Huyu binti, Rachel, yuko vizuri sana, mie namkubali na naamini hajatokea promota mzuri, au producer mzuri aliyefanikiwa kumuona. Sauti anayo nzuri sana, hajapata wa kumuweka vizuri akawa mwanamziki mkubwa. Kila nikimsikia akiimba huwa namkumbuka Mbilia Bel. Naamini akipata bahati ya producer mzuri atafika mbali.