo ulikuwa mji hasaa pilika pilika za mwanaisungwi, muziki mzuri wa Tabora jazz pale Tabora hoteli na ungeleta fujo ulikuwa unapigwa ngumi hasa na vijana walioshiba hawa walikuwa makuli kwenye Godown mbalimbali stesheni au mafundi wa karakana vijana wa leo wananyanyuma vyuma kutukaba asalalee .....

Hatujawah iangusha CCM ila nasikitika haijawah kutuonesha mkono wa msaada pale tunapotaka kudondoka kwa sasa nadhani mkoa huu ni miongoni mwa mikoa yenye wabunge vijana nafikiri wanaona taab wanayopata vijana wenzao na namna wanavyokimbia mji...Little has been done ila there so much to do wakati tunapozungumzia viwanda kuna sehemu ziangaliwe kwa jicho pana sana ...

Lakini ni wasaa muafaka kuangalia aina ya viongoz wanaopelekwa kwenye huu mkoa ambao mm naona sasa ni kama umekufa na Watawala wanatumia kujaribia viongoz mbalimbali leo mtu akipata kazi akapewa post Tabora anaonekana kapata demotion kuna vijana wengi wazuri wazawa wenyenguvu na uwezo fanisi wa kuuokoa huu mji wapeni nafasi msihangaike sana kuwaomba watu waje watujengee viwanda vya asali alakishen reli (SGR ) maana hizi barabara mnajengea wenzetu wachache wanaoongeza maroli kila siku
 
Tabora

Poleni sana wana wa Mboka Manyema

Lakini hayo ni matunda ya uoga,, uoga umasikini,, hebu angalieni mikoa ambako watu wao waliamua kukipa kisogo chama, wakasadiki upande wa pili, maisha ki ujumla kwao ni nafuu kuliko kwenu.. Tizama mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Mara,Tanga,Kagera,Mbeya,Mwanza na sasa Mtwara na Morogoro... Hakuna machozi kama huko kwenu...

Hamjachelewa kama hawawapi walichowaahidi wabwageni tu..
 
maendeleo ya tabora itachukua muda sana, tena kwa msaada mkubwa wa watu wa kuja. maendeleo huletwa na elimu na tabora kabla ya ujio wa shule za kata, mkoa ulikuwa na shule ya sekondari moja tu ya serikali, milambo, (tabora boys na girls ni za kitaifa), japo nayo baadae 'o' level ilifutwa. hata shule za kata nyingi mwendo wake ni hoi, msukumo wa wazazi kwa watoto ni duni na vijana wengi hawapendi shule. fursa zipo upande wa kilimo na ufugaji, lakini vijana wenyeji wanapenda starehe kuliko. ni mji wa starehe hasa unywaji na ndio maana grocery ni nyingi kuliko bar.
 
Sisi Tumeanza kuamka mapema sana na Tuliacha woga mapema mno ukiachilia mbali Kina kasanga Tumbo, Kaselabantu ....1995 Urambo ilimchagua mzee wangu mzee Msima alikuwa wa chama cha Upinzan ila alichowafanya hawana hamu
 
maendeleo ya tabora itachukua muda sana, tena kwa msaada mkubwa wa watu wa kuja. maendeleo huletwa na elimu na tabora kabla ya ujio wa shule za kata, mkoa ulikuwa na shule ya sekondari moja tu ya serikali, milambo, (tabora boys na girls ni za kitaifa), japo nayo baadae 'o' level ilifutwa. hata shule za kata nyingi mwendo wake ni hoi, msukumo wa wazazi kwa watoto ni duni na vijana wengi hawapendi shule. fursa zipo upande wa kilimo na ufugaji, lakini vijana wenyeji wanapenda starehe kuliko. ni mji wa starehe hasa unywaji na ndio maana grocery ni nyingi kuliko bar.
Nakubaliana na ww mzee ila kuna Viongozi au wasomi wa juu wengi kuna diaspora wengi sana wapo connected na Tabora ubunifu tu mdogo mdogo wa wabunge wakuu wa mkoa kutembeza bakuli tukapata hata technical school moja tu
 
Back
Top Bottom