Jamani nisaidieni maana ya ndoto hii

Jamani nisaidieni maana ya ndoto hii

AMBASSADOR-M

Senior Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
170
Reaction score
83
Salaam wakuu,

Usiku wa manane nimeota ndoto inayonipa maswali mengi kiasi asbuhi ya leo. Kwa kifupi tuu ni kwamba; Nilikuwa na wazazi walipotea katika ulimwengu huu zaidi ya miaka 10 iliyopita. Mama alifariki nikiwa darasa la pili na baba nikiwa darasa la saba.

Usiku huu wa manane nimeota kama nilikokuwa nafanya kazi nimepokea kamshahara kangu kama laki mbili na nusu hivi. Lakini katika mshahara wangu huo nikaamua kuwagawia kiasi watu kadhaa katika familia yangu. Tukiwa chini ya mwembe karibu na tulipokuwa tunaishi, baba alikuwepo na wajukuu wake. Kiasi flani wajukuu walikuwa wamemkwaza baba, akawa amekasirika kwa mda hivi.

Mimi nikiwa katika utaratiibu wangu, nikaamua kuchukua noti ya elfu 10 na ya elfu 5, jumla elfu 15 nikaenda kumpatia baba yangu mkononi huku nikimsisitiza aitumie chochote anachokusudia. Nikashangaa baba anaanza kulia kiasi cha kuona kama nimemuonesha upendo na akanifanya namimi kuanza kulia ghafla, wote tukiwa chini ya mwembe.

Kumbe wakati hayo yakiendelea ilikuwa ni usiku wa mbalamwezi hivi. Baba akanisogeza mahali hivi, akaniambia mwanangu tazama kule. Alikokuwa akinionesha ni makaburini. Akanionesha mama yangu mzazi akiwa ameng'aa kwa mbaali, mbalamwezi imemuangaza. Nikamuona mama ambaye sikumkumbuka muda mrefu kiasi. Mama baada ya kutuona akapotea. kwenye ndoto ilionekana baba alikuwa hai na mama tuu ndiyo alifariki. Baada ya tukio hilo mama akapotea kule kwa mbaali na baba nae akanishukuru na sikumuona tena.

Baada ya muda kidogo nikagutuka toka usingizini na kuanza kutafakari nini maana ya hiyo ndoto. Nimekuwa nikikumbuka ndoto kama hizi mara nyingi huwa na ishara flani hata kama sitoijua. Na ni nadra sana kuota ndoto ya kuwakumbuka wazazi wangu. Inapotekea hivyo huwa na jambo flani.

Labda kama kuna mjuvi tafadhali anipe mwanga kidogo, binafsi bado naona maruweruwe tuu! Natanguliza shukrani na samahani kama nitawakwaza, nawatakia siku na jumapili njema nyote!
 
Watakuja, ila uwe makini. Na matapeli wapo pia. Najua kuna mtu atakwambia baba yako yupo hai, ila jua kuwa akili ya kuambiwa changanya na yako.

Kwangu Mimi naona ni reflection ya mawazo yako tu, Kama ni mkristo nenda church ukaombewe uepuke hayo mawazo ya kukusababishia kuongea na wafu ktk ndoto.
 
asante Mangi flani hivi , nitakuwa makini. lakini huwa sinaga mazoea siku hizi ya kuwawaza wazazi wangu. Ndotoni ni nadra sana kuwaota. But sijui tuu labda ndoto zinapita tuu
 
mshana jr a.k.a Rabbi a.k.a Master a.k.a Mentor a.k.a Teacher a.k.a Guru naomba uje umsaidie kijana.
Binafsi naweza sema unakumbushwa kuwasaidia wengine ambao wana maswahibu kama yako. Wale walio yatima na wahitaji.
Sadaka ni njema hutuepusha na madhira mbalimbali ambayo yalitakiwa yatupate. Kila kitu huanzia rohoni ndio hutokea kwenye mwili. Ili uumwe ugonjwa utaanzia rohoni na baadae ndio mwili utashambuliwa.
 
Nashukuru sana Bujibuji inawezekana hilo pia mkuu. nitalifanyia kazi
 
nimecomment ili nije kufuatilia muendelezo...
 
Salaam wakuu,

Usiku wa manane nimeota ndoto inayonipa maswali mengi kiasi asbuhi ya leo. Kwa kifupi tuu ni kwamba; Nilikuwa na wazazi walipotea katika ulimwengu huu zaidi ya miaka 10 iliyopita. Mama alifariki nikiwa darasa la pili na baba nikiwa darasa la saba.

Usiku huu wa manane nimeota kama nilikokuwa nafanya kazi nimepokea kamshahara kangu kama laki mbili na nusu hivi. Lakini katika mshahara wangu huo nikaamua kuwagawia kiasi watu kadhaa katika familia yangu. Tukiwa chini ya mwembe karibu na tulipokuwa tunaishi, baba alikuwepo na wajukuu wake. Kiasi flani wajukuu walikuwa wamemkwaza baba, akawa amekasirika kwa mda hivi.

Mimi nikiwa katika utaratiibu wangu, nikaamua kuchukua noti ya elfu 10 na ya elfu 5, jumla elfu 15 nikaenda kumpatia baba yangu mkononi huku nikimsisitiza aitumie chochote anachokusudia. Nikashangaa baba anaanza kulia kiasi cha kuona kama nimemuonesha upendo na akanifanya namimi kuanza kulia ghafla, wote tukiwa chini ya mwembe.

Kumbe wakati hayo yakiendelea ilikuwa ni usiku wa mbalamwezi hivi. Baba akanisogeza mahali hivi, akaniambia mwanangu tazama kule. Alikokuwa akinionesha ni makaburini. Akanionesha mama yangu mzazi akiwa ameng'aa kwa mbaali, mbalamwezi imemuangaza. Nikamuona mama ambaye sikumkumbuka muda mrefu kiasi. Mama baada ya kutuona akapotea. kwenye ndoto ilionekana baba alikuwa hai na mama tuu ndiyo alifariki. Baada ya tukio hilo mama akapotea kule kwa mbaali na baba nae akanishukuru na sikumuona tena.

Baada ya muda kidogo nikagutuka toka usingizini na kuanza kutafakari nini maana ya hiyo ndoto. Nimekuwa nikikumbuka ndoto kama hizi mara nyingi huwa na ishara flani hata kama sitoijua. Na ni nadra sana kuota ndoto ya kuwakumbuka wazazi wangu. Inapotekea hivyo huwa na jambo flani.

Labda kama kuna mjuvi tafadhali anipe mwanga kidogo, binafsi bado naona maruweruwe tuu! Natanguliza shukrani na samahani kama nitawakwaza, nawatakia siku na jumapili njema nyote!

POLE KWA KUFIWA NA BABA NA MAMA, CHA KUFANYA ACHA KUWAWAZA, HUWEZI KUWARUDISHA, WAMEPUMZIKA.
 
Hebu nenda hospitali kacheki malaria. Malaria inaletaga ndoto za mawenge sana
 
Kama ni muislamu wazee wanataka uwaombee dua hao na uwatolee sadaka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom