Jana nimesimama karibu na duka fulani. Nilikuwa nacheki simu nataka kujua hukumu ya Lissu imekwenda vipi.
Kwa hiyo nimekwenda pale kwenye kivuli( shade) kucheki simu.
Pembeni pale nimeiona noti ya sh elfu kumi.
Nimeichukua Ile noti( baada ya kuhakikisha kwamba ni noti) nimeiweka mfukoni.
Hakuna mtu pale karibu.
Obviously kuna mtu kaiangusha Kwa bahati mbaya.
Kwa hii noti ni yangu sasa.
Ile safari niliyokuwa nakwenda,nikaghairi.
Nikageuza njia kurudi nilikotoka.
Nikaenda barabarani kusimamisha daladala.
Nadhani nilipoiokota noti,within sixty seconds, nilikuwa ndani ya daladala. Nilikuwa na hofu nikizubaa pale,nitasikia makelele ya,"mwizi"
Njia nzima nilikuwa na hofu atatokea mtu kuniita "mwizi."
Halafu baadaye nikafikiria: jambo Gani lilitokea pale? Imekuwaje nimeokota hela pale?
Baada ya kutafakari nikaona kwamba: pale lilikuwepo duka,na yule mtu alikwenda kwenye sala ya Ijumaa,na pale chini alitupa hela,ili kibaka akifika aichukue Ile hela,aliache duka lake salama.
It is that bad,wanatuogopa, wanasema sisi wote ni wezi,wanaweka hela pembeni.
Lakini sasa, ndio hapa watu wanabishana.
Mimi nimeokota hela,nimefurahi sana.
Ndio watu wanasema,kama una hela,mshukuru Mungu.
Acha kusema,"Yule kahaba,yule *****"