jamani noti fake kwenye atm zinatoka wapi tena!!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jamani noti fake kwenye atm zinatoka wapi tena!!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by white wizard, Apr 19, 2012.

 1. w

  white wizard JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  jana nimekwenda bank ya nmb-temeke,kwenda kuchukua pesa kwenye atm,nilitoa tsh.laki moja cha ajabu wakati nazihesabu nikagundua kuna sh.elfu thelathini(wekundu 3) ni bandia!nikatoka nikaingia ndani kumuona customer manager,nikamuonyesha hizo fedha,cha ajabu anasema haiwezekani kabisa!eti nimekuja nazo!ikabidi niachane nao,na nilipoulizia wa2 wanasema mbona,kwenye atm za nmb ni ki2 cha kawaida sana,hivyo nachelea kusema kwamba mjiadhari kwani huwezi kukwepa na kurudishiwa haiwezekani,ila mimi kuanzia sasa kama nachukua pesa nyingi nitalazimika kwenda kwa teller,japo huwa hawataki nitapambana,kwani cku unaweza kuta laki 2 zote fake c inakuwa balaa!na huu mchezo watakuwa wanaufanya wale wanaoongeza pesa kwenye hizi atm.na zile hela fake nilimrushia meneja.
   
 2. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ungewawashia moto mpaka kwa meneja.
  Wangekupa haki yako
  OTIS
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Tanzania shamba la bibi.
   
 4. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,140
  Likes Received: 859
  Trophy Points: 280

  Kumbe huu mchezo upo kote kote, niliwahi kutoa fedha CRDB ili nikazitume kwenye a/c ya mtu Barcleys. Sikuwa na noti kubwa mfukoni (kwamba ningeweza dhani nimepata kwingine) so nikaenda ATM ya CRDB nikatoa laki na nusu nikazikunjia mfukoni mie huyooo moja kwa moja bank ya Bacleys, kwa uaminifu wangu kwa ATM (kwa wakati huo) kulinifanya nisizikague zile pesa.

  Nilihamaki fedha zimewekwa kwenye kijimashine cha kuhesabia fedha noti moja ya 10,000/ inakataa kabisaa, tela akaichukua na kuniambia ni feki, sikuamini ila ukweli ndo ulikuwa ndiyo huo.

  Vitambulisho na risiti ya ATM ndivyo viliniokoa siku hiyo.

  Ni tabia mbaya sana na ukiingia ndani wanakataa!!! Ila ipo siku
   
Loading...